Kumbe biashara ya mahindi mabichi inalipa na wadau mmekaa kimya hamsemi

Kumbe biashara ya mahindi mabichi inalipa na wadau mmekaa kimya hamsemi

jokotinda_Jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2022
Posts
882
Reaction score
1,536
Screenshot_20221229-152546_Instagram.jpg
 
Mkiambiwa mlipe kodi 20,000 kwa mwaka. kama mjasiriamali mnaanza kulia kwamba hampati kitu.

Hapo mnapiga hesabu za mamilioni kwa kuuza mahindi ya kuchoma
 
Hio faida ya 650 umeipataje? Umechukua 800 - 150 sindio? Kwa maana ya kwamba huo mhindi ukinunua shambani unakuwa ushachomwa sindio? Wewe unanunua na kuja kuuza tu. Au hukuwaza hilo, hujui kuna kununua mkaa?

Aliekwambia utauza mahindi 100 kila siku kwa mwaka mzima nani? Mahindi ya kuchoma yanauzika sana kipindi cha mvua, kipindi cha baridi. Katika kipindi hichi unaweza kuuza mahindi 100 kwa siku japo sijawahi fanya huo utafiti kwahiyo sina uhakika sana. Ila kipindi cha joto huwezi kuuza mahindi choma 100 kwa siku labda utumie uchawi.

Swala lingine, ingekuwa biashara ya mahindi choma inaweza kutengeneza faida ya 23M kwa mwaka, wauza mahindi wangekuwa wanauza wakiwa kwenye Range.

Sisemi hio biashara haina faida, faida ipo ndo maana watu wanafanya na maisha yao yanaenda. Mtu anaepata 1.95M kwa mwezi kama faida hata biashara yake utaiona tu, hata yeye mwenyewe utamuona tu.
 
Wamasai wanauza ng'ombe mmoja kwa shilingi 100000.

Mshikaki wa nyama ya ngombe unauzwa shilingi 500.

Ukiuza mishikaki 100000 kwa ng'ombe mmoja unapata faida ya millioni 49.9
Kwahiyo hiyo mishkaki unachomea jua cyo
 
Hio faida ya 650 umeipataje? Umechukua 800 - 150 sindio? Kwa maana ya kwamba huo mhindi ukinunua shambani unakuwa ushachomwa sindio? Wewe unanunua na kuja kuuza tu. Au hukuwaza hilo, hujui kuna kununua mkaa...
Unakatisha tamaa sana mjomba ... kwani hujui huu ni msimu wa mvua boss
 
Biashara inalipa sana hii ukifanya vzr japo sio kwa hayo mahesabu.

Chukulia unatafuta genge unauza mahindi, mishikaki na fastfoods nyingine za kuchoma, usafi 100% unawawekea watu tv hapo wakiwa wanasubiri oda zao.

Ukiwa na vijana wawili watatu na mtaji wa 7M mbona investment nzr tu. Shida watu hufikiria biashara kuubwa kubwa sana
 
Unakatisha tamaa sana mjomba ... kwani hujui huu ni msimu wa mvua boss
Hapana sikatishi tamaa mimi naongea uhalisia. Ndo maana nikasema hio biashara inayo faida, ingekuwa haina faida watu wasingeifanya.

Ila kama tunaona watu wanafanya na maisha yao yanaenda basi faida ipo. ILA HAWAPATI FAIDA KAMA WEWE ULIVYOONESHA KWENYE PROJECTION YAKO

Labda ufungue matawi mbalimbali ndani na nje ya nchi, ya kuuza mahindi ya kuchoma
 
Back
Top Bottom