Kumbe Dr Asha Rose Migiro ni chaguo la Kikwete!

Kumbe Dr Asha Rose Migiro ni chaguo la Kikwete!

Lazima nikiri wazi hizi ni "habari za mitaani".Leo nilikuwa katikati ya mji napata chakula cha mchana katika mgahawa maarufu Alshababu au kwa waSomali ndani ya vyumba vya uwanja wa michezo Sheikh Amri Abeid.Nimekaa katika meza yenye watu wanne siwajui hata mmoja isipokuwa navutiwa na mazungumzo yao.

Mazungumzo yao yamejikita katika uchaguzi wa mwaka 2015.Wote wanakubaliana uchaguzi wa mgombea wa CCM tayari umeshaanza tangu mwaka 2011 najikuta nikijikaribisha mwenyewe bila kukaribishwa,nauliza ni kitu gani kimewaaminisha uchaguzi ndani ya CCM umeshaanza wote wanacheka mmoja anajibu unasikia Bwana hizi kelele za kuvuana gamba unafikiri ni nini kama siyo mkakati wa kumtafuta mgombea au wewe huko dunia ipi ?.Najianda kutoa majibu naambiwa na Kijana mwingine tulia Mzee unajua Kikwete mjanja sana anajua kundi la mapacha watatu lina nguvu kubwa sana na linaweza kuzuia chaguo lake ahaa naingilia kati kwani chaguo la Kikwete ni nani ?.Mzee mpaka leo hujui chaguo la Kikwete we mtanzania kweli kwa taarifa yako Dr Asha Rose Migiro Rais wako 2015.

Mkakati wa Mwenyekiti wa CCM ni kupendekeza mgombea mwanamke "Safari hii ni mwanamke".Upo Mzee wataangaliwa wanawake wenye uzoefu mkubwa.

[1] Anna Makinda Spika wa bunge la JMT,huyu atagaragazwa kwa skando la posho.Suala la posho kwa taarifa yako Rais analijua na alishalikubali kaamua kuliacha lilivyo ili kumuondolea sifa Makinda.Nauliza wapi mmepata hizi habari [Naomba source].Mimi mbunge wangu kanimbia kila kitu,vikao vya wabunge wa CCM suala la posho lilishapitishwa siku nyingi Mama wa watu kaachiwa kikapu.Hivi vikao vya CDM Magogoni nia yake kubwa ni kumdhalilisha spika asivyojua kazi yake vizuri.

[2] Professor Tibaijuka Waziri wa Ardhi,huyu atagaragazwa na waZanzibar au hujasikia alivyoshutumiwa na waZanzibar Tanzania kujiongezea mipaka ya eneo la Bahari kuu.Mzee huu ni mkakati wa Kikwete kamtuma Jussu kupayuka maksudi auanataka kujifanya hujui Jussu alipewa ubunge na Kikwete hawa ni marafiki wakubwa wana mikakati yao siku mkishtuka Dr wake kashakalia kiti cha magogoni.

[3] Dr Asha Rose Migiro Naibu katibu mkuu UN,huyu atapeta hana kashfa wimbo sasa ni zamu ya kina mama utaimbwa waTanzania kama kawaida yenu mtaupokea na kuongezea madoido.Mzee kwa taarifa yako huyu Mama kaambiwa ni lazima arejee nyumbani haraka wajumbe na warasimu wa CCM wamzoee mapema siku ngoma ikipigwa msijesema alikuwa wapi siku zote.Namalizia juice baridi tunaagana na hawa marafiki zangu wapya nafurahi uTanzania wangu namkumbuka Nyerere lugha ya kiswahili imetuunganisha waTanzania.Marafiki zangu wapya hatukuulizana dini wala makabila yetu.

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika na watu wake.

hana kasi/
easy to control
we don't want!!
 
mwanaume akiwa rais mkewe anaitwa " first lady " vipi kama rais akiwa mwanamke je mumewe ataitwaje? nataka nianze kujiandaa kulitumia hilo jina / neno la kidhungu!

Anaitwa First Father mkuu
 
Hatuwezi kutawaliwa na binadamu anayelala chali na kisha kukojolewa.Tanzania si taifa la kutawaliwa na mwanamke hapa siyo Philipines,Liberia,Ireland au Finland,ccm inatafuta tu sababu ya kuanguka.
 
Hatuwezi kutawaliwa na binadamu anayelala chali na kisha kukojolewa.Tanzania si taifa la kutawaliwa na mwanamke hapa siyo Philipines,Liberia,Ireland au Finland,ccm inatafuta tu sababu ya kuanguka.

Eti anayelala chali na nini mkuu???
 
Rais lowasa full stop. ..aspopitishwa na ccm nguvu ya umma tutajua cha kufanya enzi za zidumu fikra za mwenyekiti zilishaptwa na wakati na wakijarbu kuztumia ccm tutajua cha kufanya wananchi ambacho ni kumpa kura silaha na wabunge wote wa ukawa ata waksmamaisha jiwe...na wakiiba tutajua option b

Kamanda mdogomdogo yaani nimecheka sana, hasa neno "option b" dah punguza hasira
 
Hatuwezi kutawaliwa na binadamu anayelala chali na kisha kukojolewa.Tanzania si taifa la kutawaliwa na mwanamke hapa siyo Philipines,Liberia,Ireland au Finland,ccm inatafuta tu sababu ya kuanguka.

wacha nicheke mie!
 
kama ni kweli ni chaguo lake basi ni changuo la watanzania kwa kweli ana mvuto na anaweza kutufikisha sehemu salama:drama:
 
wanawake wanaweza wakiwezeshwa , hivyo sina shaka dr migiro akiwezeshwa anaweza kuwa rais mzuri tu .APEWE
 
Lakini tuangalie vilevile na uwezekano wa kuwa na makundi mabaya asije akatupeleka pabaya zaidi
mkuu barubaru.

Ni kweli lakini tanzania kila kitu kinawezekana kikiwezeshwa ndiyo maana anna makinda ni spika wa bunghe letu.
 
Hatuwezi kutawaliwa na binadamu anayelala chali na kisha kukojolewa.Tanzania si taifa la kutawaliwa na mwanamke hapa siyo Philipines,Liberia,Ireland au Finland,ccm inatafuta tu sababu ya kuanguka.

Na akitokea rais mwanamke utafanyaje??
 
Anaitwa First Father mkuu

First father atakuwa kama boya tu, amfuate mkewe kila sehemu...
Mke wake akikutana na viongozi wenzake wajadili mambo muhimu yeye atakuwa anauza sura hotelini??...
First father shughuli zake ni zipi hasa??
 
kama ni kweli ni chaguo lake basi ni changuo la watanzania kwa kweli ana mvuto na anaweza kutufikisha sehemu salama:drama:
​Acha uvivu wewe huyu mama atawafikisha wapi??hii ni zamu ya UKAWA sasa watake wasitake nguvu ya umma itafanya kazi yake this time.
 
Hatuwezi kutawaliwa na binadamu anayelala chali na kisha kukojolewa.Tanzania si taifa la kutawaliwa na mwanamke hapa siyo Philipines,Liberia,Ireland au Finland,ccm inatafuta tu sababu ya kuanguka.
Mmh...... sasa wewe lengo lako ni kuwadhalilisha kina mama.
 
Kabinti ka katiba kaliondoa mawazo yetu, pole huwezi mama go home fasta
 
Sielewi mtu awe mwanachama wa ccm for less than 5 yrs leo anaamkia kutaka urais,jamani tumelogwa na nani?hata mtu msomi,makini kama jaji augustino unaingizwa mkenge eti unafaa kuwa rais,ghosh tunakwenda wapi?kama mnataka kuikabidhi ccm kwa ukawa .
 
Back
Top Bottom