Kama kawaida yenu wakenya, hamna mnachojua zaidi ya kupiga domo tupu, kila nchi ilichangia sawa katika kuundwa kwa EAC mwaka 1967, ila Kenya ilichafuliwa kuwa maka makuu ya East Africa Airways, Tanzania kuwa HQ hapo Arusha, na Uganda kuwa makao makuu ya posta na simu.
Baada ya kuvunjika kwa EAC, Tanzania tulibaki na Mali nyingi zaidi zisizohamishika, majengo yote pale Arusha tuliyachukua, hapakua na sababu yoyote ile ya kugombea ndege nyingi zilizokua Kenya ambako ndio kulikua HQ ya East Africa Airways, sio kwasababu Kenya ilikua imechangia zaidi katika ndege, je unataka kutuaminisha kwamba Tanzania ilichangia zaidi katika ujenzi wa HQ pale Arusha ndio sababu ikabaki na majengo yote?.
Kwanini inataka Zanzibar wakati hapakua na Zanzibar mwaka 1967 EAC ilipoundwa, na kamwe Zanzibar haijawahi kuwa na ndege zake?, nchi zilizounda EAC mwaka 1967 ni tatu tu, Kenya Uganda na Tanzania, hii ZANZIBAR umeitoa wapi?.