Kumbe Kenya pamoja na kujidai koote na shirika lao la ndege walidhulumu ndege za EAC

Nimensikia Rais wangu akisema baada ya EAC kuvunjika Kenya ilitoa order ya ndege zote zipack pale Kenya. Tuliambulia ndege 1. Ebwana Wakenya pamoja na kujidai kote walidhulumu ndege za tz, ug bila hata shukrani. Hawa jamaa ni hatari
Wezi sana, waliiba ndege kibao
 
Ukianzisha uzi wenye utata lazima uweke data ili upingwe kwa data, lakini ukitumia akili za kinyumbu unapingwa kinyumbu....
Mwisho wa siku huu uzi wako utajaa mipasho tu maana hukuanza na reference yoyote, ni full vijembe..

 

Hiyo source uliyoleta mbona haiendani na ulichoandika humu, endelea kutafuta Google natumai utafanikiwa na kupata jibu kwanini Nyerere pamoja na alivyokua anapenda kuwa na ubabe wa kuhusisha Tanzania kwenye vita Afrika, mbona hili la ndege aliufyata na hakusema hata ng'wee wala kujifanya kama anajikuna, kasomeni historia ipasavyo, mlidanganywa sana na mtaendelea kudanganywa hadi siku mtatia akili.
 

Soma habari yote nyang’au
 
Source please?
Source ni rais wako. 'Common knowlegde' ni kwamba Tz haikuwa na umiliki wa hata asilimia kumi ya E.A.Airways. Zanzibar; 0.7%, Tanganyika; 9%, Uganda; 22.6%, Kenya; 67.7%. Kati ya wafanyikazi 5,000 wa E.A.Airways 3,000 walikuwa wakenya. Makao makuu ya E.A.Airways, uwanja wa ndege wa Eastleigh, Nairobi na baadaye Embakasi na Wilson Airport. Uwe unajiongeza kwa kufanya utafiti kwanza kabla ya kuteletea umbea kutoka kwa rais wako.
 
wengi wanauliza mbona mdomo wa jiwe hauna breki? au anaugua ugonjwa wa mnyika!?
Ni kwamba inawezekana ilikuwa bahati mbaya au kwa makusudi viongozi wengi wa mashirika ya eac walikuwa wakenya. Sasa inaonekana Kenya walijua kuwa jumuia itavunjika. Walichokifanya walihakikisha mali nyingi zinazohamishika zinaenda Kenya. Hata vichwa vya treni waliviutisha kwenda kufanyiwa service kenya. Ujue wakati huo reli ya Tanzania na Kenya zilikuwa zimeungana. Hata meli ya mb Victoria walihakikisha iko Kisumu.
Ndio maana baada ya kuvunjika Mwalimu Nyerere akakasirika akafunga mpaka na kuwaita manyang'au yaani mafisi.
Ni baada ya Dr. Umbrich kufanya mgao ndio baadhi ya vitu vikaachiwa kama mv Victoria na kuwa ya Tanzania.
 
Kenya airways si zinatua kila siku dar, Kamateni basi kama waliwadhulumu. Vinginevyo mnatupigisha hekaya za esopo na kalumekenge amekataa kwenda shule
Labda hupendi kusikia historia.
 
Soma habari yote nyang’au

Nilisoma yote neno kwa neno hakuna sehemu inaeleza KWANINI Kenya ilichukua ndege zote na washirika wote wa EAC kila mmoja akakunja mkia bila hata kung'aka.
Na hata hotuba ya Magu nimeiona, anampongeza rubani kutorosha ndege lakini hakuthubutu kuongea yaliyopelekea au kusababisha huyo rubani kuiba hiyo ndege.
Ni kama ilivyo hata kwenye vita, kuna wapiganaji hupongezwa kwa mauaji waliyoyafanya licha ya nchi yao kuwa mchokozi.
 
Wakati huo nchi zote zikimiki asilimia sawa.
Aaa wapi! East Africa Airways ilipobuniwa, na hadi iliposambaratika umiliki ulikuwa ni ule ule. Kenya ilimiliki kwa kiasi kikubwa zaidi, 67.7% huku jamaa wa blah blah nyingi Tanganyika na Zanzibar wakimiliki 9% na 0.7% mtawalia. Uganda 22.6%.
 
MaBongolala hawawezi kutumia bongo zao kucheki kwenye mtandao, wanasubiri kuambiwa tu. Haya, kwa hisani ya Wikipedia............... Nasisitiza kwa kutumia colours, na bold type. If you can't see, I recommend you to go to school of the blind.

Management assistance from Aer Lingus was contracted in mid-1976 amid deteriorating relations between the three countries that ran the airline.[25] Financial difficulties deepened when both Tanzania and Uganda struggled or failed to pay their outstanding debts for the operations of the airline.[26][27][28] EAA operations came to a total halt in January 1977.[29][30] The airline had incurred in a debt of US$120,000,000 (equivalent to $485,403,624 in 2017) when it went into liquidation in February 1977, with the Kenyan government being one of the major creditors.[26] Both Kenya and Uganda had established their own national airlines before the folding of the corporation, with Uganda Airlines forming in 1976 and Kenya Airways in 1977.[29] Tanzania followed in April 1977 with the formation of Air Tanzania.[31]
 

Source please, imeipata wapi?
 
Aaa wapi! East Africa Airways ilipobuniwa, na hadi iliposambaratika umiliki ulikuwa ni ule ule. Kenya ilimiliki kwa kiasi kikubwa zaidi, 67.7% huku jamaa wa blah blah nyingi Tanganyika na Zanzibar wakimiliki 9% na 0.7% mtawalia. Uganda 22.6%.
Ok. Sikumbuki inawezekana. Lakini bado ilikuwa kampuni ya nchi 3
 
Nimensikia Rais wangu akisema baada ya EAC kuvunjika Kenya ilitoa order ya ndege zote zipack pale Kenya. Tuliambulia ndege 1. Ebwana Wakenya pamoja na kujidai kote walidhulumu ndege za tz, ug bila hata shukrani. Hawa jamaa ni hatari

Tatizo kubwa la Watanzania walio wengi ni uvivu wa kufikiri na kufanya utafiti japo kidogo ili kujiridhisha na facts kabla ya kusema au kuandika jambo. Japo ni kweli ilipovunjika EAC ndege nyingi zilikuwa Kenya LAKINI KWENYE MGAO WA MALI NA MADENI ULIOFANYIKA BAADAE KENYA ILILIPIA.
Pili ndege zilizokuwa enzi hizo ni VC na DC. Je zipo leo?
Mwacheni jiwe azidi kujidhalilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…