Kumbe Fatma Karume mkali hivi! Amchenjia mtangazaji wa Clouds FM live redioni

Kumbe Fatma Karume mkali hivi! Amchenjia mtangazaji wa Clouds FM live redioni

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Wakili mzoefu, Fatma Karume almaarufu shangazi leo amemtuhumu mtangazaji wa kipindi cha michezo cha Clouds FM, Prisca Kishamba kuwa ni muongo na yeye hamna kitu hapendi kama watu wanaofanya 'Assumption'.

Fatma alitengeneza swali na kumtaka mtangazaji amuulize upya kama alivyosema baada ya mtangazaji kulikosea, jambo ambalo mtangazaji alifanya. Mahojiano yao yalihusu sakata la Fei Toto kushindwa rufaa yake ambapo alikuwa anasimamiwa na Fatma Karume kama mwanasheria wake.

Video niambatanisha

Kajibu kisomi sana. Media zikiwa zinafanya reasoning vizuri, wakichagua watu wazuri kwenye mahojiano yao. Wallahi. Media zitakua taamu sana.

Reasoning!!!! Bonge kitu kwenye maongezi. Huwa nafurahi sana Aljazeera na BBC, ukiona mtu anahojiwa na ni mzito, akiongea mpaka unameza mate daaah. Safi.

Isichukuliwe vibaya hii na huyo Prisca wala wenzake hao naona walikuwa wanamdowngrade Fatuma. Wajifunze kitu hapo. Si kila siku wapo na yule mzee wa tafsiri tu.
 
Mimi Shangazi ananishangaza kwenye kiingereza tu. Ndio unaweza kufaham na kuongea kiingereza kwa ufasaha lakini Aunty licha ya kuongea kingereza kwa ufasaha lakini anakiongea kabisa na lafudhi ya uingereza tena kama ile ya Newcastle. Ni vigumu kwa mtu siyo Muingereza kuongea kiingereza na lafudhi ya uingereza. Hivi kawezaje? Aliishi na waingereza tangu utotoni?

Sky Eclat
 
Mimi Shangazi ananishangaza kwenye kiingereza tu. Ndio unaweza kufahamna na kuongea kiingereza kwa ufasaha lakini Aunty licha ya kuongea kingereza kwa ufasaha lakini anakiongea kabisa na lafudhi ya uingereza tena kama ile ya Newcastle. Ni vigumu kwa mtu siyo Muingereza kuongea kiingereza na lafudhi ya uingereza. Hivi kawezaje? Aliishi na waingereza tangu utotoni?

Sky Eclat
Sio ngumu ni mazoea tu.

Huwezi kuwa umesoma ktk shule za kajamba nani primary&secondary schools then uje usome vyuo vyetu hivi ambavyo hata wakufunzi ni chenga alafu utarajie raia wajue hiyo lugha vizuri.

Kitu kingine ujuzi wa lugha ni kipaji si kila mtu kajaaliwa kuwa na uwezo wa kumaster lugha nje ya asili yake alipokulia na kuizoea.

Cha mwisho mazoezi, ili uwe mzuri wa jambo fulan inakupasa uwe na mazoezi+mazoea ya kulifanya jambo hilo kwa kujifunza daily,

Note[emoji117]. Kujua English sio kigezo cha akili&ufaham acheni Utumwa wa akili.
 
Sio ngumu ni mazoea tu.

Huwezi kuwa umesoma ktk shule za kajamba nani primary&secondary schools then uje usome vyuo vyetu hivi ambavyo hata wakufunzi ni chenga alafu utarajie raia wajue hiyo lugha vzr...
MIMI SIZUNGUMZII KUJUA KIINGEREZA. NAZUNGUMZIA LAFUDHI. LAFUDHI YA FATMA NI YA UINGEREZA. ELEWA COMMENT YANGU.

Mkuu wengi wako Uingereza wanaongea kiingereza kwa ufasaha lakini siyo lafudhi. Ukizingatia Fatma siyo Muingereza kazaliwa na wazazi wazanzibar lakini kiingereza chake ni lafudhi ya Uingereza. Kiingereza cha Salim Kikeke na Zuhra Yunus ni kizuri na kimeenyooka wameishi Uingereza lakini wakiongea siyo lafudhi ya Uingereza.
 
Mimi Shangazi ananishangaza kwenye kiingereza tu. Ndio unaweza kufaham na kuongea kiingereza kwa ufasaha lakini Aunty licha ya kuongea kingereza kwa ufasaha lakini anakiongea kabisa na lafudhi ya uingereza tena kama ile ya Newcastle. Ni vigumu kwa mtu siyo Muingereza kuongea kiingereza na lafudhi ya uingereza. Hivi kawezaje? Aliishi na waingereza tangu utotoni?

Sky Eclat
Secondary mpaka chuo amesoma Uingereza.
 
Secondary mpaka chuo amesoma uingereza.
Wangapi wamezaliwa Uingereza na wazazi wa mataifa mengine lakini kiingereza chao licha ya kuongea kifasaha hawana lafudhi ya Uingereza? Ni wachache sana. Wataongea kiingereza kizuri tu lakini ile lafudhi. Huyu Riki Sunak ni tofauti na wahindi wengine waliozaliwa Uingereza, kiingereza chake ni lafudhi ya Uingereza lakini mke wake amezaliwa na kukulia Uingereza tofauti. Fatuma aliwezaje tena akizungumza ni kile ka ndani ndani lafudhi ya wa Newcastle
 
MIMI SIZUNGUMZII KUJUA KIINGEREZA. NAZUNGUMZIA LAFUDHI. LAFUDHI YA FATMA NI YA UINGEREZA. ELEWA COMMENT YANGU.

Mkuu wengi wako uingereza wanaongea kiingereza kwa ufasaha lakini siyo lafudhi. Ukizingatia Fatma siyo Muingereza kazaliwa na wazaz wazanzibar lakini kiingereza chake ni lafudhi ya uingereza. Kiingereza cha Salim Kikeke na Zuhra Yunus ni kizuri na kimeenyooka wameishi uingereza lakini wakiongea siyo lafudhi ya uingereza.
Kasomea huko huko Uingereza...mpaka ngazi ya kuwa barrister.
 
Hawa Watangazaji wa hiki pindi cha michezo cha Clounds leo wameukwaa mchongoma. Hawana hata uwezo wa kuchambua sheria wao wanakurupuka na maswali ya kijinga, hatimaye wamepelekwa shule. Aunt yupo calm anatoe elimu kwa wajinga.
 
Mimi Shangazi ananishangaza kwenye kiingereza tu. Ndio unaweza kufaham na kuongea kiingereza kwa ufasaha lakini Aunty licha ya kuongea kingereza kwa ufasaha lakini anakiongea kabisa na lafudhi ya uingereza tena kama ile ya Newcastle. Ni vigumu kwa mtu siyo Muingereza kuongea kiingereza na lafudhi ya uingereza. Hivi kawezaje? Aliishi na waingereza tangu utotoni?

Sky Eclat
Alisoma elimu ya shule ya msingi, upili na chuo akiwa nchini Uingereza.
 
Waandishi wengi wahabari nawashangaa sana. Ninawasikiliza katika chambuzi zao mbalimbali sheria wanaja wao, mambo ya ndoa ndio wamooo, ikija dini ukristo na uislam dini zote wamoooo, ukigusia mpira ndio utashangaa. Iguse siasa sasa utainjoi na roho yako.

Walio wengi hata hawajui mambo na hawajui wanachokitaka. Makanjanja
 
Wakili mzoefu, Fatma Karume almaarufu shangazi leo amemtuhumu mtangazaji wa kipindi cha michezo cha Clouds FM, Prisca Kishamba kuwa ni muongo na yeye hamna kitu hapendi kama watu wanaofanya 'Assumption'.

Fatma alitengeneza swali na kumtaka mtangazaji amuulize upya kama alivyosema baada ya mtangazaji kulikosea, jambo ambalo mtangazaji alifanya. Mahojiano yao yalihusu sakata la Fei Toto kushindwa rufaa yake ambapo alikuwa anasimamiwa na Fatma Karume kama mwanasheria wake.

Video niambatanisha

View attachment 2535339
Katazo la kufanya uanasheria lilishaondoshwa?
 
Waandishi wa habari hasa wa Tz wao weamua kukuza habari za migogoro tu, wakisikia habari mbayambaya ndo wanakutafuta huku wakiwa wanamajibu yao wanayotaka ujibu vipindi vyote vimekua vya umbea, magazeti yanasomwa kimbea, habari za michezo umbea
 
Back
Top Bottom