Kumbe Dr Asha Rose Migiro ni chaguo la Kikwete!

Kumbe Dr Asha Rose Migiro ni chaguo la Kikwete!

Hayo ni maneno ya mitaani yenye chuki binafsi, ya uzandiki na yasiyo na tija yoyote ile.
Watanzania hatujafunga macho wala masikio mpaka tusifaham kazi kubwa na ya pekee inayofanywa na Dr.Migiro pale UN.
Wewe ni mtu wa namna gani usiyelionea haya jasho la mwanadamu mwenzako tena hasa mtanzania mwenzako?
Nyie ndio wale watu ambao ni bora apate mzungu lkn ni sumu kwenu akipata mtanzania mwenzako. Na ikitokea akipata au akisifiwa basi kazi yenu ni kutapakaza majungu na chuki.
Kwa taarifa yako utamchukia mwenyewe na hiyo chuki yako itakurudia mwenyewe.
Watanzania wote tunamfahamu na tunathamini kazi nzuri ya Mama yetu Dr. Migiro.
Hongera MAMA na tunakuombea dua kwa Mungu uepushwe na watu wenye chuki zao kama huyu.
Heko Dr.Migiro.

Wewe utapata ukuu wa wilaya.
 
Uzi huu ni wa 2012. Upepo umebadilika msipoteze muda kujadili
 
Lazima nikiri wazi hizi ni "habari za mitaani".Leo nilikuwa katikati ya mji napata chakula cha mchana katika mgahawa maarufu Alshababu au kwa waSomali ndani ya vyumba vya uwanja wa michezo Sheikh Amri Abeid.Nimekaa katika meza yenye watu wanne siwajui hata mmoja isipokuwa navutiwa na mazungumzo yao.

Mazungumzo yao yamejikita katika uchaguzi wa mwaka 2015.Wote wanakubaliana uchaguzi wa mgombea wa CCM tayari umeshaanza tangu mwaka 2011 najikuta nikijikaribisha mwenyewe bila kukaribishwa,nauliza ni kitu gani kimewaaminisha uchaguzi ndani ya CCM umeshaanza wote wanacheka mmoja anajibu unasikia Bwana hizi kelele za kuvuana gamba unafikiri ni nini kama siyo mkakati wa kumtafuta mgombea au wewe huko dunia ipi ?.Najianda kutoa majibu naambiwa na Kijana mwingine tulia Mzee unajua Kikwete mjanja sana anajua kundi la mapacha watatu lina nguvu kubwa sana na linaweza kuzuia chaguo lake ahaa naingilia kati kwani chaguo la Kikwete ni nani ?.Mzee mpaka leo hujui chaguo la Kikwete we mtanzania kweli kwa taarifa yako Dr Asha Rose Migiro Rais wako 2015.

Mkakati wa Mwenyekiti wa CCM ni kupendekeza mgombea mwanamke "Safari hii ni mwanamke".Upo Mzee wataangaliwa wanawake wenye uzoefu mkubwa.

[1] Anna Makinda Spika wa bunge la JMT,huyu atagaragazwa kwa skando la posho.Suala la posho kwa taarifa yako Rais analijua na alishalikubali kaamua kuliacha lilivyo ili kumuondolea sifa Makinda.Nauliza wapi mmepata hizi habari [Naomba source].Mimi mbunge wangu kanimbia kila kitu,vikao vya wabunge wa CCM suala la posho lilishapitishwa siku nyingi Mama wa watu kaachiwa kikapu.Hivi vikao vya CDM Magogoni nia yake kubwa ni kumdhalilisha spika asivyojua kazi yake vizuri.

[2] Professor Tibaijuka Waziri wa Ardhi,huyu atagaragazwa na waZanzibar au hujasikia alivyoshutumiwa na waZanzibar Tanzania kujiongezea mipaka ya eneo la Bahari kuu.Mzee huu ni mkakati wa Kikwete kamtuma Jussu kupayuka maksudi auanataka kujifanya hujui Jussu alipewa ubunge na Kikwete hawa ni marafiki wakubwa wana mikakati yao siku mkishtuka Dr wake kashakalia kiti cha magogoni.

[3] Dr Asha Rose Migiro Naibu katibu mkuu UN,huyu atapeta hana kashfa wimbo sasa ni zamu ya kina mama utaimbwa waTanzania kama kawaida yenu mtaupokea na kuongezea madoido.Mzee kwa taarifa yako huyu Mama kaambiwa ni lazima arejee nyumbani haraka wajumbe na warasimu wa CCM wamzoee mapema siku ngoma ikipigwa msijesema alikuwa wapi siku zote.Namalizia juice baridi tunaagana na hawa marafiki zangu wapya nafurahi uTanzania wangu namkumbuka Nyerere lugha ya kiswahili imetuunganisha waTanzania.Marafiki zangu wapya hatukuulizana dini wala makabila yetu.

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika na watu wake.

mwanaume akiwa rais mkewe anaitwa " first lady " vipi kama rais akiwa mwanamke je mumewe ataitwaje? nataka nianze kujiandaa kulitumia hilo jina / neno la kidhungu!
 
hana nguvu ya kumsimamia mtu huyo

Rais lowasa full stop. ..aspopitishwa na ccm nguvu ya umma tutajua cha kufanya enzi za zidumu fikra za mwenyekiti zilishaptwa na wakati na wakijarbu kuztumia ccm tutajua cha kufanya wananchi ambacho ni kumpa kura silaha na wabunge wote wa ukawa ata waksmamaisha jiwe...na wakiiba tutajua option b
 
siku hizi hapa jamii forums wana mtindo mbaya sana wananyofoa post..kuna uzi wa mmoja nilimuwasha Makongoro wakaunyofoa uzi wangu..hili la huyu mama Migiro kua chaguo la mukulu mie nililijua kitambo huku huku na wala sipo dar kua mzee anatetea himaya yake na hili ndo chaguo lake...lakini piga ua garagaza sasa hivi nguvu ya wananchi ndo itaamua na UKAWA ndo mkombozi wao.tumewachoka CCM.
 
siku hizi hapa jamii forums wana mtindo mbaya sana wananyofoa post..kuna uzi wa mmoja nilimuwasha Makongoro wakaunyofoa uzi wangu..hili la huyu mama Migiro kua chaguo la mukulu mie nililijua kitambo huku huku na wala sipo dar kua mzee anatetea himaya yake na hili ndo chaguo lake...lakini piga ua garagaza sasa hivi nguvu ya wananchi ndo itaamua na UKAWA ndo mkombozi wao.tumewachoka CCM.
Tumewachoka kweli Na hao akina migilo waliokuwa wanashabikia katiba ya ajabu.ccm tulia mkabidhi madaraka kwa aman
 
kwa huyu mama sioni hata bayalake ilA wanamsifia kwa uchapakazi sijajua sana kama akixhaguliwa huyu mayb japo snA uhakika ila anaonekana kufaa bank moon anasema ni mtendaji zaid si msemaji sana
ngoja tuone.
 
Nchi hii mwanamke kushinda hasa kwa mwaka huu ambapo nchi iko Dilema haiwezekani,ukawa watashinda kiurahisi kama migiro atakua mgombea
 
Nchi hii mwanamke kushinda hasa kwa mwaka huu ambapo nchi iko Dilema haiwezekani,ukawa watashinda kiurahisi kama migiro atakua mgombea

Toa sababu ni kwanini inakuwa vigumu mwanamke kushinda nafasi ya uRais.
 
Kikwete baba naomba mawazo yako uende nayo wal hatutaki kuyasikia. Nchi utuharibie upo na hata ukiwa haupo ? Haiwezekani !!!
 
Watanzania wakati umefika tuikomboe nchi yetu toka kwa hawa watawala CCM huu ndio mwaka wenu wa kuhamishiwa jumba la makumbusho

Chonde Chonde watanzania iwe mwisho wetu wa kuteswa na hawa mafisadi waliojichotea mabilioni na kuacha watanzania kwenye maisha duni elimu duni matibabu duni na hali mbaya

Huko vijijini ndio mnaoteseka zaidi kwa kukosa huduma za kijamii kutokana na kuongozwa na hawa mafisadi CCM sasa basi na acheni kudanganywa kwa kanga na kofia acheni mambo ya kuuza nchi kwa kanga na kofia kama mlivyouza madini kwa kuonyeshwa kioo cha kujiangalia.
 
Jamani,nwacheni jk,hana mgombea,dr migiro hawezi kuwa mwenyekiti wa ccm taifa,itakuwa shiida,hajawahi hata kusimama akagombea ubunge,anapewa viti maalum tu,akatafute jimbo agombee,tuone,tunayajua madudu aliyofanya UN atuache mwanamama huyu.
 
Back
Top Bottom