Kumbe bilionea Bakhresa na Adani Gautam kuwekeza Tanzania lilikuwa ni hitaji la Hayati Mwl. Nyerere!

Kumbe bilionea Bakhresa na Adani Gautam kuwekeza Tanzania lilikuwa ni hitaji la Hayati Mwl. Nyerere!

View attachment 3169472

☝️Unafahamu ya kuwa huo ndio msingi wetu wa kumpa DPW bandari.

Sasa mpaka sasa ni kipi kipo kwenye harakati za uwekezaji uliotajwa hapo.

Huo upuuzi hata kwenye report ya CAG mwakani utaukuta ya kuwa Mwarabu hakuna la maana aliloleta.

Mimi sipingi uwepo wa DPW Iła what’s the return na justification ya kupewa bandari kwa miaka 30.
Fuatilia mapato ya Bandari kabla na wakati wa DPW
 
Alikuwa raisinfor more than 20yrs,

Tena kulikiwa hakuna vyombo vya habari wala mitandao, so kila kitu alichotaka kufanya alifanya bila kupigwa wala kelele

Kama kuna kitu hakufanya ni kwa sababu alitaka kisifanyike.

So malalamiko yake baada ya kustaafu ni kujikosha tu, hamaanishi alichokuwa anakisema.

Note: alifanya mengi mazuri, Asifiwe kwa mazuri yake ila asiachwe kusemwa kwa mabaya yake.
Marehemu huwa hasemwi kwa mabaya
 
Umeitumia vibaya hiyo clip.

Tatizo kubwa aliliokuwa akilizungumzia Nyerere ni suala la ubaguzi wa ndani ya nchi uliojitokeza kwa nguvu katika utawala wa awamu ya pili ya AH Mwinyi baada ya milango ya sekta binafsi katika uwekezaji na PPP ilipofunguliwa. Viongozi wengi walianza kusisitiza UZAWA katika fursa za ubinafsishaji, PPP, na uwekezaji katika sekta nyeti. Kwamba Watanzania waafrika (weusi) (Wazawa) wapewe kipaumbele badala ya wenye asili ya Asia. Hilo ndilo lililomuudhi sana Nyerere. Kama ilivyokuwa kwa suala la muungano (kuwabagua Wazanzibari) enzi za G 55.

Hii kudai alipenda sekta binafsi na hasa PPP - na hao kina Adani na Bakhresa ni kuingiza porojo kwa kutumia hiyo clip iliyofupishwa ya Nyerere bila kusoma maudhui yote ya hotuba yake.

Enzi za JKN (awamu ya kwaza) hakutaka kabisa kusikia mambo ya sekta binafsi, PPP, wala ushiriki wa watumishi wa umma katika uwekezaji, n.k. Azimio la Arusha ndilo lilikuwa blueprint yake kuhusu sera za uchumi na utumishi wa umma. Ndio sababu ya yeye kutokuwa tayari kusaini mkataba na IMF. LAKINI akakubali mrithi wake, AH Mwinyi, asaini na apokee yote hayo na kuyatekeleza.

Ikumbukwe pia Nyerere ndiye aliyeua ufanisi (management) katika vyama vya ushirika na mashirika ya umma kwa kusisitiza kigezo cha ukada wa CCM katika ajira za CEOs na bodi za taasisi hizo. Na Rais (Mwenyekiti wa CCM) kuwa na madaraka ya kuidhinisha na kufuta ajira za watendaji wakuu wa taasisis hizo. Pia serikali za mitaa aliziweka chini ya mamlaka ya serikali kuu moja kwa moja na kuziondolea uhuru ziliokuwa nao wa utendaji katika maeneo yao.

Ni vyema kwamba alikiri makosa yote BAADA YA KUSTAAFU (Tujisahihishe). But it was too late. Legacy yake inaumiza taifa hadi leo. Hiyo clip ndiyo jinsi JKN alivyokuwa akiongea baada ya kustaafu hasa anapokosoa mambo anayoona hayaendi vyema chini ya utawala wa Mwinyi na baadaye kidogo chini ya Mkapa.
Unataka kumaanisha Nyerere hakuruhusu Privatization?
 
Ni jambo zuri lakini utekelezaji wake sasa, utasikia wabia hao hao ni wanasiasa hao hao nyuma ya migongo ya wafanyabiashara wa asia wakitumia pesa ya serikali hiyo hiyo yenyewe, kushirikiana kwa miradi hiyo hiyo. Yani wanasiasa wataingia ubia na serikali, na kuwekeza pesa ya serikali wale percent huku in reality watakuwa hawajawekeza kitu.
Subiri hapa utaona. Hii ndiyo Tanzania a.k.a Afrika.
Hii Sasa ndio mbaya kama kwa hao wanasiasa
 
Ni jambo zuri lakini utekelezaji wake sasa, utasikia wabia hao hao ni wanasiasa hao hao nyuma ya migongo ya wafanyabiashara wa asia wakitumia pesa ya serikali hiyo hiyo yenyewe, kushirikiana kwa miradi hiyo hiyo. Yani wanasiasa wataingia ubia na serikali, na kuwekeza pesa ya serikali wale percent huku in reality watakuwa hawajawekeza kitu.
Subiri hapa utaona. Hii ndiyo Tanzania a.k.a Afrika.
Hii Sasa ndio mbaya kama kwa hao wanasiasa nao watamiliki miradi
 
View attachment 3169359

Tofauti sana na watu wengi walivyofikiri kuwa Hayati Mwl JK. Nyerere hakutaka sekta binafsi PPP, Hii si kweli,

Ukweli wa wazi MwL JK. Nyerere aliamini zaidi katika sekta binafsi kuwa ni ndio msingi pekee wa kuleta mtaji na zaidi sana kuchochea ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa Serikali yake Leo ni zaidi ya miaka sitini (60) imepita mawazo ya Mzee huyu yanaingia katika utekelezwaji rasmi.

Kwa msiofahamu moja ya jambo ambalo Mzee huyu alilikiri hadharani tena Waziwazi kufanya makosa katika awamu yake ni kupoka Mali za sekta binafsi kama Mashamba ya mkonge, Pamba, Kahawa kutoka sekta binafsi na kuyarudisha Serikalini, hili lilikuwa ni kosa kubwa la kiufundi mtakumbuka kabla ya hiki Tanzania tulikuwa ndio vinara wa Mkonge duniani leo majibu sote tunayo.

Swala jingine ambalo Mzee alijutia baada ya kung'atuka madarakani ni kuufanya ushirika uendeshwe na Serikali badala ya kujiendesha wenyewe kama sekta binafsi nadhani madhara haya hata Leo bado yanaonekana.

Wakati flani nikimkumbuka Hayati Mwl JK Nyerere, nikikumbuka maono yake hasa haya ya Ubia huwa napata faraja sana ninapomwona Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akipita mulemule na hii ni baada ya miaka 60 kupita Leo hakika hakuna kama Samia.

Hoja fikirishi zaidi kwa wasomaji wangu, "Kama Muasisi wa Taifa hili hakuwa na Wasiwasi juu ya wahindi wala Wapemba au Wawekezaji wengine wowote wazawa wa Ubia nyie wengine hofu yenu mnaitoa wapi juu ya hii PPP kama sio kutuchelewesha kama Taifa?"
Sasa nimemwamini zaidi Kafulila,Hongera sana kufuata nyayo za Baba wa Taifa.
 
Hivi unajua hata unachoongelea ? Ukishaweka watu Binafsi / Sekta Binafsi hakuna tena transparency wala uwezo wa serikali kuchunguza nitty gritty (kuna vitu vinafichwa kwa mgongo wa siri zao za kibiashara) hio ndio moja ya loopholes....

  • PPPs originated as an accounting trick, a way round the government’s own constraints on public borrowing. This remains the overwhelming attraction for governments and international institutions. Just as companies like Enron had tried to conceal their true liabilities by moving them‘off-balance-sheet’, so governments started using PPPs as “tricks…. whereby public accounts imitate the creative accounting of some companies in the past.”
  • “In developing countries, the development banks and multinational companies encouraged the spread of PPPs in the 1990s, especially in the water and energy sectors, as part of the general promotion of privatisation – and as a way around the fiscal limits which the same IFIs were imposing on developing countries. The main form of privatisation in water was concessions or lease contracts, which are a classic form of PPP.”
  • Governments have also started providing subsidies for PPPs, mainly by lending public money at low rates of interest that the private sector could not otherwise obtain – despite the obvious intrinsic contradiction of using public finance to finance PPPs.
  • A further danger is the recent effort by the World Bank,the G20, OECD and others to ‘financialize’ PPPs in order to access the trillions of dollars held by pension funds,insurance companies and other institutional investors.
  • Although PPPs are often promoted as a solution for countries under fiscal constraints, the evidence suggests rather that they worsen fiscal problems. According to the EIB, the six countries which have made the greatest use of PPPs in recent years are Cyprus, Greece, Ireland, Portugal, Spain and the UK. Four of these are subject to ‘Troika’ rescue packages, and the other two – Spain and the UK – both face large fiscal problems. In both Portugal and Cyprus, the IMF/EU ‘troika’ packages have identified PPPs as a contributory cause of the countries’ fiscal problems, and required an audit and renegotiation of existing PPPs and a freeze on new PPPs.
Hii umeisoma na kuielewa vizuri?
 
Alikuwa raisinfor more than 20yrs,

Tena kulikiwa hakuna vyombo vya habari wala mitandao, so kila kitu alichotaka kufanya alifanya bila kupigwa wala kelele

Kama kuna kitu hakufanya ni kwa sababu alitaka kisifanyike.

So malalamiko yake baada ya kustaafu ni kujikosha tu, hamaanishi alichokuwa anakisema.

Note: alifanya mengi mazuri, Asifiwe kwa mazuri yake ila asiachwe kusemwa kwa mabaya yake.
Unafahamu kuwa walioko nje ya uwanja wanafahamu mpira zaidi ya wanaocheza?

Acheni Mzee apumzike kwa amani
 
Enzi za Nyerere ubia ulikuwa wa haki pande zote tofauti na ubia unaoingiwa kipindi hiki Cha awamu ya mama Samia ambapo mwekezaji wa nje hunufaika zaidi kuliko Nchi yetu nzuri ya Tanzania.Anataka wajukuu wetu wasikute chochote
Roho ya uoga na umaskini inakusumbua. Kina Bill Gates na Dangote wasingefika walipo sasa kama wangeuendekeza uoga ambao ni sifa ya maskini dunia nzima.
 
View attachment 3169359

Tofauti sana na watu wengi walivyofikiri kuwa Hayati Mwl JK. Nyerere hakutaka sekta binafsi PPP, Hii si kweli,

Ukweli wa wazi MwL JK. Nyerere aliamini zaidi katika sekta binafsi kuwa ni ndio msingi pekee wa kuleta mtaji na zaidi sana kuchochea ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa Serikali yake Leo ni zaidi ya miaka sitini (60) imepita mawazo ya Mzee huyu yanaingia katika utekelezwaji rasmi.

Kwa msiofahamu moja ya jambo ambalo Mzee huyu alilikiri hadharani tena Waziwazi kufanya makosa katika awamu yake ni kupoka Mali za sekta binafsi kama Mashamba ya mkonge, Pamba, Kahawa kutoka sekta binafsi na kuyarudisha Serikalini, hili lilikuwa ni kosa kubwa la kiufundi mtakumbuka kabla ya hiki Tanzania tulikuwa ndio vinara wa Mkonge duniani leo majibu sote tunayo.

Swala jingine ambalo Mzee alijutia baada ya kung'atuka madarakani ni kuufanya ushirika uendeshwe na Serikali badala ya kujiendesha wenyewe kama sekta binafsi nadhani madhara haya hata Leo bado yanaonekana.

Wakati flani nikimkumbuka Hayati Mwl JK Nyerere, nikikumbuka maono yake hasa haya ya Ubia huwa napata faraja sana ninapomwona Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akipita mulemule na hii ni baada ya miaka 60 kupita Leo hakika hakuna kama Samia.

Hoja fikirishi zaidi kwa wasomaji wangu, "Kama Muasisi wa Taifa hili hakuwa na Wasiwasi juu ya wahindi wala Wapemba au Wawekezaji wengine wowote wazawa wa Ubia nyie wengine hofu yenu mnaitoa wapi juu ya hii PPP kama sio kutuchelewesha kama Taifa?"

Tuache ujinga wa kumfananisha ndugu yetu mzalendo Salim Bakhresa na Billionaire mtoa rushwa Adani Gautam. Hii sio sawa. Huyu Mzawa ni kati ya walipa kodi wakubwa , pamoja na utajiri hana kashfa yeyote ya rushwa na hatoi rushwa kwa yeyote. Tumebaki kusifia wanasiasa ambao wala rushwa, mikataba ya siri, wezi wa kura na kututeka wapinzani na kuacha wawekezaji wazawa kama Bakhresa na kuwachukulia powa!​

Back
Top Bottom