Mheshimiwa Willima, Heshima sana,
Kwanza napenda kukupongeza kuwa kila mara wewe huleta hoja zinazojadilika na kuzungumzika humu jf. Leo umenichosa na mtazamo wako hasi juu ya suala la mabadiliko ya katiba na hata mfumo mzima wa NEC. Nadhani haya ni matokeo ya kutoshiriki siasa za nyumbani moja kwa moja na kuona matatizo yanayotuzunguka kama taifa.
Wakati huu tusipoziba ufa ujuwe kwa hakika tutajenga ukuta na utakuwa huko ulipo ukitoa ushauri na maoni kwenye mtandao kama unavyofanya leo. Ziko sababu za kutosha za katiba yetu kutazamwa upya kabisa
1. Suala la Muungano: Mfumo wa sasa hauturidhishi watanzania tlio wengi, na Kataba haiko clear kuhusu jambo hili, leo Zanzibar wana Makamu wa rais wawili ambao hawapo katika katiba yetu ya Jamhuri kwa sababu tu ya mfumo wa Zimamoto, Uwiwano wa uongozi na mzigo mkubwa unaobebwa na raslimali za bara kuendesha Zanzibar ni moja ya Changamoto kubwa.
2. Upatikanaji wa tume ya uchaguzi na namna inavyofanya kazi; Uchaguzi huu tume bila aibu inawaambia watanzania matokeo ya kawe na Ubungo yamechelewa kutangazwa kwa sababu ya matatizo ya miundombinu ya usafiri huku ikiwa tayari imetangaza matokeo ya Ngorongoro, Hivi Will huko US ndivyo mnavyofanya kazi kweli? Tume inasubiri watu wapigwe mabomu Mwanza ndiyo itangaze matokeo alafu unaipigia makofi Willy? Uko wapi uwiano wa Demokrasia unaouzungumzi! Alafu hakuna sheria ya kuwawajibisha hawa watu kisha unasema katiba inatosha iko sawa!! Ahaaa mzee think twice hapo, Tumeona katika kampeni hizi wakuu wa wilaya wakisoma taarifa za kazi kwa RizI ili mtoto asiharibu unga kwa baba, nguvu nyingi za serikali zimetumika kwenye kampeni kubeba chama tawala kwa sababu ya ubovu wa katiba, Hakuna mwenye chuki na RZ1 mbona nyie hatukuwaona mkitumia nafasi za wazee wenu ku propage siasa?? Rais ana vyeo vyingi mno vya kuteua watu na hivyo wanalazima kutumika kwa namna yoyote ili walinde nafasi zao alafu unasema hatutaki katiba itakayopunguza nguvu ya Rais, Bunge liliazimia mambo mengi baada ya Saga ya richmond, kwa sababu ya katiba mbovu hayakuenda popote maan na hiari ya Mkulu kuyafanyia kazi au kuyashiti, Hii ni aibu Willy nchi inahitaji katiba kabla kina Kayumba hawajachoka, watauana vibaya watakapochoshwa na mfumo unaoongeza mzigo wa umaskini vichwani mwao na kwa kuwa hutakuwepo utafuatilia kwenye Luninga na mtandao huku ukishaa. Mzee nchi inahitaji katiba iweke mambo sawa.
Mimi sikupiga kura mwaka huu, nina sababu nyingi za hovyo hovyo tu, moja ni kuchoshwa na mfumo mbovu usio na matumaini ya kumkomboa mtanzania, huko US manesi na madaktari ni moja kati ya makundi yanayolipwa vizuri hapa kwetu malipo mazuri yako kwenye siasa (Consumer unawalipa vizuri kuliko wanasayansi producer) Alafu Willy bado hutaki katiba eti tukuwe, hatuwezi kukuwa chini ya mfumo mbovu huu tuliionao ila tutadidimia
Mzee nina mengi lakini ngoja niache tu. nCHI INAHITAJI MABADILIKO YA KATIBA KABLA AKINA KAYUMBA WA MANZESE, BUGARIKA, MABATINI, HAWAJACHOSHWA NA HUU UFUKARA WA KUPINDUKIA
- Mkuu heshima yako sana, sikatai kwamba katiba yetu ina mapungufu ni kweli sana isipokuwa tatizo langu ni how to go about kuirekebisha kwa maudhui ya wananchi wote, wengi mnaolilia kubadilishwa mnaonekana kuwa na hisia kali sana bila kujali POLITICAL FACTS on the ground, hamuwajali kabisa wananchi wengi walioichagua CCM kushika power kwenye huu uchaguzi. Mnaonekana kuamini sana kwamba ni nyinyi tu Chadema wenye wabunge 46 ndio wenye mandate ya wananchi kuhusu the political future of our nation.
- Mnakosea sana, ushauri wowote wa kubadili katiba lazima uwajali CCM kwanza kwa sababu wananchi ndio wamewachagua for the last 50 years, nimesema na ninarudia kwamba Demokrasia, inataka wananchi wazungumze kupitia kwenye kura, kama kweli unaamini in Demokrasia then utaelewa point yangu kwamba ni vigumu sana kuibadilisha katiba under political system ya CCM wabunge 270 Vs Chadema wabunge 46, it is simply impossible. Otherwise inaonekana mnashauri tuvunje katiba, yaani tutumie njia za mkato kuirekebisha kwa ku-overpass katiba inayodai 2/3 ya wabunge kuirekebisha kikatiba,
- Kwa maneno mengine tuvunje katiba kwa ajili ya kuirekebisha katiba, ili wabunge wa upinzani 46 wawe na nguvu sawa na wabunge 270 wa chama tawala, hivi mkuu huoni kwamba itakua the joke of the century! Ninawaulizeni swali dogo sana, under your new proposal ya katiba mpya ili NEC iwe fair inatakiwa kuchaguliwa na nani?
William