Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Karibu viongozi wote wa Afrika wana tabia moja inayofanana - kujitajirisha binafsi kwa kuingia mikataba ya siri inayoumiza nchi zao, huku wakidanganya umma mikataba hiyo ni kwa faida ya nchi zao. Mtu yeyote mwenye akili atajua kwamba mkataba ambao kweli una nia ya kuinufaisha nchi hauwezi kufanywa uwe wa siri. Utaufanya wazi ili ukusaidie kujinadi kwa watu wako.
Viongozi wa Afrika wengi sana wanapenda kusifiwa. Sasa jiulize, kama kiongozi anafanya mambo kwa manufaa ya nchi yake, pamoja na mikataba, kwa nini afanye iwe siri badala ya kuiweka wazi ili watu wamsifie kuwa kiongozi mzuri, badala ya kutumia pesa nyingi kujifanyia kampeni? Tangu lini mtu anaependa sifa akafanya kitu kizuri kwa ajili ya watu kwa siri?
Na ndivyo ilivyo kwa mikataba mingi inayofanywa hapa Tanzania, hasa nchini ya uongozi wa sasa wa Raisi Samia. Inafanywa kuwa siri kubwa. Na watu hata hawajiulizi; Raisi wetu anapenda sana kusifiwa kuwa anapiga mwingi au apewe maua yake. Sasa kwa nini afanye mambo ambayo ni kwa faida ya Tanzania kwa siri? Kama hii mikataba ni kwa faida ya Tanzania, kwa nini asiiweke peupe ili tumsifie hata zaidi na hata baadhi ya wale wenzetu wajinga wajinga wale waanze kusema tubadilishe Katiba awe raisi kwa vipindi vya miaka kumi kumi? Utafanyaje mambo makubwa mazuri kwa siri ili utumie fedha nyingi kujinadi kwa wapiga kura? Contradiction.
Sasa leo hii, huko Kenya imegundulika kuwa uongozi wa Kenya uliamua kuingia mkataba wa siri wa kumpa mwekezaji toka India achukue airport kwa miaka 30, kwa bei chee kabisa. Mkataba huu ulikuwa wa siri sana kiasi kwamba hata makamu wa Raisi wa Ruto hakushirikishwa, na inaonekana ilikuwa ni dili ya Ruto.
Lakini tofauti na sisi Yombayomba wa Tanzania, wenzetu Wakenya wamekuja juu wanasema hii airport hachukui mtu hapa,piga ua! Natamani tungefanya hivyo kwa ajili ya badnari zetu.
www.jamiiforums.com

Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga kugoma wakipinga Kampuni ya Adani kuendesha Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta
KENYA: Wafanyakazi na Watoa Huduma katika Sekta ya Anga wametangaza kufanya Mgomo kuanzia Agosti 19, 2024 wakipinga kampuni ya Adani Airport Holdings ya India kupewa tenda ya miaka 30 kusimamia na kuendeleza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Kwa mujibu wa taarifa ya Muungano wa...