Hivi umeleta taarifa hii hapa kwa minajili gani na hasa ikiwa ni taarifa ya kupotosha kabisa!
Inaonekana taarifa yenyewe inaungwa mkono na 'moderator' kwa kufuta maoni yanayorekebisha uongo huu. Kuweka uongo kama huu hakuwezi kuifanya Tanzania iwe bora zaidi ya nchi nyingine.
La kushangaza ni kwamba hata namba zilizowekwa haionyeshwi zimetoka wapi!
Moderator uliyefuta mchango wangu hukutenda haki hata kidogo. Hii ni mara ya pili kufanyiwa hivi. Nitakata rufaa ukiendelea kuninyima haki ya kuwasilisha maoni yangu bila ya sababu inayoeleweka. Unapofuta mchango wa mtu aleza sababu aelewe. Huwezi kufuta tu na kukaa kimya maadam tu wewe hukupenda yaliyoandikwa.
Tufungwe midomo kule, na huku pia mnataka kutuziba tusiseme yaliyo ya kweli?