Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…

Good,itakuwa ajabu Kama Mh. Rais asikuteue nafasi yoyote hata ya u-DED, mkuu upo vizuri sana, japo sometimes unazingua,aswa kipindi kile Cha Ngosha
Akili zako na huyo Paskali wote sawa and please (do no add the biblical connotations on this arguments) the guy you adore is almost 70 yrs a toothless dog in politics.

CCM oyee
 
Hata kwa Magu ulisifia hivi hivi. Sema walitaka kuku-ulimboka ulipokuwa unakosoa na kushauri. Bora uhai kwanza.
 
Brilliant!
 
Wala usizunguke sana Paskali, tatizo zima liko kwenye hii katiba inayompa rais mamlaka ya kimungu. Huyu DPP wa sasa sidhani kama anatenda haki kwa maana ya haki, bali anafuata maagizo ya rais aliyeko madarakani. Ikitokea rais huyu akaondoka madarakani kwa sababu yoyote leo hii, na akaingia rais muovu kama aliyepita, DPP huyu huyu ataagizwa kufanyia watu maovu tena.

Kama kweli unaongelea haki kwa maana ya haki, kuandika mada ndefu za kumsifu DPP ni kupoteza muda, maana DPP anapewa maagizo na rais. Ni vyema ukajiunga na watanzania wengine kudai katiba mpya, itakayopunguza madaraka ya rais, na kutoa nguvu kwa taasisi. Vinginevyo akifanikiwa kuingia rais mwingine muovu kama Mwigulu Nchemba, utaishia kuandika mada za kupingana na haya iliyoandikwa hapa, na tutaendelea kukuona ni bendera fuata upepo tu.
 
Wewe ni msomi mkubwa na member maarufu sana humu. Ila wakati wa mauaji na mateso ya mwendazake wewe na Mwanakijiji mlikaa kimya na mkasapoti mauaji na mateso
Mpe heshima yake Mayala, we umewahi kuitwa Bungeni kwa ajili ya Post zako?
 
Hizi makala zako zingeegemea KATIBA MPYA.Ila siwezi kukushangaa akili zimeanza kurudi mwezi murch.

Emu tumieni elimu yenu kwa ufasaha ili kusaidia Taifa. Siasa wekeni pembeni kwenye mambo ya msingi.

Ila ukada huwa unawaondoa akili.
Mi niishie hapa.nilitaka nijue tu kipindi cha miaka mitano iliyopita hakuna matukio yaliyotokea na haukuandika chochote .
Ney was mitego ndie aliweza kueleza,kuonya na kusema waziwazi.kwa kutumia nafasi yake.
 
Kwa muda wa mwezi mmoja sasa, wiki nne mfululizo, nimekuwa nikiandika makala za "Kilio cha Haki" nikijiekeza ofisi ya DPP, hatimaye sasa kuna kitu kinatendwa na kinaonekana
Mbona hukuwahi kuandika kabla? Kaka, hebu acha unafiki ndio maana unakosa teuzi.

Tunakujjua upande uliopo na wakiitwa Wazalendo wa nchi hii, kamwe jina lako haliwezi kuwemo. Wewe ni opportunistic
 
Pasco nimesikitika kuwa mama hajakupatia hata uDC na kuna wengine ambao wanaonekana hawastahili lakini wamepata teuzi. Usife moyo. Endelea kupambania kombe.
Nafasi ya Juliana holaa, nafas ya Abbas holaa, nafasi ya Garson holaa. Iliyobakia sasa hivi ni nafas ya Ryoba tu na hii ikishindikana basi itakuwa tu KARMA lazima itakuwa kamfanyia mtu kitu kwa iyo inamrudia haiwezekani vijana uchwara wanalamba teuzi Pasco anaachwa. Haiwezekani!
 
Hayo ni maelekezo na maagizo over.
 
Pisi kali next time utapewa u das wa Wilaya ya Jamiiforum
 
Mkuu Pascal Mahakimu/Majaji, bado ni tatizo kubwa sana katika Mahakama zetu,wengi wao wamekuwa wanatowa maamuzi kwa upendeleo! Nasii kwa kuangalia haki! Hawatowi haki,Bali wao ndiyo wanauza haki kwa mwenye nacho!!
Ukweli hii idara imeoza kabisa
 
PASI, PASIKALI, DPP kutenda haki ni subjective to.( ), Sio passive. Inategemea na upepo na maelekezo ya mtawala, sana sana mtakosana tu. Hakuna independence na haiwezi kuwa kutokana na upatikanaji wake.Fullstop

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Kujali maisha ni wajibu pia nje na fani yake ana haki ya kuwa partisan inapobidi. Nawasilisha sijui Pascall anasemaje?
 
Apo hakuna haki hata moja iliyotendeka,Bali no maagizo tu kutoka mhimili uliojichimbia chini zaidi usitake kutuaminisha sisi wenye macho matatu.
Hivi wewe unaweza kwenda kusimama mahakamani kutoa ushahidi wa ugaidi,mfano mzuri waliokua wanahusika na mauaji ya kibiti wewe unaweza kuisaidia serikali kuwatambua?
Kwa ujumla hakuna haki DPP ametenda ukirejelea hotuba ya mh.rais siku anapokea report ya CAG na report ya takukuru unapata picha kamili kwamba ni maelekezo toka mhimili uliojichimbia chini zaidi na ndio maana alikimbilia kumteua yule ili iwe vyepesi kumpa maagizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…