Hayo makeke yake yote anayafanya sababu yupo ccm, lingine ccm ya sasa inamakundi hata kama hayaonekani so inawezekana yeye ni speaker tu walioshika mic (vigogo wa chama) wapo nyuma. Siro kamjibu waziri wa Afya kama vile anamjibu Mnyika, ndio ufahamun kuwa hata Siro anakundi lake linalomtumia.
Ni mweli hata Mimi nimeshangaa sana Siro alivyomtetea Kibwetere wa Tanzania.
Nakumbuka Kule Moshi kuna gaidi wa kidini alimwaga mafuta na kuwashawishi watu kwenda kuyakanyaga kwa spidi kali huku akijua kuwa mafuta yanateleza. Matokeo yake aliua watu zaidi ya 20 na ushee.
Alitoroka na baadae akajipeleka kwenda kujidhamini na kurudi nyumbani kwake . Yani MTU ameua watu 20 kwa mgongo wa dini kama Kibwetere halafu hata mahakamani hakufikishwa ili ushahidi uletwe kuthibitisha kuwa hakuua kwa kukusudia lakini anachukuliwa poa tu kwa sababu in shabiki wa CCM.
Sasa Rais chanjo ni salama ,waziri anasema Chanjo ni salama ,wataalamu na wansayance wanasema chanjo ni salama lakini Gwajima anapinga kwa nguvu zote bila ushahidi wa kitaalam.
Anachanganya watu na kuoyumbisha serikali.
Siro ameonyesha upendeleo wa wazi kwa kada huyu wa CCM alitetumia dini kupinga pinga serikali na nia ya serikali ya kuwakinga watu wake na korona.
Mbowe alikua ana nia tu ya kwenda kwenye kongamano la Kuunga mkono Katiba Mpya iliyoanzishwa kihalali na serikali ya CCM. Lakini akaambiwa kuwa ni Gaidi.
Sasa Gwajima aliyeipinga serikali na Msimamo wa Rais mpaka sasa Siro anamkingia kifua na kusema kuwa hakuna Jinai. Tujiulize wale waliokua wanasali kule Mbeya na Mwanza walifanya Jinai gani kwenye Ibada ?
Je, kumwombea Kiongozi wa Upinzani ni Jinai kubwa kuliko kumpinga Rais kwa sababu ya imani za kidini?
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app