Kuna umuhmu wa vijana wote wakimaliza standard 7 waende jeshi miezi 3 na zaidi, vijana wengi wanaanza kupoteza uzalendo
Badala ya kuwapa watu elimu ya maarifa tunawapa watu ukatili.
Hao hao ndio watakuja kuondoa mfumo muovu watakapogundua kuwa kesho yao imehujumiwa na kundi dogo linalowatumia kujilimbikizia mali. Ukumbuke vijana hawa waoga ni zao la kizazi kilichokua bila kupitia JKT .
Watamaliza JKT kama taifa moja lakini watashangaa kuona wenzao wanaajiriwa kikanda ,kidini, kiitikadi,kujuana, na upendeleo wa kila aina. Hapo moto wake mtakumbuka mfumo wa vyama vingi.
Uzalendo bila usawa ni kama kuahirisha matatizo kwa kunywa pombo na kulewa.
Enzi za Chama kimoja Kwenda JKT ilikua ni lazima na uzalendo uliimbwa midomoni tangu shule ya msingi.
Maandamano Chuo kikuu yalikua hayakomi. Maandamano ya wafanyakazi yalikua hayaepukiki mana walikua Jasiri.
Lakini usisahau kuwa kule Jeshini wanafundishwa kuwa Polisi ni kama wanawake tu ,hivyo hawaogopi polisi.
Ile CUF Ngangari ya Kina Lipumba ilikua ni zao la vijana waliopita JKT.
Walioondoa JKT baada ya Mfumo wa vyama vingi kuingia hawakua wajinga. Waliona mbali na walijua wazi kuwa sasa ulimwengu umebadilika na viongozi wanachaguliwa kwa ridhaa ya wananchi wenyewe hivyo hakuna haja ya kutumia nguvu. Sasa mnawarudisha watu kwenye kutumia nguvu wakati mlishindwa wakati huo Nchi ikiwa na Watu mil. 27 ,lao watu mil.60 wanataka kuchagua viongozi wao wenyewe ili wawaongoze na kuwasikiliza badala ya kuwatawala kimabavu.
Amini usiamini Ipo siku isiyojulikana ambapo CCM itaangushwa ghafla bila kutegemea kutokana na ubaguzi mkubwa uliojengwa awamu hii. Hata ukifuatilia wanaomtisha Lisu na wale waliokua wanawanyanyasa wapinzani walikua wanafanya hivyo kikikakati ya kulinda himaya zao walizozipewa kinyumbani.
Watu watawakataa siku moja kwa ghafla bila kujiandaa hapo ndipo hata mali walizojilimbikizia makada zitakapo vakimiwa kama shamba la Sumaye lilivyokuwa limenyakuliwa na wananchi.
Watu watafanya tathmini na watabaini kuwa Makada wa CCM ndio wanaokalia mali zote zilizopo nchini kila kona ya nchi lakini pia wanawatumia watoto wa maskini ndani ya vyombo vya dola kulinda mali zao na vyeo vyao walivyopata kidhalimu.