Uchaguzi 2020 Kumbe kuna hatari ya kukosa Trilioni 2 kutoka kwa Wahisani kutokana na Kasoro za Uchaguzi(?)

Uchaguzi 2020 Kumbe kuna hatari ya kukosa Trilioni 2 kutoka kwa Wahisani kutokana na Kasoro za Uchaguzi(?)

Mmeanza propaganda [emoji1787][emoji1787][emoji1787] mbona bado
 
Ndugu yangu uko Tanzania ya wapi wewe bado unawaza misaada.Jiwe ameshaondoka huko. Tayari tuna viwanda viwili vya kuchengua dhahabu, mpaka sasa tunauza dhahabu safi siyo ghafi tena.Tuna dividend kila mwaka toka bariick, tumepata certificate ya bati yetu. Kifupi ni kwamba TANZANIA kwa sasa ni mafuta.
Tunajitegemea kila kitu sasa kwa pesa zetu za ndani hatuhitaji misaada TUTAKOPA!!!
Sisi ni inchi tajiri hatupaswi kuombaomba!!!
 
Watateuliwa wabunge kutoka nccr, udp na tlp watasimamia kamati. Mchezi
 
Anaandika Leonce Marto wa CHADEMA kupitia mtandao wa Twitter:

Kanuni za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinataka kamati za kudumu za PAC na LAAC ziongozwe na wapinzani, CHADEMA hatupeleki Wabunge wa Viti Maalum na hatutaki kunajisi chombo hiki muhimu cha wananchi.

Mtakosa 2 Trillion za Donor Countries kwa nchi kukosa utawala Bora

Mengi yanakuja CCM jiandaeni.
Busara na hekima ni jambo muhimu sana kwenye maisha ikiwa ni pamoja na siasa. Salary Slip naona CHADEMA wanataka kurudia kosa lile lile. Ni wazi kuwa bado hawajajifunza kuhusu nini wananchi wanataka, nini kinaweza kutumika kuwaadhibu na zaidi sana nini maana ya kuweka mbele maslahi mapana ya nchi dhidi ya maslahi ya chama.

Nadhani ni bora hata mwandishi asingeandika, wangekaa tuu wajadiliane wenyewe. Trilioni 2 haziendi lumumba bali zingetumika kwa huduma za wananchi. Hivi mfano CCM ikishindwa kutekeleza baadhi ya ahadi zake halafu uchaguzi wa 2025 ikaenda kuwaambia wananchi wa Kyekelo kuwa tulikuwa tupate trilioni 2 za kuwajengea barabara ya lami lakini CHADEMA wamezuia, itakuwa wamekosea?

A
 
Busara na hekima ni jambo muhimu sana kwenye maisha ikiwa ni pamoja na siasa. Salary Slip naona CHADEMA wanataka kurudia kosa lile lile. Ni wazi kuwa bado hawajajifunza kuhusu nini wananchi wanataka, nini kinaweza kutumika kuwaadhibu na zaidi sana nini maana ya kuweka mbele maslahi mapana ya nchi dhidi ya maslahi ya chama.

Nadhani ni bora hata mwandishi asingeandika, wangekaa tuu wajadiliane wenyewe. Trilioni 2 haziendi lumumba bali zingetumika kwa huduma za wananchi. Hivi mfano CCM ikishindwa kutekeleza baadhi ya ahadi zake halafu uchaguzi wa 2025 ikaenda kuwaambia wananchi wa Kyekelo kuwa tulikuwa tupate trilioni 2 za kuwajengea barabara ya lami lakini CHADEMA wamezuia, itakuwa wamekosea?

A
uchaguzi ulirubuniwa sasa mnataka nini?
kwanza hizo trillions 2 ni za wazee wa
Mavi 8 Sisi hatuzioni

bado uingereza ambayo hutoa theluthi ya bajeti wana jambo Lao safari hii

dhulma hauzai.... inaua
 
Wananchi wataona kumbe upinzani nao unaamua mambo ya maisha yetu watakuwa wamepata awareness na serikali pia itajifunza. Pia wale wanaotumika kusaidia wizi watapata somo.
 
Baada ya njia ya uchaguzi kuzimwa kidikteta Kuna njia kuu mbili tu zimebaki za kuleta demokrasia na uhuru wa kweli Tanzania nazo ni ama Wananchi kuandamana au kutumia mbinyo wa jumuiya za kimataifa; Tanzania hakukuwa hi kujitokeza wakati mzuri wa kutumia mbinyo wa jumuiya za kimataifa kama huu uliotayarishwa na ccm wenyewe. Kutokana na wananchi kutishiwa na kuumizwa na vyombo vya dola pale wanapotaka kuandama na ili kuepusha vifo na vilema kwa wananchi wasio na hatia njia pekee iliyobaki ya uhakika ni kutumia mbinyo wa jumuiya hizi. Viongozi wetu wa upinzani watumie mwanya huu kwa umakin mkubwa sana sababu bahati kama hii haiji mara mbili. Waieleze dunia kwa maneno na ushahidi wa moja kwa moja na wa kimazingira (ambao ni mwingi umejaa kila kona) kwa namna ambavyo dunia itaelewa kinagaubaga uzito wa ubaya kidemokrasia uliopo Tanzania kwa sasa. Kila hatua inayowezekana ichukuliwe na jumuiya za kimataifa kwa uzito ambao utapeleka machungu ya kutosha kwa mtawala na kundi lake. lengo kuu iwe ni uchaguzi urudiwe chini ya tume huru ya uchaguzi. Kukubali teuzi uchwara bungeni au serikalini hakutakaa kamwe kulete katiba mpya Tanzania bali itakuwa ni kutukanwa na kudharauliwa kwa upinzani kwa namna isiyoelezeka na pia itakuwa ndiyo mwanzo wa kifo rasmi cha upinzani na demokrasia nchini.

upinzani msisahau mwaka huu mgombea urais wenu aliyenyang'anywa haki yake ni mtu jasiri, mwenye akili na uwezo, na ni so eloquent pengine kuliko Mtanzania yeyote yule; mtumieni huyu jamaa kuleta mbinyo Tanzania na kuelezea mateso ya watanzania tunayoyapitia ili dunia ielewe. Pia msisahau aliyeshinda kiti cha urais marekani si Trump bali ni yule mdemokrasia Joe Biden. yaan mazingira yote yamejiweka vizuri kwa akili yenu wapinzani myatumie...kazi kwenu sasa.
 
Mwanachama mwenzetu gani wakati wanataka kuweka mapandikizi ya CCM? Tunawaonya wasijaribu huo ujinga!
Usichanganye mafaili ndugu, rejea kwenye post uliyoirusha iliyokua ikisema hivi👇🏾
Watakayemweka kwamba ni mpinzani tukimjua ama zake ama zetu! Labda wahamishie battalion nzima nyumbani kwake na kwa ndugu zake!
Hapo ulimaanisha nn?? Kama sio kutaka kuutoa uhai wa huyo mpinzani??
 
Ni mataahira kama wewe tu huwa wanaweza kuamini hizi ngonjera unazozisema, eti pesa za ndani.


Yuko sahihi.
Mtu anaweza kuwa na hela ya kununua nguo za ndani lakini pesa ya kununua nguo za kuvaa nje ikawa mtihani.
Tatizo linakua huwezi kutembea hadharani ukiwa umevaa nguo za ndani .
 
Ujanja mwingi, mbele kiza.
Sana, especially pale taasisi inapojipambanua kwa uanaharakati wa kisiasa halafu kumbe humo ndani yake kunakuwa na mambo kama ya ughaidi wa chini chini yakiwa yanaendelea. Mimi siku zote nilishasema mtu usijaribu kuipa dola kazi, iache dola ikupe wewe kazi, kama itakuona kuwa unafaa kupewa kazi. Ujanja mwingi, mbele kiza.
 
Kuna umuhmu wa vijana wote wakimaliza standard 7 waende jeshi miezi 3 na zaidi, vijana wengi wanaanza kupoteza uzalendo

Badala ya kuwapa watu elimu ya maarifa tunawapa watu ukatili.
Hao hao ndio watakuja kuondoa mfumo muovu watakapogundua kuwa kesho yao imehujumiwa na kundi dogo linalowatumia kujilimbikizia mali. Ukumbuke vijana hawa waoga ni zao la kizazi kilichokua bila kupitia JKT .
Watamaliza JKT kama taifa moja lakini watashangaa kuona wenzao wanaajiriwa kikanda ,kidini, kiitikadi,kujuana, na upendeleo wa kila aina. Hapo moto wake mtakumbuka mfumo wa vyama vingi.
Uzalendo bila usawa ni kama kuahirisha matatizo kwa kunywa pombo na kulewa.
Enzi za Chama kimoja Kwenda JKT ilikua ni lazima na uzalendo uliimbwa midomoni tangu shule ya msingi.
Maandamano Chuo kikuu yalikua hayakomi. Maandamano ya wafanyakazi yalikua hayaepukiki mana walikua Jasiri.
Lakini usisahau kuwa kule Jeshini wanafundishwa kuwa Polisi ni kama wanawake tu ,hivyo hawaogopi polisi.
Ile CUF Ngangari ya Kina Lipumba ilikua ni zao la vijana waliopita JKT.

Walioondoa JKT baada ya Mfumo wa vyama vingi kuingia hawakua wajinga. Waliona mbali na walijua wazi kuwa sasa ulimwengu umebadilika na viongozi wanachaguliwa kwa ridhaa ya wananchi wenyewe hivyo hakuna haja ya kutumia nguvu. Sasa mnawarudisha watu kwenye kutumia nguvu wakati mlishindwa wakati huo Nchi ikiwa na Watu mil. 27 ,lao watu mil.60 wanataka kuchagua viongozi wao wenyewe ili wawaongoze na kuwasikiliza badala ya kuwatawala kimabavu.

Amini usiamini Ipo siku isiyojulikana ambapo CCM itaangushwa ghafla bila kutegemea kutokana na ubaguzi mkubwa uliojengwa awamu hii. Hata ukifuatilia wanaomtisha Lisu na wale waliokua wanawanyanyasa wapinzani walikua wanafanya hivyo kikikakati ya kulinda himaya zao walizozipewa kinyumbani.
Watu watawakataa siku moja kwa ghafla bila kujiandaa hapo ndipo hata mali walizojilimbikizia makada zitakapo vakimiwa kama shamba la Sumaye lilivyokuwa limenyakuliwa na wananchi.
Watu watafanya tathmini na watabaini kuwa Makada wa CCM ndio wanaokalia mali zote zilizopo nchini kila kona ya nchi lakini pia wanawatumia watoto wa maskini ndani ya vyombo vya dola kulinda mali zao na vyeo vyao walivyopata kidhalimu.
 
Usichanganye mafaili ndugu, rejea kwenye post uliyoirusha iliyokua ikisema hivi👇🏾

Hapo ulimaanisha nn?? Kama sio kutaka kuutoa uhai wa huyo mpinzani??
Kwani waliowaua huko Pemba siyo binadamu? Wacha tumtoe tu kwa maana wanataka kupandikizwa kwa ngozi ya upinzani wakati ni ma-CCM!
 
Sana, especially pale taasisi inapojipambanua kwa uanaharakati wa kisiasa halafu kumbe humo ndani yake kunakuwa na mambo kama ya ughaidi wa chini chini yakiwa yanaendelea. Mimi siku zote nilishasema mtu usijaribu kuipa dola kazi, iache dola ikupe wewe kazi, kama itakuona kuwa unafaa kupewa kazi. Ujanja mwingi, mbele kiza.
CCM kuiba kura ili kufuta upinzani bungeni, wakati inahitaji wapinzani bungeni ili kupata uhalali wa bunge kimataifa ni ujanja mwingi, mbele kiza.
 
Back
Top Bottom