Kumbe Diamond ana nyodo kiasi hiki


Umemaliza! Yaani Kosa ni kuwa masikini halafu kwa bidii yake mwenyewe kutajirika ni kosa kubwa sana. Kwa Tanzania, Ukizaliwa Tandale uzeekee Tandale wewe ndio shujaa!Kijana kama Diamond ni muhanga wa hao/ baadhi ya mabinti I am telling you! inawezekana kwa hali aliyofikia anajitahidi sana hata kuepuka hivyo vishawishi nina uhakika ni vingi! Kwa munaomsema mwekeni kwenye maombi Mungu amsaidie kuepuka vishawishi. Mi kuna mtu wangu wa karibu ( sitaki kusema uhusiano wake kwangu) namuhubiria kila siku na kumwambia: anatakiwa awe na misimamo kwa sababu quality alizonazo ndio zinapendwa na oposite sex wengi, sitetei ufuska lakini kuna watu wanaqualities ni upako tu wa Mungu unaweza kumsaidia. Kun thread hapa ililetwa ya Kijana anamwambia Obama asimsemeshe girlfriend wake! Jamani kuna watu wana qualities mpaka unawaonea huruma ya jinsi wanavojitahidi kukabiliana na oposite sex!
 
Aiseee wanambeya mkiisema hiyo ya mbeya nakumbuka kua kuna lifti moja tu naumia mbavu, ila Diamond anaongelewa yaan mnampa umaarufu mara zoteeee

Nyie hamjawah kusema kua kitu flan hakina hadhi au mmemnyooshea kidole Ndomo tu heloooo mtaumwaa sana

Wewe ndio walewale...hiyo lift I unaona issue sana eeh??wewe hapo nyumbani kwako unayo hadi uiseme mbeya nzima hamna???
 
kwenye hii issue ya diamond kila member wa jf atafungua thread. Nahisi pple walikua wanatamani kuanzisha thread zao ila walikua hawana topic hahaha wengne tuwe tunachangia tu since yaliyoandikwa yote
yameshadiscusiwa humu.
 

Umeshupaa na kutoa povu jingi mdomoni lakini ulichokiandikia ni upuuuzi na upuumbavu mtupu kwani hakuna kitu hapo. Wahenga walisema "mtu mpu.mbavu akikaa kimya huwezi kuujua upumba.vu wake mpaka akiongea" pekee nilichokisoma hapo ni kuwa maelezo yako yamejaa chuki, wivu wa kike , tamaa na roho mbaya.

Swala la Diamond kutokea katika maisha ya kimasikini au dhiki kama unavyosema wewe ingawa huna data zozote za kuthibitisha hilo si jambo la ajabu sana duniani. Tumeona historia za wasanii na wanamichezo na hata wafanyabiashara wakubwa mbalimbali zikielezea jinsi maisha yao yalivyokuwa kabla ya kupata mafanikio kimaisha na ukiangalia wanavyoishi sasa ni tofauti. Haimaanishi kama umetoka katika umasikini basi uendelee kuishi kimasikini labda kwa mtu mwenye umasikini wa kimawazo kama ulivyo wewe. Kwa level ya kimafanikio aliyofikia Diamond si ubishi kwamba yupo katika level za kimataifa na lazima alinde hadhi yake aliyokuwa nayo ili aendelee kuongeza heshima yake na kubwa zaidi kuongeza thamani ya kazi zake na kujipatia fedha nyingi zaidi.

Kubali au kataa Diamond siyo wa kumualika katika vitamasha vya vichochoroni vya kiingilio chupa ya pombe na yeye aende huko ni kujishusha hadhi na kuharibu soko la kazi zake. Alafu hicho kinachotokea sio yeye bali ni nguvu ya soko kwani principle za demand and supply zinasema wazi " the higher the demand the higher the price" sasa demand ya Diamond ipo juu sana hivyo lazima na bei yake nayo iwe juu sana vile vile.

Ali Kiba anajitahidi kuimba lakini ni upumbavu kudhani kwamba unaweza kuiongeza thamani ya Ali Kiba kwa kulazimisha kuishusha thamani ya Diamond.

Sisi washabiki wa Diamond wala hatukasiriki jinsi kijana anavyoringia talent yake kwani ile resource ya thamani kubwa aliyokuwa nayo na lazima aringie ni sawa na Daktari Bingwa anapotaka mshahara mkubwa kwa kuringia elimu yake au Prof. Anapotaka chuo kimlipe fedha nyingi na yupo tayari kufundisha vyuo vyenye hadhi na majina makubwa anaringia taaluma yake. Kwanini unataka Diamond ajitoe bure tu.

Kuhusu mapenzi yake na Wema hayo ni maswala binafsi sana na yanahusu mapenzi siyo kazi. Sasa wewe ulitaka aje kukuoa wewe?

Mwisho nakushauri kama unataka utajiri fanya kazi kwa bidii kwani chuki au tamaa au wivu wa kike hautokusaidia kitu.
 
Wewe ndio walewale...hiyo lift I unaona issue sana eeh??wewe hapo nyumbani kwako unayo hadi uiseme mbeya nzima hamna???

Samahani nifah unaishi Mbeya, !!!pole sanaa
 
Last edited by a moderator:
chura dume hata heshima niliyokuwa nampa dada mleta mada imekwisha;
Ameonesha moja kwa moja chuki yake ilivyo, naona hao ni lile kundi la zomea zomea;

Hawajui aliye juu mfuate huko huko, wao wanabaki chini huku wakilenga mawe juu kwa mnati.

Ni kweli kabisa@ Mamndenyi. Yaani wao wanataka kumpandisha msanii kwa kutumia kumdhalilisha yule anayefanya juhudi zake binafsi
 
Last edited by a moderator:
Aiseee wanambeya mkiisema hiyo ya mbeya nakumbuka kua kuna lifti moja tu naumia mbavu, ila Diamond anaongelewa yaan mnampa umaarufu mara zoteeee

Nyie hamjawah kusema kua kitu flan hakina hadhi au mmemnyooshea kidole Ndomo tu heloooo mtaumwaa sana

Anajitahidi kuimba kijana wa watu, mi nilifurahi kumuona akiongea kiingereza kizuri kwenye interview ya sporah, atleast kaonyesha bidii maana miaka ya nyuma alikuwa hoi,ukizingatia lugha hiyo ndo mtaji kwenye dunia hii ya technology, inshort ndomo anafanya vizuri hakuna wa kubisha ila jeuri na majivuno vitampeleka pabaya, akumbuke alipandishwa na watu na atashushwa na watu

Mungu ana baraka zake,pia jamii inayotuzunguka ina baraka zake, sidhan ata kama uwe na pesa kiasi gan ukadharau watu wanaokuzunguka ata Mungu pia atakudharau na mwisho wake ni mbaya, huwezi kusema unampenda Mungu usiyemuona halafu usimpende ndugu au jiran yako unayemuona, huo ni unafik
 

Bina hili gazet uliloniandikia ungekua ni ubuyu ningependa zaidi aisee,
Dharau zipi ndomo kafanya acheni kumuonea kupanda kapanda kwa juhudi zake kwani kina Blue hawana mashabiki kwanini hawajapandishwa na mashabiki ndomo habari nyingine yupo spid 1000
 
Hapo kapelekwa na chata ya cocacola
halafu wanasema akalale sijui nonde sijui soko matola sijui mbeya hoteli;
hii kitu haiwezekani, acha dogo ajiachie aliyepata kapata tu.

Ukipata kitumieee ukikikosa kijutieeeee
 

Mwambien boss wenu ahame sinza jaman anatia aibu, ameshindwa hata kukaa masaki kama dada jide? Jide ukisema habar
 
Ngoja niondoke huku siyo size yangu nimevamia.
 
Mi nashangaa kuzomewa diamond imekuwa ishu,wakati mheshimiwa rais kikwete alizomewa na akatupiwa mpaka mawe huko mbeya.kwani diamond ni malaika. Tufanye kufunga huu Uzi. Who's diamond by the way
 
chura dume hata heshima niliyokuwa nampa dada mleta mada imekwisha;
Ameonesha moja kwa moja chuki yake ilivyo, naona hao ni lile kundi la zomea zomea;

Hawajui aliye juu mfuate huko huko, wao wanabaki chini huku wakilenga mawe juu kwa mnati.

Kumbe ni mdada mwe................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…