Elections 2010 Kumbe kuna wabunge kumi wa chadema hawajatoka Bungeni Rais alipokua akihutubia bunge


- Nilichosema na ninachosema tena ni kwamba tusikimbikilie kutembea kabla ya kutambaa, maana ukienda Bumbuli naamini utaambiwa CCM sio mchezo, polisi wote wako upande wa ushindi!

William.
 

- Kuongezeka kwa Demokrasia hakuwezi kulazimishwa kwa nguvu na kubadili katiba under our current political situation ndio ndoto zenyewe hasa, maana utakua unabadili katiba under expense ya CCM na wananchi walioichagua kutawala, siamini kwamba hao walioandika kuhusu Demokrasia ndicho walichosema!

- Nimetoa mfano mdogo sana, eti ili NEC iwe fair itachaguliwa na nani under hiyo katiba mpya ya Chadema?



William.
 
- Mkuu mimi huwa ninaongea facts, sijadili hadithi nenda kwenye clip za mdahalo utaona Mh. Hamad akisema haya maneno na hutaona Mh. Mbowe akikanusha kwamba sio kweli, mimi ninaongelea nilichokiona kwenye mdahalo tu!


William.


Umekuwa muwazi wa kuchanganua kuwa umefuata facts za vyanzo ambavyo Mhe Hamad amenukuliwa, ni kweli Mh Hamad amesema hayo ila ktk upotoshaji wake ambao nimeona sana miongoni mwa viongozi wengi wa TZ huwa wanafanya makosa makubwa sana kwa kupindisha na ku deceive audience kama alivyofanya yeye Mh. kwa kusema kuwa kuna wabunge 10 waligoma kutoka, sasa awataje basi!
 
Mheshimiwa Willima, Heshima sana,
Kwanza napenda kukupongeza kuwa kila mara wewe huleta hoja zinazojadilika na kuzungumzika humu jf. Leo umenichosa na mtazamo wako hasi juu ya suala la mabadiliko ya katiba na hata mfumo mzima wa NEC. Nadhani haya ni matokeo ya kutoshiriki siasa za nyumbani moja kwa moja na kuona matatizo yanayotuzunguka kama taifa.
Wakati huu tusipoziba ufa ujuwe kwa hakika tutajenga ukuta na utakuwa huko ulipo ukitoa ushauri na maoni kwenye mtandao kama unavyofanya leo. Ziko sababu za kutosha za katiba yetu kutazamwa upya kabisa
1. Suala la Muungano: Mfumo wa sasa hauturidhishi watanzania tlio wengi, na Kataba haiko clear kuhusu jambo hili, leo Zanzibar wana Makamu wa rais wawili ambao hawapo katika katiba yetu ya Jamhuri kwa sababu tu ya mfumo wa Zimamoto, Uwiwano wa uongozi na mzigo mkubwa unaobebwa na raslimali za bara kuendesha Zanzibar ni moja ya Changamoto kubwa.
2. Upatikanaji wa tume ya uchaguzi na namna inavyofanya kazi; Uchaguzi huu tume bila aibu inawaambia watanzania matokeo ya kawe na Ubungo yamechelewa kutangazwa kwa sababu ya matatizo ya miundombinu ya usafiri huku ikiwa tayari imetangaza matokeo ya Ngorongoro, Hivi Will huko US ndivyo mnavyofanya kazi kweli? Tume inasubiri watu wapigwe mabomu Mwanza ndiyo itangaze matokeo alafu unaipigia makofi Willy? Uko wapi uwiano wa Demokrasia unaouzungumzi! Alafu hakuna sheria ya kuwawajibisha hawa watu kisha unasema katiba inatosha iko sawa!! Ahaaa mzee think twice hapo, Tumeona katika kampeni hizi wakuu wa wilaya wakisoma taarifa za kazi kwa RizI ili mtoto asiharibu unga kwa baba, nguvu nyingi za serikali zimetumika kwenye kampeni kubeba chama tawala kwa sababu ya ubovu wa katiba, Hakuna mwenye chuki na RZ1 mbona nyie hatukuwaona mkitumia nafasi za wazee wenu ku propage siasa?? Rais ana vyeo vyingi mno vya kuteua watu na hivyo wanalazima kutumika kwa namna yoyote ili walinde nafasi zao alafu unasema hatutaki katiba itakayopunguza nguvu ya Rais, Bunge liliazimia mambo mengi baada ya Saga ya richmond, kwa sababu ya katiba mbovu hayakuenda popote maan na hiari ya Mkulu kuyafanyia kazi au kuyashiti, Hii ni aibu Willy nchi inahitaji katiba kabla kina Kayumba hawajachoka, watauana vibaya watakapochoshwa na mfumo unaoongeza mzigo wa umaskini vichwani mwao na kwa kuwa hutakuwepo utafuatilia kwenye Luninga na mtandao huku ukishaa. Mzee nchi inahitaji katiba iweke mambo sawa.
Mimi sikupiga kura mwaka huu, nina sababu nyingi za hovyo hovyo tu, moja ni kuchoshwa na mfumo mbovu usio na matumaini ya kumkomboa mtanzania, huko US manesi na madaktari ni moja kati ya makundi yanayolipwa vizuri hapa kwetu malipo mazuri yako kwenye siasa (Consumer unawalipa vizuri kuliko wanasayansi producer) Alafu Willy bado hutaki katiba eti tukuwe, hatuwezi kukuwa chini ya mfumo mbovu huu tuliionao ila tutadidimia
Mzee nina mengi lakini ngoja niache tu. nCHI INAHITAJI MABADILIKO YA KATIBA KABLA AKINA KAYUMBA WA MANZESE, BUGARIKA, MABATINI, HAWAJACHOSHWA NA HUU UFUKARA WA KUPINDUKIA
 
- Mkuu mimi huwa ninaongea facts, sijadili hadithi nenda kwenye clip za mdahalo utaona Mh. Hamad akisema haya maneno na hutaona Mh. Mbowe akikanusha kwamba sio kweli, mimi ninaongelea nilichokiona kwenye mdahalo tu!


William.


What facts? hata kitu cha uongo ni facts? know well definition ya facts, hamad ni muongo, wote walitoka waliokuwapo bungeni, na wengine hawakuingia bungeni,
sasa ww una conclude hapo hapo, think... search... ask... if u don't know, then utoe mawazo/ conclusion, na hakuna facts kwa uongo, got it, tumia ubongo kidogo, then write
 
Hahahahah u need brain surgery Muafaka upi unaongelea wewe? ama unaimanisha ndoa iliyoifuta FUC kwenye medani za siasa Tanzania?

mkuu ngoja nikukorect naona hizi ni typing error lakini hamna shida ..umeandika hapo juu FUC ..ila nina uhakika una maanisha CUF, lakini kwa vile herufi zote tatu zipo hakuna shida unaweza hata kuandika CUF,UCF,CUF,FUC,FCU.zote zina maana moja.
 
Wanasiasa kwa kupindisha maneno mahodari sana

Hamad Rashid atasema "nilisema hawakutoka bungeni kwa sababu hawakuingia hasa. Hawawezi kutoka bila kuingia"

Kimsingi Zitto na wenziwe hawakutoka bungeni kwa sababu hawakuingia. Na Zitto mwenyewe amekuja hapa na kuandika kuwa "aliona bora kutokwenda (ingia) bungeni kabisa kwa sababu angekwenda asingetoka".

Na Mbowe labda kwa kujua kuwa ni mtego wa kumfanya azungumzie namna ndani ya chama chake kulivyokuwa na tofauti ya mitazamo kuhusu suala hilo ndio maana akaliwacha lipite tu.

Btw, nini ilikuwa dhamira ya mdahalo ule?
 
- The FACT ni kwamba yote Mh. Hamad aliyosema ambayo sio kweli Mh. Mbowe alijibu, lakini hili hakujibu hiyo ni FACT sihitaji zaidi in that case of the FACT, as a FACT!

William.
let's agree to disagree, Hamad R wanted public opinion in underming CDM, not everything CDM does is correct, but given what it had managed to uncover, I don't buy HR one bit, actually all their previous efforts are in vain for being soothed by muafaka, they now wants to apply Uk politica in Africa, HR is calculating his next post in 2015 actually them forming a unity govt means they will get an in on all CCM inside stuff, if they are to weaken opposn for 2015 he needs to also get an in on the strong opposn, he didn't invite other parties when he formed his opposn kambi the first time, so I agree totally with CDM u don't want to get people in who also bite ur back,WJ Malecela, deal or no deal?
 

Kuna kimoja ambacho tumekisahau ambacho kabla ya kufika kwenye conclusion tunatakiwa kukitilia maanani.

CHADEMA iliiomba CUF ishirikiane nae bungeni. CUF ikakataa kwa sababu vyama vyengine havijashirikishwa.

Sasa tunapofika kwenye conclusion ya kuwa CUF inalazimisha iingizwe kwenye kambi ya upinzani mimi hata sielewi tulifikaje huko.

Suala la msingi ni la kujiuliza kwa nini CHADEMA ilitaka CUF pekee ishirikiane nae? Na ilipoenda kuomba ushirikiano haikujua kuwa CUF imeolewa na CCM na si chama cha upinzani? Kwa sababu hizo facts zipo wazi siku nyingi sana hata kabla matokeo ya uchaguzi kwa Tanzania na Bunge hayajatolewa.

Nionavyo:

CDM wana tatizo la kushindwa kudhibiti misimamo yao. Wanapobadili badili misimamo kila dakika wanachofanya ni kutuchanganya tu wananchi na sio chenginecho.
 
- Nilichosema na ninachosema tena ni kwamba tusikimbikilie kutembea kabla ya kutambaa, maana ukienda Bumbuli naamini utaambiwa CCM sio mchezo, polisi wote wako upande wa ushindi!

William.

Kupita bila kupingwa hakuna maana CCM si mchezo.
Taja jimbo jingine.

Polisi kuwa upande wa ushindi ni jibu lenye uchanga mkuu.
Polisi wanatakiwa kulinda Haki ili Amani iwepo.
Polisi hawafungamani na upande wowote, ni wanasiasa uchwara wenye uroho na roho ya Fisi ndiyo pekee hujaribu kuwaweka polisi nyuma yao.
Polisi kuwa upande wa ushindi ni kwenda kinyume cha Katiba JMT.
 

Haya wee!
 
Mwaka 1865, wakati rais Lincoln anaamua kuwapa haki watu weusi ya kutokuendelea kuwa watumwa, asilimia 70 ya waamerika ilikuwa inapinga,mpaka kusababisha vita kati ya kusini na serikali. Kama Lincoln na wenzake wangekuwa wanafuata maoni ya wengi leo waamerika weusi bado wangekuwa watumwa. Demokrasia ina maana wachache nao wasikilizwe. Kama CCM na mgombea wake anaanguka toka asilimia 80 mpaka 60 na huku zaidi ya watu milioni kumi hawakupiga kura, panaonyesha pana tatizo hapo. Jambo moja mnalosahau, katiba mbovu ya Zambia chini ya Kaunda ilitumiwa na Chiluba kumnyanyasa yeye Kaunda. Madaraka ni kama kumpanda simba, ipo siku atakuangusha na ndipo atakpokukula. Ipo siku CCm wataanguka na hawa wapinzani hawatabadili katiba, watatumia katiba hii hii kuwapa tabu CCM. Hii katiba ni mbovu na inaitaji kubadilishwa, manogopa nini?
 
I bet Bill you are kidding, yaani turudi tena 1990 chini ya chama kimoja, hata huyo Nyerere kama angekuwa anaona ulichoandika angelia. Bila ivi vyama vingi tungejua mambo waliyotufanyia benki kuu na Lowassa na Balali na hao kina Liyumba?
 

Hao wabunge kumi anaosema Hamad Rashid hawakutoka sio kweli anajaribu kupindisha ukweli ambao ni huu hapa; hao wabunge kumi hawakuhudhulia kikao!!
 
Hivi wewe unategemea wabunge 10 wa chadema wabaki bungeni halafu TBC wasioneshe mgawanyiko huo? Hamad Rashid kaumia sana kupoteza malupulupu aliyokua akiyapata kama kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni sasa anaona wivu na anajaribu kuivuruga chadema.
 
Tupeni hayo majina ya wabunge waliogopa kutoka Bungeni ili tuwahujue , mbona hadithi nyingi ?
 

Tupe majina ya hao wabunge waliobaki mjengoni! Halafu sikushangai kumbe bado unasomaga magazeti ya chama?:embarrassed:
 
 
Mbona jamani mmeishaelezwa maana yake!HAWAKUTOKA KWA SABABU HAWAKUWA NDANI WAKATI JK ANATAKA KUHUTUBIA!Ni Kwamba wao waligoma kabisa kuingia,mmojawapo Zitto Kabwe,pengine wao walitaka kuonyesha msimamo wao kwamba HAWAMKUBALI KABISA KABISA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…