Kumbe kuna uhaba wa USD ($) Tanzania?

Kumbe kuna uhaba wa USD ($) Tanzania?

Unaujua uchumi wa India au Brazili? We mjinga India kwa sasa ni ya 5 kama sio ya nne kwa uchumi mkubwa, inapitwa na USA, China, Japani, na Ujerumani basi
Mimi naongelea mashiko ya huo muunganiko. Wameungana kujitutumua tu na kupiga picha, hata haiweleki nini wanafanya, wananufaikaje nao au wanasimamia nini.
 
Si benki kuu ya Marekani federal reserve wamepandisha interest rate ? , hivyo uhaba wa cash ni lazima ,na wanazidi kuipandisha ili kupambana na mfumuko wa bei
Mataifa wanao import zaidi kuliko ku export watapata tabu sana kipindi hiki Fed wakifanya yao kupambana na Inflation.
Bado wengine wana mizigo ya madeni ya kulipa kwa dola!
 
Unaujua uchumi wa India au Brazili? We mjinga India kwa sasa ni ya 5 kama sio ya nne kwa uchumi mkubwa, inapitwa na USA, China, Japani, na Ujerumani basi
India ishirikiane kiuchumi na adui yake namba moja China? Ambaye aliifanya hadi itumie gharama kubwa kutengeneza silaha za nyuklia, ambaye walipigana vita na mpaka leo wanagombea mpaka? Ambaye ndio military partner mkuu wa adui yake namba mbili, Pakistan?

Brazil humo kwenye BRICS iachane na Marekani na washirika wake iungane na China na Russia muuza gesi, na India? Unajua tech transfer na biashara inayofanywa na Brazil na Western countries, iachane na hizo ikajiunge kwenye sarafu ya BRICS?

South Africa kabisa we unaona itajiunga kwenye hiyo sarafu na uchumi wake usioeleweka siku hizi. Yani BRICS itafanya lipi la kuizuia $, kwani BRICS tangu 2009 imeanza kuna kipi imefanya
 
Uchina yuko kote Urusi na US,EU.
Nawacheka sana watu ambao wanasema dedolarisation ,hizo ni ndoto ya alinacha ya watu ngumbaru wasiojua uchumi kiundani , we subiri miezi mingine hata minne mpaka sita utaona balaa lake hasa nchi zetu hizi ,nasikia wanataka kuongeza step tena kupandisha interest rate .
Yaani Dollar tutake tusitake ni lazima tuitafute na tusipofanya hivyo cha moto tutakiona ,tutakuwa kama Zimbabwe, Siri Lanka ,Aregentina , Pakistan ,Lebanon ,Venezuela ,Cuba na shitholes nyingine zilizofilisika kiuchumi tu ,Dollar Ndio medium of transaction Kwa kiasi kikubwa huyo mchina na yuan yake hafiki hata asilimia 5 ya Transactions zinazofanyika kwa yuan Dunia nzima , hapo hapo china Dollar transaction asilimia 47 yani juzi juzi tu hapa ndio yuan imefikia asilimia 48 kwa mara ya kwanza kihistoria sasa imagine .
 
Jamani tuwe tunasoma soma kidogo! Tatizo la uhaba wa USD currency sio la Tanzania peke yake, hili ni tatizo la dunia yote. Please soma link hizi hapa chini kwa taarifa zaidi



Halafu nyie machawa huwa mnapenda kujificha sana kwenye kichaka cha swala la dunia
 
Nchi masikini za Afrika zinajenga uchumi wa china na kumnufaisha china bila kujua , unaagiza bidhaa nyingi kuliko unachouza nje ,mwisho wa siku wewe ni looser Maana hutakiwa na pesa za kigeñi na thamani yako ya pesa itashuka
Huna option labda Serikali izuie msululu wa bidhaa za kutoka China kiasi ikifanya hivyo na wao wanajibu Kwa kuweka vikwazo vya uhafifu wa bidhaa zenu..

Njia pekee ni kuzalisha import substites na kuongeza investments zako tuu.
 
Back
Top Bottom