Kumbe bilionea Bakhresa na Adani Gautam kuwekeza Tanzania lilikuwa ni hitaji la Hayati Mwl. Nyerere!

Kumbe bilionea Bakhresa na Adani Gautam kuwekeza Tanzania lilikuwa ni hitaji la Hayati Mwl. Nyerere!

Huu uzi mwazoni sikuw nimeuelewa ila baada ya kuurudia vizuri nimeon vile vi-ID vinavyolipwa na Kafulila kuja kupigia debe utapeli wake.

Niwaambie tu siku zote ukiona mkataba unapigiwa sana kelele ufanywe siri jua siku moja ukweli utajulikana.

Leo nchi ina viporo vya kutosha ICSID kwa sababu ya wajinga wachache kutokana na maslahi ya matumbo yao.
Hapo nani kapigiwa chepuo Mzee, Punguza wenge maneno ya Mwl yanaishi kama vile bishana nae
 
So what ? Kila kitu kinahitaji na kinategemea mazingira na kama kuna transparency hakuna kitu kitafanya vibaya..., ngoja nikupe mfano wa PPPs katika uhalisia na ubora wake..., mfano kuna shida ya usafiri wa kwenda huko kijijini..., Serikali haina pesa wala mpango wa kutengeneza hio Barabara anakuja mtu binafsi anasema mimi hapa naweza kujenga barabara na mapato ya kupita hapa takuwa nachukua kama faida kwa miaka thelasini baada ya hapo barabara inakuwa ya serikali (Serikali inatoa ardhi ambayo ingeendelea kuwa pori ila after 30 years inakuwa yake) na mtu anapata faida kulingana na alivyoona kwamba kuna need....

Ila uhalisia kwa Afrika na kwingineko watu wanaingia mikataba ya ajabu na hata jambo ambalo Serikali ingeweza kufanya au ilikuwa inafanya mtu anakopea hio asset ya serikali na anafanya (mwisho wa siku akipata hasara au ikienda ndivyo sivyo anapewa ruzuku kwa kodi ya serikali ili aendelee kula) au mradi unakuwa white elephant wenye madeni unaishia kupigwa mnada kwa bei ndogo na walewale wananunua..., In short PPPs ina loopholes kibao za upigaji

Ni wapi PPP haijaonesha transparency?
 
Ni wapi PPP haijaonesha transparency?
Hivi unajua hata unachoongelea ? Ukishaweka watu Binafsi / Sekta Binafsi hakuna tena transparency wala uwezo wa serikali kuchunguza nitty gritty (kuna vitu vinafichwa kwa mgongo wa siri zao za kibiashara) hio ndio moja ya loopholes....

  • PPPs originated as an accounting trick, a way round the government’s own constraints on public borrowing. This remains the overwhelming attraction for governments and international institutions. Just as companies like Enron had tried to conceal their true liabilities by moving them‘off-balance-sheet’, so governments started using PPPs as “tricks…. whereby public accounts imitate the creative accounting of some companies in the past.”
  • “In developing countries, the development banks and multinational companies encouraged the spread of PPPs in the 1990s, especially in the water and energy sectors, as part of the general promotion of privatisation – and as a way around the fiscal limits which the same IFIs were imposing on developing countries. The main form of privatisation in water was concessions or lease contracts, which are a classic form of PPP.”
  • Governments have also started providing subsidies for PPPs, mainly by lending public money at low rates of interest that the private sector could not otherwise obtain – despite the obvious intrinsic contradiction of using public finance to finance PPPs.
  • A further danger is the recent effort by the World Bank,the G20, OECD and others to ‘financialize’ PPPs in order to access the trillions of dollars held by pension funds,insurance companies and other institutional investors.
  • Although PPPs are often promoted as a solution for countries under fiscal constraints, the evidence suggests rather that they worsen fiscal problems. According to the EIB, the six countries which have made the greatest use of PPPs in recent years are Cyprus, Greece, Ireland, Portugal, Spain and the UK. Four of these are subject to ‘Troika’ rescue packages, and the other two – Spain and the UK – both face large fiscal problems. In both Portugal and Cyprus, the IMF/EU ‘troika’ packages have identified PPPs as a contributory cause of the countries’ fiscal problems, and required an audit and renegotiation of existing PPPs and a freeze on new PPPs.
 
Unataka kushauri Nini?
IMG_7634.jpeg

☝️Unafahamu ya kuwa huo ndio msingi wetu wa kumpa DPW bandari.

Sasa mpaka sasa ni kipi kipo kwenye harakati za uwekezaji uliotajwa hapo.

Huo upuuzi hata kwenye report ya CAG mwakani utaukuta ya kuwa Mwarabu hakuna la maana aliloleta.

Mimi sipingi uwepo wa DPW Iła what’s the return na justification ya kupewa bandari kwa miaka 30.
 
Nani amethibitisha hoja ya rushwa kwa Adani?
Sio Siri Adani anajulikana kwa kutoa Mlungula hilo lipo wazi na sio Adani tu Kampuni nyingi duniani zinafanya hivyo hata sakata la RADA na BAE au BAE na nchi za Kiarabu Mlungula wa kufa mtu ulitoka..., Ingawa hio sio issue sana hapa ila tujiulize huyu Dalali anafanya hivyo sababu Mikataba ina umuhimu kwa nchi au anafanya hivyo kwa Mlungula aliopewa (kama amepewa)..., Sababu tunajua kuhusu suala la Sekta ya UMEME ADANI amefanya worse kwa nchi husika (refer Bangladesh)

Nani amethibitisha hoja ya rushwa kwa Adani?

Wizara ya Sheria ya Marekani imemu indict Adani na kumuanzishia kesi. Wizara ya Sheria ya Marekani hai indict watu ovyo ovyo tu bila ya kuwa na serious case.

View: https://youtu.be/CEGxkO-IGcQ?si=RsHqQ-wYZ7x9p1Ly

Hivi unajua hata unachoongelea ? Ukishaweka watu Binafsi / Sekta Binafsi hakuna tena transparency wala uwezo wa serikali kuchunguza nitty gritty (kuna vitu vinafichwa kwa mgongo wa siri zao za kibiashara) hio ndio moja ya loopholes....

  • PPPs originated as an accounting trick, a way round the government’s own constraints on public borrowing. This remains the overwhelming attraction for governments and international institutions. Just as companies like Enron had tried to conceal their true liabilities by moving them‘off-balance-sheet’, so governments started using PPPs as “tricks…. whereby public accounts imitate the creative accounting of some companies in the past.”
  • “In developing countries, the development banks and multinational companies encouraged the spread of PPPs in the 1990s, especially in the water and energy sectors, as part of the general promotion of privatisation – and as a way around the fiscal limits which the same IFIs were imposing on developing countries. The main form of privatisation in water was concessions or lease contracts, which are a classic form of PPP.”
  • Governments have also started providing subsidies for PPPs, mainly by lending public money at low rates of interest that the private sector could not otherwise obtain – despite the obvious intrinsic contradiction of using public finance to finance PPPs.
  • A further danger is the recent effort by the World Bank,the G20, OECD and others to ‘financialize’ PPPs in order to access the trillions of dollars held by pension funds,insurance companies and other institutional investors.
  • Although PPPs are often promoted as a solution for countries under fiscal constraints, the evidence suggests rather that they worsen fiscal problems. According to the EIB, the six countries which have made the greatest use of PPPs in recent years are Cyprus, Greece, Ireland, Portugal, Spain and the UK. Four of these are subject to ‘Troika’ rescue packages, and the other two – Spain and the UK – both face large fiscal problems. In both Portugal and Cyprus, the IMF/EU ‘troika’ packages have identified PPPs as a contributory cause of the countries’ fiscal problems, and required an audit and renegotiation of existing PPPs and a freeze on new PPPs.
Hii ni irreverent kabisa
 
Wanaopinga Ubia wengi wao ni wapigaji nia yao miradi ibaki serikalini ili waendelee kutupiga😂😂

Ova!
Ni jambo zuri lakini utekelezaji wake sasa, utasikia wabia hao hao ni wanasiasa hao hao nyuma ya migongo ya wafanyabiashara wa asia wakitumia pesa ya serikali hiyo hiyo yenyewe, kushirikiana kwa miradi hiyo hiyo. Yani wanasiasa wataingia ubia na serikali, na kuwekeza pesa ya serikali wale percent huku in reality watakuwa hawajawekeza kitu.
Subiri hapa utaona. Hii ndiyo Tanzania a.k.a Afrika.
 
View attachment 3169359

Tofauti sana na watu wengi walivyofikiri kuwa Hayati Mwl JK. Nyerere hakutaka sekta binafsi PPP, Hii si kweli,

Ukweli wa wazi MwL JK. Nyerere aliamini zaidi katika sekta binafsi kuwa ni ndio msingi pekee wa kuleta mtaji na zaidi sana kuchochea ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa Serikali yake Leo ni zaidi ya miaka sitini (60) imepita mawazo ya Mzee huyu yanaingia katika utekelezwaji rasmi.

Kwa msiofahamu moja ya jambo ambalo Mzee huyu alilikiri hadharani tena Waziwazi kufanya makosa katika awamu yake ni kupoka Mali za sekta binafsi kama Mashamba ya mkonge, Pamba, Kahawa kutoka sekta binafsi na kuyarudisha Serikalini, hili lilikuwa ni kosa kubwa la kiufundi mtakumbuka kabla ya hiki Tanzania tulikuwa ndio vinara wa Mkonge duniani leo majibu sote tunayo.

Swala jingine ambalo Mzee alijutia baada ya kung'atuka madarakani ni kuufanya ushirika uendeshwe na Serikali badala ya kujiendesha wenyewe kama sekta binafsi nadhani madhara haya hata Leo bado yanaonekana.

Wakati flani nikimkumbuka Hayati Mwl JK Nyerere, nikikumbuka maono yake hasa haya ya Ubia huwa napata faraja sana ninapomwona Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akipita mulemule na hii ni baada ya miaka 60 kupita Leo hakika hakuna kama Samia.

Hoja fikirishi zaidi kwa wasomaji wangu, "Kama Muasisi wa Taifa hili hakuwa na Wasiwasi juu ya wahindi wala Wapemba au Wawekezaji wengine wowote wazawa wa Ubia nyie wengine hofu yenu mnaitoa wapi juu ya hii PPP kama sio kutuchelewesha kama Taifa?"
Umeitumia vibaya hiyo clip.

Tatizo kubwa aliliokuwa akilizungumzia Nyerere ni suala la ubaguzi wa ndani ya nchi uliojitokeza kwa nguvu katika utawala wa awamu ya pili ya AH Mwinyi baada ya milango ya sekta binafsi katika uwekezaji na PPP ilipofunguliwa. Viongozi wengi walianza kusisitiza UZAWA katika fursa za ubinafsishaji, PPP, na uwekezaji katika sekta nyeti. Kwamba Watanzania waafrika (weusi) (Wazawa) wapewe kipaumbele badala ya wenye asili ya Asia. Hilo ndilo lililomuudhi sana Nyerere. Kama ilivyokuwa kwa suala la muungano (kuwabagua Wazanzibari) enzi za G 55.

Hii kudai alipenda sekta binafsi na hasa PPP - na hao kina Adani na Bakhresa ni kuingiza porojo kwa kutumia hiyo clip iliyofupishwa ya Nyerere bila kusoma maudhui yote ya hotuba yake.

Enzi za JKN (awamu ya kwanza) hakutaka kabisa kusikia mambo ya sekta binafsi, PPP, wala ushiriki wa watumishi wa umma katika uwekezaji, n.k. Azimio la Arusha ndilo lilikuwa blueprint yake kuhusu sera za uchumi na utumishi wa umma. Ndio sababu ya yeye kutokuwa tayari kusaini mkataba na IMF. LAKINI akakubali mrithi wake, AH Mwinyi, asaini na apokee yote hayo na kuyatekeleza.

Ikumbukwe pia Nyerere ndiye aliyeua ufanisi (management) katika vyama vya ushirika na mashirika ya umma kwa kusisitiza kigezo cha ukada wa CCM katika ajira za CEOs na bodi za taasisi hizo. Na Rais (Mwenyekiti wa CCM) kuwa na madaraka ya kuidhinisha na kufuta ajira za watendaji wakuu wa taasisis hizo. Pia serikali za mitaa aliziweka chini ya mamlaka ya serikali kuu moja kwa moja na kuziondolea uhuru ziliokuwa nao wa utendaji katika maeneo yao.

Ni vyema kwamba alikiri makosa yote BAADA YA KUSTAAFU (Tujisahihishe). But it was too late. Legacy yake inaumiza taifa hadi leo. Hiyo clip ndiyo jinsi JKN alivyokuwa akiongea baada ya kustaafu hasa anapokosoa mambo anayoona hayaendi vyema chini ya utawala wa Mwinyi na baadaye kidogo chini ya Mkapa.
 
Lakini walau alitambua ukweli wa mambo
Alikuwa raisi for more than 20yrs,

Tena kulikiwa hakuna vyombo vya habari wala mitandao, so kila kitu alichotaka kufanya alifanya bila kupingwa wala kelele

Kama kuna kitu hakufanya ni kwa sababu alitaka kisifanyike.

So malalamiko yake baada ya kustaafu ni kujikosha tu, hamaanishi alichokuwa anakisema.

Note: alifanya mengi mazuri, Asifiwe kwa mazuri yake ila asiachwe kusemwa kwa mabaya yake.
 
Back
Top Bottom