Kumbe biashara ya mahindi mabichi inalipa na wadau mmekaa kimya hamsemi

Kumbe biashara ya mahindi mabichi inalipa na wadau mmekaa kimya hamsemi

Biashara za kijinga ndio uwa zinalipa ila hapo ongeza bei za usafirishaji na mkaa
Tatizo la watanzania kudharau kazi heti biashara ya kijinga,wengi wakiona watu matajiri udhani hizo mali wazonazo zilishuka toka mbinguni

Walio wajinga baadhi yao uwanza kudharau kazi uwezi kufikia 1000 lazima uanze 1 pia ujitume ujinyime uwe na mrengo vinginevio wenzio watakuwa wanafanya kazi unazo ita za kijinga baadae wanabalisha biashara wanaanza kulia kivulini utawaita wachawi
 
Hio faida ya 650 umeipataje? Umechukua 800 - 150 sindio? Kwa maana ya kwamba huo mhindi ukinunua shambani unakuwa ushachomwa sindio? Wewe unanunua na kuja kuuza tu. Au hukuwaza hilo, hujui kuna kununua mkaa?

Aliekwambia utauza mahindi 100 kila siku kwa mwaka mzima nani? Mahindi ya kuchoma yanauzika sana kipindi cha mvua, kipindi cha baridi. Katika kipindi hichi unaweza kuuza mahindi 100 kwa siku japo sijawahi fanya huo utafiti kwahiyo sina uhakika sana. Ila kipindi cha joto huwezi kuuza mahindi choma 100 kwa siku labda utumie uchawi.

Swala lingine, ingekuwa biashara ya mahindi choma inaweza kutengeneza faida ya 23M kwa mwaka, wauza mahindi wangekuwa wanauza wakiwa kwenye Range.

Sisemi hio biashara haina faida, faida ipo ndo maana watu wanafanya na maisha yao yanaenda. Mtu anaepata 1.95M kwa mwezi kama faida hata biashara yake utaiona tu, hata yeye mwenyewe utamuona tu.
Biashara kweli ya mahindi inalipa lakini inategemea haya mahindi unayachomea sehemu gani?

Ikumbukwe watanzania walio wengi kutafuta pesa wanaweza tatizo ni kutunza kipato kinacho patikana pia wengi wetu huwa tunafanya kazi kwa bidii bila malengo,kazi zote zinalipa itategemea umelenga nini kwenye utafutaji wako
 
Wamasai wanauza ng'ombe mmoja kwa shilingi 100000.

Mshikaki wa nyama ya ngombe unauzwa shilingi 500.

Ukiuza mishikaki 100000 kwa ng'ombe mmoja unapata faida ya millioni 49.9
Duu utanipusua bandama kwa kucheka
 
Back
Top Bottom