- Mkuu wangu heshima sana, in my opinion ni kwamba hapa Wapenzi wa Chadema wanashindwa ku-grasp the big picture kwamba Mwenyekiti wa Chadema jana aliksoea kutojibu hii hoja, kinachotakiwa hapa ni fundisho kwamba next time awe muangalifu na hasa wasaidizi wake, maana this falls right in their hands, mmojawapo alitakiwa kufikiri haraka sana na kugundua hili na kumpasia ki-note ili aliseme hata kama muda wa debate umekwisha, that is all I could ask!
- Mkuu wangu sana, mimi ni mfuatiliaji sana wa mambo ya katiba za mataifa mbali mbali, hakuna katiba ya taifa lolote Duniani, ambayo ina mwanya wa urahisi rahisi katika kurekebishwa, kule Zambia walijaribu hili la kukurupuka na kurekebisha katiba kumbe Chiluba alikuwa na mikakati yake ya siri ambayo thanks to Mwanawasa, ikaja ikamlipukia usoni akashindwa kufanya alichotaka yaani kuwahadaa wa-Zambia, ili aendele na madaraka, Kenya tumejionea wananchi walivyogoma kabisaa through their votes kwamba hawataki kina Kibaki waiguse katiba maana hawawaaamini, USA ndio kabisaa huwezi gusa katiba bila mpango maana Judicial Branch watakulima tena kiroho mbaya sana, kama walivyokataa kusikiliza kesi ya uchaguzi ya New Jersey State.
- Sawa ninaikubali hoja yako kimsingi kwamba katiba yetu ina upungufu inahitaji marekebisho, tatizo langu ni nina wasi wasi kwamba a lot is missing katika kuirekebisha hii katiba, unahitaji wananchi ambao so far sio siri hawaonyeshwi kuona tatizo na katiba yetu kuacha wananchi wachache sana wanaopiga kelele, sasa huwezi kubadili katiba bila kuwa sambamba na wananchi, tuwapeni nafasi wananchi ambao tayari wameshaanza kuonyesha kuamka usingizini, waamke vizuri ama sivyo tutakuwa tunafukuza hewa! Nimesema mara nyingi sana na ninarudia tena kwamba huwezi kuwa na political system ya Checks and Balance katika taifa ambalo uwiano wa wabunge uko kama hapa kwetu Tanzania, na huwezi kulazimisha kuongeza wabunge wa Upinzani kwa kutumia katiba, Demokrasia ina njia moja tu inayokubalika sana na ni perfect sana nayo ni votes, yaani kura za wananchi.
- As much as ninaheshimu sana mafanikio ya Chadema recently, lakini I am not going over my head na kuanza kuamini kwamba wamepata mafanikio makubwa sana ya kuwapa mandate ya wananchi wengi on kubadilisha katiba, halafu infact taifa letu bado ni changa miaka 50 sio mingi sana kwa taifa lililokuwa under chama kimoja, kwamba ukitoa miaka 15 ya vyama vingi unaweza kupata busara ya kubadili katiba na uwiano uliopo sasa, hapana hiyo katiba itaishia kupwaya tu ndugu yangu. Kwa mfano NEC, inawezaje kuwa fair under our political system ya sasa, unless imechaguliwa na kusimamiwa na Chadema, sasa how could that be possible wakati CCM ndio majority boom your stuck, I mean dead end, sasa why waste time na hoja zisizojadilika ma kutaka kulazimisha kwa nguvu?
- Chadema wajiimarishe zaidi kwenye chaguzi, wananchi wameonyesha mwamko na kuanza kuamka usingizini wapeni time, tumejionea jinsi wananchi walivyoyazingira majengo ya kutoa matokeo ya uchaguzi, itawachukua muda kuelewa kwamba wanachohitaji ni kuchagua wabunge wengi wa Upinzani inaitwa political maturity ambayo inahitaji progress, sasa ukiilazimisha hiyo utakuja kuleta matatizo makubwa sana kwa taifa mbele ya safari kwa sababu utakua unalilia short term results over long term, I mean mtoto anakuwa sasa aachiwe akue, sawa kupiga makelele inakubalika lakini yawe makelele ambayo yako samba samba na political realities on the ground!
- Well, thanks for the compliment ninaamini umetoa huu ushauri kutokana na kupima uwezo wangu wa kuelewa siasa zaidi kuliko kujali jina la familia na kaka yangu au generations!
Thanks.
William.