Kwenye hii issue sina uhakika wowote kwahiyo naiacha inipite kushoto tu, ila ningependa kuongelea issue ya nguvu ya Manara ndani ya Yanga
Ukiangalia Kwa makini na tukiacha huu unafki wa usimba na uyanga utagundua kuwa ni kweli Haji ana nguvu Fulani ndani ya Yanga
Tukianza kwa kutazama sababu ya kuondoka Antonio Nugazi na kuja Haji Manara, Kwa Akili ya kawaida tu sidhani kama kuna mwana Yanga ambae alifurahia kufukuzwa Kwa Nugazi na kuletwa Manara
Tukija kwenye issue ya Manara kufahamika kama Afisa muhamasishaji ila cha ajabu anakuwa na nguvu/mamlaka makubwa kuliko Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli
Hadi hapa tulipofikia ni wazi kuwa Hassan Bumbuli sio Afisa habari tena, kwahiyo hajulikani ana cheo gani tena pale Yanga ila sio ajabu kama atakuwa kashatemwa jumla ili kutengeneza mazingira ya nafasi yake kupewa Manara moja Kwa moja
Ukiangalia issue ya Manara kwenda kwenye tamasha la siku ya wanachi ni wazi kuwa Hilo wazo haliwezi kuwa la Raisi wa club bwana Hersi, bali lazima litakuwa ni wazo la Haji na Raisi akawa hana budi kukataa, Manara ni mtu ambae anapenda sana tabia ya kutunishiana misuri hivo alikuwa anaijaribu TFF kwa pride yake mwenyewe na sio Yanga
Issue ya Yanga kutangaza official kuwa wameingiza mapato mengi kwenye siku ya wanachi kuliko Simba day, hili limekuja baada ya kuona Simba imejaza uwanja sasa ili kuondoa hilo Haji akatafuta justification
Haji majuzi kupitia account yake ya Instagram ndio alienzisha vita ya Nani kaingiza mapato mengi ila cha ajabu haikuishia hapo club nayo ikaamua kulitangaza official
Hivi vilabu havijaanza leo kufanya haya matamasha ila kulikuwa hakuna ushamba wa kutambiana nani kaingiza hela nyingi kuliko mwingine, imeanzia kwenye tabia ya kutokubali kushindwa Kwa Manara na sasa kila kitu kimekuwa ni kama vita vile
Kwahiyo ukiangalia baadhi ya Mambo vile yanaenda pale Yanga utagundua kuwa ni kweli Haji ana nguvu flani au kuna nguvu ya mtu mkubwa nyuma yake, ambae obviously atakuwa ni Raisi wa club
Kutokana na hizo Mambo, Kuna kamba nyembamba sana inatenganisha ukweli na uongo wa ule uvumi kuwa Raisi na Muhamasishaji kuna kitu kinaendelea Kati yao
Anyway, kupanga ni kuchangua