Kumbe kuna uhaba wa USD ($) Tanzania?

Kumbe kuna uhaba wa USD ($) Tanzania?

Mimi naongelea mashiko ya huo muunganiko. Wameungana kujitutumua tu na kupiga picha, hata haiweleki nini wanafanya, wananufaikaje nao au wanasimamia nini.
Wanataka waache kutumia Dola ,mbona India na Russia wanauziana mafuta bila Kutumika Dola? Labda watakwama kama wakitaka bidhaa zingine Nje ya Nchi zao watalazimika tena kutafuta Dola.
 
Halafu nyie machawa huwa mnapenda kujificha sana kwenye kichaka cha swala la dunia
Kwani wewe unaona ni swala la Tzn pekee? Nchi ngapi Zina shida hii?

Sababu za hapa ziko nyingi sana yoote imeletwa na covid 19 na vita ya Russia ndivyo vilisababisha kupanda Kwa bei ya vitu muhimu Dunia nzima..

Kitu ulichokuqa unaagiza Kwa Dola chache Sasa unatumia Dola nyingi kuagiza hicho hicho wakati uwezo wako kuzalisha Dola nyingi ni mdogo .
 
Kila siku tunanunua mavitu kwa pesa za nje miradi yote tunalipa kwa Dollars
Meanwhile hakuna tunachofanya kupata hizo dollars hatuuzi vitu nje
Walitegemea izo pesa hazina hazitaisha?
Miezi zaidi ya 5 dollar haipo banks wanasema hawawezi kukupa peke ako dollar 8000 waache wengine
Kama una kihela chako hauna mpango nacho usiweke fixed acc kanunue dollar sindika ndani mpaka mama atoke unaenda unachange
 
Sina uhakika kama una ufahamu wa kutosha juu ya hii kitu inayoitwa BRICS. Na utakuwa unatazama sana habari za BBC, Sky News, CNN, na hizo media za kimagharibi ambazo kutwa kazi yao ni kupotosha.

Uyo ni wale Brainwashed wanafikiri US ndo kila kitu. Ishu ni kwamba dollar itazidi kupotea taratibu alternative ni kuanza kutumia sarafu nyingine
 
Wanataka waache kutumia Dola ,mbona India na Russia wanauziana mafuta bila Kutumika Dola? Labda watakwama kama wakitaka bidhaa zingine Nje ya Nchi zao watalazimika tena kutafuta Dola.

Nchi za Asia asilimia kubwa zinatumia local currencies. Sisi maskini Africa ndo bado tunapambana na dollar, tulikua tunawaaambia Russia na nchi nyingi zimeipiga chini dollar haya ndo matokea naona US hana habari na kuprint pesa [emoji23][emoji23]
 
Hata hizo nchi ulizozitaja zina reserve za kutosha za USD, achilia mbali uwekezaji waliofanya ama serikali zao ama matycoon wao wote upo katika usd.

Leo hata hao suppliers wa china sijui india wanakomaa walipwe kwa dollar. Hawataki kusikia kbs habar za currency za nchi zao.

Ila kinachoshangaza bongo ni exchange rate. Naona mamlaka imeamua kuifix/peg.

Athari zake ni kubwa sana, ikiwamo black markets, wananchi kuitilia shaka financial system na watu ku hold hard cash in usd bila kuziweka kwenye mifumo rasmi.
 
Eeeh tuambie impact ya Dola nini ikiwa haipo kwa wingi kwa nchi yetu.

1. Tunaweza kushindwa kulipa mikopo yetu ambayo mingi ipo katika sarafu ya usd

2. Upande wa biashara hasa kwenye kuagiza bidhaa nje itatuwia ugumu.

3. Mashaka ya uchumi wetu hasa kwa wawekezaji.

4. Masoko ya mchongo, maana haipekiki usd, mamlaka zitashindwa kudhibiti mfumo wa fedha hivyo kukosa kuaminiwa.

5. Mfumuko wa bei na riba kuongezeka. Riba kuingezeka ili kuwavutia wawezeji kuweka fedha zao huku, lakini kwa wakopaji ikawa kilio.
 
Hata hizo nchi ulizozitaja zina reserve za kutosha za USD, achilia mbali uwekezaji waliofanya ama serikali zao ama matycoon wao wote upo katika usd.

Leo hata hao suppliers wa china sijui india wanakomaa walipwe kwa dollar. Hawataki kusikia kbs habar za currency za nchi zao.

Ila kinachoshangaza bongo ni exchange rate. Naona mamlaka imeamua kuifix/peg.

Athari zake ni kubwa sana, ikiwamo black markets, wananchi kuitilia shaka financial system na watu ku hold hard cash in usd bila kuziweka kwenye mifumo rasmi.

Zitaje hizo nchi uwe unakuja na facts
 
1. Tunaweza kushindwa kulipa mikopo yetu ambayo mingi ipo katika sarafu ya usd

2. Upande wa biashara hasa kwenye kuagiza bidhaa nje itatuwia ugumu.

3. Mashaka ya uchumi wetu hasa kwa wawekezaji.

4. Masoko ya mchongo, maana haipekiki usd, mamlaka zitashindwa kudhibiti mfumo wa fedha hivyo kukosa kuaminiwa.

5. Mfumuko wa bei na riba kuongezeka. Riba kuingezeka ili kuwavutia wawezeji kuweka fedha zao huku, lakini kwa wakopaji ikawa kilio.

Ndo muda muafaka wa kutrade kwa local currencies msiipe dolla kichwa sana
 
Matatizo mengine ya kujitakia huko nyuma mlisha-ambiwa kuna watu wanatumia bureau de changes kutakatisha hela wanazoiba na wanaogopa kuziweka banks kwa majina yao (majizi serikalini na wauza nganda).

Kwenye kufanya ivyo wanawekeza hizo hela haramu kama mitaji kwenye bureau de change. Hizo hela za kitanzania zinanunulia foreign currency na kusababisha demand kuwa kubwa hasa ya dollar, kuleta uhaba na thamani yake kupanda.

Akaja yule mtu mnaemwita mshamba akataka bureau de change zionyeshe source za mitaji yao wakishindwa anataifisha hizo hela; wenye vitabu na kuweza kufanyiwa forensic auditing kuthibitisha hakuna sources of investment zisizoeleka hawakuwa na shida. Ukishindwa kuthibitisha sources ya mtaji wako imekula kwako.

Hizo zilikuwa hatua za kuondoa artificial demands zinazosababisha dollar kuhitajika; mkasema anaua uchumi. Lakini baada ya hatua hizo exchange rate ilikuwa stable kwa miaka yote hiyo.

Sasa hivi marehemu hiyo michezo imerudi sasa mnalalamika nini; si tunataka wenyewe. Tena huyo Maria Sarungi ndio anatakiwa kuwa mtu wa mwisho kulalamika na wendawazimu wenzake wa Twitter.

Kwenye uchumi wowote kunapokuwa na hela nyingi ambazo chanzo chake sio uzalishaji halali, tegemea shortages, inflation ambazo chanzo chake ni artificial activities.

Juzi watu wamerudishiwa hela zao ambazo walishindwa kuelezea wamezitoa wapi na leseni za kuendelea na biashara zao za bureau de change. Ilhali ufisadi umerudi kwa nguvu na biashara ya madawa ya kulevya; sasa mnashangaa nini.

Magufuli wasn’t perfect kuna mambo kadhaa alifanya hasa mwanzoni mwa uongozi wake yaliyo kera na ndio anayo hukumiwa nayo. Lakini wengi awakuelewa vita aliyokuwa akipigana na majizi kwa maslahi mapana ya watanzania; alikuwa mzalendo mwenye kuipenda nchi na raia wake.

Sasa leo sijui mnalalamika nini si ndio mnayoyataka haya; we unadhani hii mijizi na wauza unga hela zao wataficha wapi.
 
Mwamba ameondoka kaicha BoT in reserve ya $5 billion; aijawahi tokea katika historia ya Tanzania. Ndani ya mwaka walizalamba zaidi ya $3 billions kulipia madeni kwa sababu ya makusanyo hafifu kutoka TRA.

Halafu hapo hapo wanamsingizia kuwaongezea madeni wakati mwenyewe yupo hai alikuwa akiyalipa bila ya shida ndani ya muda wake wote.

It’s OK watu wenye elimu ndogo kumtukana Magufuli; lakini uwezi kuwa msomi (pamoja na mapungufu yake) halafu usimuelewe Magufuli alikuwa analenga nini labda uwe sehemu ya mafisadi.
 
Mataifa wanao import zaidi kuliko ku export watapata tabu sana kipindi hiki Fed wakifanya yao kupambana na Inflation.
Bado wengine wana mizigo ya madeni ya kulipa kwa dola!

Waziri wa fedha anasema eti uchumi wetu uko vizuri kwavile tunalipa mishahara yetu kwa wafanya kazi ; lakini hazungumzii uwiano wa mapato yetu kama nchi na madeni tunayotakiwa kulipa na kwa wakati gani!!
Next year 2024 kama nchi inatakiwa ilipe madeni kiasi gani yale ya nje[ $$$$$] na yale ya Ndani[ T shs}. Tunategemea mapato kiasi gani [ Total revenue] mwakani? Je tunauwezo wa kulipa madeni yaliyoiva kutokana na mapato yetu?
Hapo akijibu hayo maswali ndio tunaweza kupima hali ya uchumi wa nchi yetu, vinginevyo anatupiga sound tu!
 
Tanzania haina "DOLLAR SHORTAGE".......

Kwa hivi karibuni nchi ambazo zimekuwa na uhaba wa Fedha hiyo ya kigeni ni :-

1)Nigeria... mwaka 2022....

2)Sudan....mwaka 2018 kupelekea mpaka bei ya MKATE ikapanda na kusababisha MACHAFUKO....na mwendelezo wake uko mpaka leo.....

Tanzania pamoja na msukosuko wa COVID 19....tumebaki IMARA zaidi ya CHUMA.....

Makali ya kuadimika kwa DOLA tungeyaona vyema tu huku mitaani....chukulia mfano SUDAN ilipelekea MKATE tu kupanda bei.....

#SiempreJMT[emoji120]
 
Back
Top Bottom