Hio faida ya 650 umeipataje? Umechukua 800 - 150 sindio? Kwa maana ya kwamba huo mhindi ukinunua shambani unakuwa ushachomwa sindio? Wewe unanunua na kuja kuuza tu. Au hukuwaza hilo, hujui kuna kununua mkaa?
Aliekwambia utauza mahindi 100 kila siku kwa mwaka mzima nani? Mahindi ya kuchoma yanauzika sana kipindi cha mvua, kipindi cha baridi. Katika kipindi hichi unaweza kuuza mahindi 100 kwa siku japo sijawahi fanya huo utafiti kwahiyo sina uhakika sana. Ila kipindi cha joto huwezi kuuza mahindi choma 100 kwa siku labda utumie uchawi.
Swala lingine, ingekuwa biashara ya mahindi choma inaweza kutengeneza faida ya 23M kwa mwaka, wauza mahindi wangekuwa wanauza wakiwa kwenye Range.
Sisemi hio biashara haina faida, faida ipo ndo maana watu wanafanya na maisha yao yanaenda. Mtu anaepata 1.95M kwa mwezi kama faida hata biashara yake utaiona tu, hata yeye mwenyewe utamuona tu.