Kumbe Diamond ana nyodo kiasi hiki

Kumbe Diamond ana nyodo kiasi hiki

Weer bado tunamalizia swimming pool

Kumbe ndo maana unajifanya unamchukia mama ubaya, kumbe unamtaka bwana ake? Basi imekula kwako, utaishia kumsifia mpaka bundle liishe,utaishia kumuona instagram na leaders club au uwanja wa pasiasi mwanza, hahaahaha ahaha utajibeba
 
Makavu Ya Leo: Masikini Akipata ------ Hulia Mbwata, bwana mdogo Diamond mtoto wa Tandale ambae wakati Wema Sepetu anakuwa miss yeye alikuwa anauza mitumba kule Tandale kapata pesa sasa naona makalio yake yanalia Mbwata.

Kama unampenda sana Diamond usipanic endelea kusoma utanielewa tu Diamond amewakera mashabiki ndio maana yamemkuta yale yaliomkuta pale Leaders.

Kijana Diamond alikuwa moja kati ya watu masikini sana nchini, alikuwa ANALALA kwenye mazingira magumu ila leo amediriki kusema kuwa MBEYA HAKUNA HOTELI YENYE HADHI YAKE, hahahaa inachekesha sana. Anasahau kuwa umaarufu wake umekuja kwasababu mashabiki WALIAMUA kumkubali.

Wema Sepetu wakati ana make headlines akiwa Miss Tanzania hakuwa anatambua kuwa pale mitaa ya Tandale kuna kijana anaitwa Nassibu anauza mitumba, na ninaamini hata kama angeonana na Diaomnd kipindi kile HAKIKA asingemuangalia mara mbili.

Ila dogo leo kapata hela anaanza kuleta dharau kwa mashabiki. Dogo ana kauli chafu sana, anapenda kujikweza.

Ukitaka ufanikiwe na ufaidi kuwa msanii bongo hakikisha UNAWAFURAHISHA mashabiki wako mdogo wangu.

Waache watu wakusifie wewe. Kitu ambacho hujui ni kwamba hapa bongo kulikwa na wasanii wakubwa kama akina Mr. Nice lakini walilewa sifa na sasa wanaishia kucheza pool pale Sinza Ambiance na kutia huruma.

Usipoangalia wewe na kaka yako Nice mtakaa kijiwe kimoja na kusema ZAMANI NILIKUWA MAARUFU.

Diamond umekuwa na tabia ya kusema wewe ni maarufu na kukataa mara kadhaa (HATA UKIOMBWA) kufanya show sehemu mbali mbali, unajiona ni msanii wa kufanya SHOO ZA MILL 30, kuna cases kadhaa za wewe kuwatolea nje mashabiki kufanya shoo eti kwa madai unataka hela nyingi.

Unasahau watanzania hawa hawa ndio waliokupigia kura ukapata hizo tuzo na kuwa nominated hata kwenye hizo BET, lakini naona sasa UMEUCHOKA umaarufu wako na uko tayari kuupoteza kwa upuuzi tu usio wa maana.

Kuna mambo mengi sana unakosea kama binadamu ila kuna mengi unayafanya makusudi kwasababu wewe ni LIMBUKENI, kwa mfano suala la kutoka na mabinti kadhaa wa kadhaa kwako umeona kama ni ufahari hivi, kumbe wenzako wanakuona zuzu tu maana huwezi kuwamaliza mabinti wote duniani.

Na kwasababu hiyo ndio maana wanaume wenye akili WAMEMUHONGA WEMA GARI wakasingizia kuwa ni Kadinda ndie alietoa, ukiacha dharau watu watakuheshimu.

Sijui niendelee au niishie hapa?! Aah nikiishia hapa ntakuwa nimekuogopa. Mdogo wangu wewe kimziki sio kwamba uko juu sana kuliko Alikiba, Linex, Barnaba, Ben Paul au hata Lady Jaydee ni kwamba umepata promo nyingi sana kiasi cha mashabiki KUAMUA kukukubali.

Unashangaa watu pale leaders waliamua kukuzomea ni kwasababu watanzania wamechoka na majivuno yako na dharau.

Sasa T.I anataka kufanya collabo na Ali Kiba ile inaonesha dhahiri kuwa wewe BADO.

Anyways kama umemaindi poa ila hayo ni maoni yangu kama SHABIKI na ungekuwa wewe ni chama cha siasa hakika leo ningerudisha kadi yangu ya Uanachama mpaka pale utakapojirekebisha!

Usije ukakonda bure kwa makavu haya. La mwisho Gwanda zile zitakuletea matatizo, inawezekana ulionywa hukusikia jaribu tena uone cha mtema kuni.

Next time hutaitwa Oysterbay watakuficha wenye nazo!

pole mkuu umejisumbua bure diamond hana access na jamii forum umepoteza time yako kuandika bureeeee
 
Kumbe ndo maana unajifanya unamchukia mama ubaya, kumbe unamtaka bwana ake? Basi imekula kwako, utaishia kumsifia mpaka bundle liishe,utaishia kumuona instagram na leaders club au uwanja wa pasiasi mwanza, hahaahaha ahaha utajibeba

Bina tafadhali nimecheka aiseeeee, ngoja nikaoge na kuoga aiseeeee, yashakua hayooooo duuu nimekuita kule kwa kiba unajifanya hunisikiiiii mfuuuu
 
Bina tafadhali nimecheka aiseeeee, ngoja nikaoge na kuoga aiseeeee, yashakua hayooooo duuu nimekuita kule kwa kiba unajifanya hunisikiiiii mfuuuu

Ndo ivo uache kumshobokea baba ubaya ana wake, tena kamnunulia murrano, sasa wewe unavyojishaua kumsifia apa utafikir kakuwekea vocha kwenye simu mfyuu, ebu nipishe apa, kwanza umeona mama ubaya yupo china anafanya shopping ya biashara ya vipodozi au ndo hutak kumsikia kabisa??
 
Mtu yeyote anayeijua kz yake hawezi kukubali kuburuzwa, kwahy hata yeye hawezi kukubali kwa mfano, TI alipwe usd 50m halafu yeye alipwe 1m, huu ni upuuzi, ila kama mmeamua kumjengea fitina ili aonekane wa ovyo kwa kudai malipo yenye kueleweka ni sawa kwa upande wa wapuuzi, lakini sisi wafuatiliaji wa mambo tunapenda kuona wasanii wa kitanzania nao wanafaidika kupitia kazi zao za kisanii, na katika suala la hawa wasanii wawili Diamond na Ali inabidi tuwashindanishe au tuwape sifa kupitia kazi zao ndio tutajua ni nani mkali kati yao na siyo kupitia ushawishi wa nje ya kazi zao.
Waandaaji walitaka akubali dau la wasanii waliojisahau ili wao wapige hela, maana inajulikana kuwa waandaaji wanataka kufaidika zaidi wao na si kuwainua wasanii, ndio maana wasanii wakitoa single 3 tu baaaas ndio imetoka, matokeo wanaendelea kusubiri ugali wa folen kwa wazazi na kupishana nao kwenda chooni, lakin waandaaji wanakula maisha safi kwa upuuzi wa baadhi ya wasanii kujikomba ili wauze sura na si kupata lipato. Inabidi wabadilike waufanye muziki ni kazi yao na si kufanya bora liende, mwenzao mjanja ametumia fursa zilizopo lakini leo hii mnataka kumshusha kwa njia haram, lakin endeleen labda mtafanikiwa waungwana.
Tuendelee kuchangia kwa hoja na si matusi!
 
haaa haaa haaa you make ma day mana ndio naingia jf sasa,na swimming pool yetu imenicost kama milion 200 pekee mana chini chini kuna system ya music.

Hhhhhaaaaaaaaaa
 
Ndo ivo uache kumshobokea baba ubaya ana wake, tena kamnunulia murrano, sasa wewe unavyojishaua kumsifia apa utafikir kakuwekea vocha kwenye simu mfyuu, ebu nipishe apa, kwanza umeona mama ubaya yupo china anafanya shopping ya biashara ya vipodozi au ndo hutak kumsikia kabisa??

Kwa taarifa yako msukuma wangu ana pesa mpaka naumwaaaaaw,hizo gari sie tunazo zaidiii,napenda mziki mengine yenu timu kiba,,uje pm nikuoneshee mme wangu alivyo handsome na pesa anayo utanitakaaaaaa,ndio masaa 24 naperuz jamii sina muda wa kuosha vyombo au kupikaaaaq
 
kwenye hii issue ya diamond kila member wa jf atafungua thread. Nahisi pple walikua wanatamani kuanzisha thread zao ila walikua hawana topic hahaha wengne tuwe tunachangia tu since yaliyoandikwa yote
yameshadiscusiwa humu.

Shikamoo! Hongera kwa kuligundua hilo, waanzishe na gazeti kabisa! !
 
Mleta mada unajidai kujua sana kanuni za maisha?? Enhe we mfuata kanuni hizo zimekusaidia vipi kufanikiwa? Bongo hii uishi kumfurahisha kila mtu is it possible!?
Eti kaonesha dharau lol! Under my foot!! We mpaka leo umewadharau Wangapi? kama hujawahi kudharau mtu, je hiyo imekuongezea nini kwenye maisha yako?

Eti anabadilisha mademu! Ebu tuambie the list yako imefikia ngapi hadi leo!

Btw, Who are you to judge others na kuwafundisha maisha?
 
acheni wivu na roho mbaya,mi nilikiwa siamini story za watu kukataa kujenga nyumba za ukweli makwao huko vijijini kwa sababu wanahofia kurogwa,sasa ndio naamini,hapa mjini tu watu roho zinataka kuwatoka,mngekuwa na uwezo nyie mngekuwa mshamroga,
diamond piga kazi,invest pesa yako sehemu za maana hata ukipotea kwenye game usije kufa masikini,kuna watu wanasibiri udondoke waanze ku
 
Kwa taarifa yako msukuma wangu ana pesa mpaka naumwaaaaaw,hizo gari sie tunazo zaidiii,napenda mziki mengine yenu timu kiba,,uje pm nikuoneshee mme wangu alivyo handsome na pesa anayo utanitakaaaaaa,ndio masaa 24 naperuz jamii sina muda wa kuosha vyombo au kupikaaaaq

Hahahaaaaa chezea watu na waume zao wewe???
Taratibu mama lupita nyongo asimvizie....
 
Kiba na Ti wataimba nn jaman😀😀😀😀 acheni promo za uongo

Hahahaaa.
Timbwili liko hivi now, imagine Q chief naye atake kuchua kiti,.. si itakua blood shed???
 
Back
Top Bottom