Kumbe Diamond ana nyodo kiasi hiki

Kumbe Diamond ana nyodo kiasi hiki

sasa tatizo ni kuwa alikuwa maskini au?
Afadhali yake alikuwa maskini akaukataa umaskini akapga kazi mpaka amefika level ambayo anaweza jipangia gharama za show zake.
Mpongeze kuwa wema kipindi anakuwa miss tz asingeweza kumkubari jamaa alikuwa kapgika lakini kwa juhudi leo anamlilia jamaa wewe ambaye hukuwa umepgika kama diamond bado uko vile vile.
Kuimba ndiyo bidhaa anayouza mziki ni biashara usitake alete usela kwenye biashara.
Hayo mengine ni minor problems.

Umemaliza! Yaani Kosa ni kuwa masikini halafu kwa bidii yake mwenyewe kutajirika ni kosa kubwa sana. Kwa Tanzania, Ukizaliwa Tandale uzeekee Tandale wewe ndio shujaa!Kijana kama Diamond ni muhanga wa hao/ baadhi ya mabinti I am telling you! inawezekana kwa hali aliyofikia anajitahidi sana hata kuepuka hivyo vishawishi nina uhakika ni vingi! Kwa munaomsema mwekeni kwenye maombi Mungu amsaidie kuepuka vishawishi. Mi kuna mtu wangu wa karibu ( sitaki kusema uhusiano wake kwangu) namuhubiria kila siku na kumwambia: anatakiwa awe na misimamo kwa sababu quality alizonazo ndio zinapendwa na oposite sex wengi, sitetei ufuska lakini kuna watu wanaqualities ni upako tu wa Mungu unaweza kumsaidia. Kun thread hapa ililetwa ya Kijana anamwambia Obama asimsemeshe girlfriend wake! Jamani kuna watu wana qualities mpaka unawaonea huruma ya jinsi wanavojitahidi kukabiliana na oposite sex!
 
Aiseee wanambeya mkiisema hiyo ya mbeya nakumbuka kua kuna lifti moja tu naumia mbavu, ila Diamond anaongelewa yaan mnampa umaarufu mara zoteeee

Nyie hamjawah kusema kua kitu flan hakina hadhi au mmemnyooshea kidole Ndomo tu heloooo mtaumwaa sana

Wewe ndio walewale...hiyo lift I unaona issue sana eeh??wewe hapo nyumbani kwako unayo hadi uiseme mbeya nzima hamna???
 
kwenye hii issue ya diamond kila member wa jf atafungua thread. Nahisi pple walikua wanatamani kuanzisha thread zao ila walikua hawana topic hahaha wengne tuwe tunachangia tu since yaliyoandikwa yote
yameshadiscusiwa humu.
 
Makavu Ya Leo: Masikini Akipata ------ Hulia Mbwata, bwana mdogo Diamond mtoto wa Tandale ambae wakati Wema Sepetu anakuwa miss yeye alikuwa anauza mitumba kule Tandale kapata pesa sasa naona makalio yake yanalia Mbwata. Kama unampenda sana Diamond usipanic endelea kusoma utanielewa tu
Diamond amewakera mashabiki ndio maana yamemkuta yale yaliomkuta pale Leaders. Kijana Diamond alikuwa moja kati ya watu masikini sana nchini, alikuwa ANALALA kwenye mazingira magumu ila leo amediriki kusema kuwa MBEYA HAKUNA HOTELI YENYE HADHI YAKE, hahahaa inachekesha sana. Anasahau kuwa umaarufu wake umekuja kwasababu mashabiki WALIAMUA kumkubali.

Wema Sepetu wakati ana make headlines akiwa Miss Tanzania hakuwa anatambua kuwa pale mitaa ya Tandale kuna kijana anaitwa Nassibu anauza mitumba, na ninaamini hata kama angeonana na Diaomnd kipindi kile HAKIKA asingemuangalia mara mbili. Ila dogo leo kapata hela anaanza kuleta dharau kwa mashabiki. Dogo ana kauli chafu sana, anapenda kujikweza. Ukitaka ufanikiwe na ufaidi kuwa msanii bongo hakikisha UNAWAFURAHISHA mashabiki wako mdogo wangu. Waache watu wakusifie wewe. Kitu ambacho hujui ni kwamba hapa bongo kulikwa na wasanii wakubwa kama akina Mr. Nice lakini walilewa sifa na sasa wanaishia kucheza pool pale sinza ambiance na kutia huruma. Usipoangalia wewe na kaka yako Nice mtaakaa kijiwe kimoja na kusema ZAMANI NILIKUWA MAARUFU.

Diamond umekuwa na tabia ya kusema wewe ni maarufu na kukataa mara kadhaa (HATA UKIOMBWA) kufanya show sehemu mbali mbali, unajiona ni msanii wa kufanya SHOO ZA MILL 30, kuna cases kadhaa za wewe kuwatolea nje mashabiki kufanya shoo eti kwa madai unataka hela nyingi. Unasahau watanzania hawa hawa ndio waliokupigia kura ukapata hizo tuzo na kuwa nominated hata kwenye hizo BET, lakini naona sasa UMEUCHOKA umaarufu wako na uko tayari kuupoteza kwa upuuzi tu usio wa maana.

Kuna mambo mengi sana unakosea kama binadamu ila kuna mengi unayafanya makusudi kwasababu wewe ni LIMBUKENI, kwa mfano suala la kutoka na mabinti kadhaa wa kadhaa kwako umeona kama ni ufahari hivi, kumbe wenzako wanakuona zuzu tu cuz huwezi kuwamaliza mabinti wote duniani. Na kwasababu hiyo ndio maana wanaume wenye akili WAMEMUHONGA WEMA GARI wakasingizia kuwa ni Kadinda ndie alietoa, ukiacha dharau watu watakuheshimu.

Sijui niendelee au niishie hapa?! Aah nikiishia hapa ntakuwa nimekuogopa. Mdogo wangu wewe kimziki sio kwamba uko juu sanaaaa kuliko Alikiba, Linex, Barnaba, Ben Paul au hata lady jaydee ni kwamba umepata promo nyingi sana kiasi cha mashabiki KUAMUA kukukubali. Unashangaa watu pale leaders waliamua kukuzomea ni kwasababu watanzania wamechoka na majivuno yako na dharau. Sasa T.I anataka kufanya collabo na Ali Kiba ile inaonyesha dhahiri kuwa wewe BADO. Anyways kama umemaindi poa ila hayo ni maoni yangu kama SHABIKI na ungekuwa wewe ni chama cha siasa hakika leo ningerudisha kadi yangu ya Uanachama mpaka pale utakapojirekebisha!

Usije ukakonda bure kwa makavu haya. La mwisho Gwanda zile zitakuletea matatizo, inawezekana ulionywa hukusikia jaribu tena uone cha mtema kuni. Next time hutaitwa Oysterbay watakuficha wenye nazo!

Umeshupaa na kutoa povu jingi mdomoni lakini ulichokiandikia ni upuuuzi na upuumbavu mtupu kwani hakuna kitu hapo. Wahenga walisema "mtu mpu.mbavu akikaa kimya huwezi kuujua upumba.vu wake mpaka akiongea" pekee nilichokisoma hapo ni kuwa maelezo yako yamejaa chuki, wivu wa kike , tamaa na roho mbaya.

Swala la Diamond kutokea katika maisha ya kimasikini au dhiki kama unavyosema wewe ingawa huna data zozote za kuthibitisha hilo si jambo la ajabu sana duniani. Tumeona historia za wasanii na wanamichezo na hata wafanyabiashara wakubwa mbalimbali zikielezea jinsi maisha yao yalivyokuwa kabla ya kupata mafanikio kimaisha na ukiangalia wanavyoishi sasa ni tofauti. Haimaanishi kama umetoka katika umasikini basi uendelee kuishi kimasikini labda kwa mtu mwenye umasikini wa kimawazo kama ulivyo wewe. Kwa level ya kimafanikio aliyofikia Diamond si ubishi kwamba yupo katika level za kimataifa na lazima alinde hadhi yake aliyokuwa nayo ili aendelee kuongeza heshima yake na kubwa zaidi kuongeza thamani ya kazi zake na kujipatia fedha nyingi zaidi.

Kubali au kataa Diamond siyo wa kumualika katika vitamasha vya vichochoroni vya kiingilio chupa ya pombe na yeye aende huko ni kujishusha hadhi na kuharibu soko la kazi zake. Alafu hicho kinachotokea sio yeye bali ni nguvu ya soko kwani principle za demand and supply zinasema wazi " the higher the demand the higher the price" sasa demand ya Diamond ipo juu sana hivyo lazima na bei yake nayo iwe juu sana vile vile.

Ali Kiba anajitahidi kuimba lakini ni upumbavu kudhani kwamba unaweza kuiongeza thamani ya Ali Kiba kwa kulazimisha kuishusha thamani ya Diamond.

Sisi washabiki wa Diamond wala hatukasiriki jinsi kijana anavyoringia talent yake kwani ile resource ya thamani kubwa aliyokuwa nayo na lazima aringie ni sawa na Daktari Bingwa anapotaka mshahara mkubwa kwa kuringia elimu yake au Prof. Anapotaka chuo kimlipe fedha nyingi na yupo tayari kufundisha vyuo vyenye hadhi na majina makubwa anaringia taaluma yake. Kwanini unataka Diamond ajitoe bure tu.

Kuhusu mapenzi yake na Wema hayo ni maswala binafsi sana na yanahusu mapenzi siyo kazi. Sasa wewe ulitaka aje kukuoa wewe?

Mwisho nakushauri kama unataka utajiri fanya kazi kwa bidii kwani chuki au tamaa au wivu wa kike hautokusaidia kitu.
 
Wewe ndio walewale...hiyo lift I unaona issue sana eeh??wewe hapo nyumbani kwako unayo hadi uiseme mbeya nzima hamna???

Samahani nifah unaishi Mbeya, !!!pole sanaa
 
Last edited by a moderator:
chura dume hata heshima niliyokuwa nampa dada mleta mada imekwisha;
Ameonesha moja kwa moja chuki yake ilivyo, naona hao ni lile kundi la zomea zomea;

Hawajui aliye juu mfuate huko huko, wao wanabaki chini huku wakilenga mawe juu kwa mnati.

Ni kweli kabisa@ Mamndenyi. Yaani wao wanataka kumpandisha msanii kwa kutumia kumdhalilisha yule anayefanya juhudi zake binafsi
 
Last edited by a moderator:
Aiseee wanambeya mkiisema hiyo ya mbeya nakumbuka kua kuna lifti moja tu naumia mbavu, ila Diamond anaongelewa yaan mnampa umaarufu mara zoteeee

Nyie hamjawah kusema kua kitu flan hakina hadhi au mmemnyooshea kidole Ndomo tu heloooo mtaumwaa sana

Anajitahidi kuimba kijana wa watu, mi nilifurahi kumuona akiongea kiingereza kizuri kwenye interview ya sporah, atleast kaonyesha bidii maana miaka ya nyuma alikuwa hoi,ukizingatia lugha hiyo ndo mtaji kwenye dunia hii ya technology, inshort ndomo anafanya vizuri hakuna wa kubisha ila jeuri na majivuno vitampeleka pabaya, akumbuke alipandishwa na watu na atashushwa na watu

Mungu ana baraka zake,pia jamii inayotuzunguka ina baraka zake, sidhan ata kama uwe na pesa kiasi gan ukadharau watu wanaokuzunguka ata Mungu pia atakudharau na mwisho wake ni mbaya, huwezi kusema unampenda Mungu usiyemuona halafu usimpende ndugu au jiran yako unayemuona, huo ni unafik
 
Anajitahidi kuimba kijana wa watu, mi nilifurahi kumuona akiongea kiingereza kizuri kwenye interview ya sporah, atleast kaonyesha bidii maana miaka ya nyuma alikuwa hoi,ukizingatia lugha hiyo ndo mtaji kwenye dunia hii ya technology, inshort ndomo anafanya vizuri hakuna wa kubisha ila jeuri na majivuno vitampeleka pabaya, akumbuke alipandishwa na watu na atashushwa na watu

Mungu ana baraka zake,pia jamii inayotuzunguka ina baraka zake, sidhan ata kama uwe na pesa kiasi gan ukadharau watu wanaokuzunguka ata Mungu pia atakudharau na mwisho wake ni mbaya, huwezi kusema unampenda Mungu usiyemuona halafu usimpende ndugu au jiran yako unayemuona, huo ni unafik

Bina hili gazet uliloniandikia ungekua ni ubuyu ningependa zaidi aisee,
Dharau zipi ndomo kafanya acheni kumuonea kupanda kapanda kwa juhudi zake kwani kina Blue hawana mashabiki kwanini hawajapandishwa na mashabiki ndomo habari nyingine yupo spid 1000
 
Hapo kapelekwa na chata ya cocacola
halafu wanasema akalale sijui nonde sijui soko matola sijui mbeya hoteli;
hii kitu haiwezekani, acha dogo ajiachie aliyepata kapata tu.

Ukipata kitumieee ukikikosa kijutieeeee
 
Bina hili gazet uliloniandikia ungekua ni ubuyu ningependa zaidi aisee,
Dharau zipi ndomo kafanya acheni kumuonea kupanda kapanda kwa juhudi zake kwani kina Blue hawana mashabiki kwanini hawajapandishwa na mashabiki ndomo habari nyingine yupo spid 1000

Mwambien boss wenu ahame sinza jaman anatia aibu, ameshindwa hata kukaa masaki kama dada jide? Jide ukisema habar
 
Mi nashangaa kuzomewa diamond imekuwa ishu,wakati mheshimiwa rais kikwete alizomewa na akatupiwa mpaka mawe huko mbeya.kwani diamond ni malaika. Tufanye kufunga huu Uzi. Who's diamond by the way
 
chura dume hata heshima niliyokuwa nampa dada mleta mada imekwisha;
Ameonesha moja kwa moja chuki yake ilivyo, naona hao ni lile kundi la zomea zomea;

Hawajui aliye juu mfuate huko huko, wao wanabaki chini huku wakilenga mawe juu kwa mnati.

Kumbe ni mdada mwe................
 
Back
Top Bottom