Elections 2010 Kumbe kuna wabunge kumi wa chadema hawajatoka Bungeni Rais alipokua akihutubia bunge


Walikuwa wanaogopa kuvunja kiapo walichokula. Kumbuka walikula kiapo kuilinda katiba ya bongo ambayo ndo imemuweka madarakani rais. Na pia kuvunja ahadi ya kuwatumikia wananchi waliowachagua kuingia madarakani. Waliona bora lawama kuliko fedheha.
 
Sikweli asemalo Mtu wa pwani ukweli ni kwamba wabunge 10 hawaku ingia kabisa bungeni siku hio na sio waligoma kutoka bungeni
:hungry:

Kwenye mdahalo kati yake na Mbowe, Hamad alitamka kuwa Wabunge hawakuwalk out hotuba ya Rais. Mbowe hakubisha.
 
Walikuwa wanaogopa kuvunja kiapo walichokula. Kumbuka walikula kiapo kuilinda katiba ya bongo ambayo ndo imemuweka madarakani rais. Na pia kuvunja ahadi ya kuwatumikia wananchi waliowachagua kuingia madarakani. Waliona bora lawama kuliko fedheha.

mbona mwanasheria mkuu ametamka kuwa wabunge wa chadema hawajavunja sheria yoyote kwa kutika nje ya bunge, katiba sheria mama waliogopa kuvunja kifungu gani?
 
- The FACT ni kwamba yote Mh. Hamad aliyosema ambayo sio kweli Mh. Mbowe alijibu, lakini hili hakujibu hiyo ni FACT sihitaji zaidi in that case of the FACT, as a FACT!

William.

Lakini HR nadhani sio mtu makini katika kutoa matamshi... Hadithi aliyoitoa kuhusu mazungumzo yake na Ndesamburo kuwa Chadema ni wakatoliki na CUF waislamu haikupaswa kuongelewa kwenye jukwaa kama lile. Yaani hapo aliharibu pande zote mbili. Ni maneno usiyotegemea kutoka kwa viongozi makini, isipokuwa tu kwa wale wasioweza kuzuia hisia zao.
 

ila huu ni ukweli na hamna haja ya kuuficha ila kwa chadema na ukatoliki nakataa waluteri tumo,walokole wengi sana wakatoliki wapo na waislam wengi sana cdm
 

Usipotoshe maana wabunge wote wa chadema waliokuwa ukumbini walitoka wale ambao hawakukubaliana na hoja ya kutoka hawakuingia kabisa ukumbini. Acheni upotoshaji!
 
“…fighting with a large army under your command is nowise different from fighting with a small one: it is merely a question of instituting signs and signals” …. Sun Tzu art of war
 

Kaka William nadhani Tanzania ya sasa ina watu wachache sana wanaopaswa kupiga kura. Japo kwenye sheria za kupiga kura kuna watu ambao hawaruhusiwi kupiga kura kwa sababu ya umri au "afya ya akili" (kwa ufupi asiwe kichaa) nadhani hizo exclusion criteria hazitoshi. Tuna watanzania wengi ambao akili ya mambo ya siasa na maendeleo hawana kwa kuwa hawakwenda shule na hivyo kuwa na uwezo mdogo wa kujua mambo; na ingekuwa amri yangu nisingewaruhusu kupiga kura. Hata CCM hufanya hivyo kupitia CC. Mtu anapiga kura ya kitu asichojua, hii si haki. Hawa wote hatuhitaji tuwasubiri waelimike mpaka tufikishe asilimia 50%. Hivyo twaweza kuwawakilisha kwa sisi wachache kusikilizwa. Na hiyo theory ya kwamba taifa letu ni changa waitoa wapi mkuu? Kwani Kenya, Zambia na Tanganyika ipi ni taifa changa zaidi?
Lakini ukweli bado unabaki palepale, kwamba hata ikiwa watanzania wengi watahitaji mabadiriko ya katiba na kwa bahati mbaya wakuu wa serikali kutohitaji mabadiriko husika, basi hatutoweza kushinda. Na hizo kura zetu zenyewe nani kahakikisha kwamba zinakuwa hazitoshi? Uchakachuaji tu. Josef Stalin anasema "It's not the people who vote that count. It's the people who count the votes". So it doesn't matter how many people will cast their votes, since they will decide nothing. What matters, is for those people who count the votes (the government) who can decide everything, if they also believe and embrace changes in question.
 
Pengine ni kweli kwamba HR alichokisema hakikuwa sahihi...lakini hoja yake kwa namna nilivyomuelewa ni kuwa, CDM hawawezi kuwalaumu CUF kwamba hawakuwaunga mkono wakati kuna baadhi ya wanaCDM hawaungi mkono pia!
 

Kuna mapungufu makubwa katika hoja yako:
Kama kweli wananchi wameichagua CCM kuendelea kutawala na una imani kuwa hata 2015 wataendela kuichagua, basi wataendelea kuichagua hata kama katiba itarekebishwa - sasa woga wa kubadili katiba wa nini? Kama unafikiri kubadili katiba itakuwa expense kwa CCM then ujue kuwa katiba purposely inawa-favour wao na katiba ya namna hiyo si ya haki. Kama unasimamia ukweli basi katiba hiyo unapaswa kuipinga.
Ili NEC iwe huru, bado mwenyekiti anaweza kuteuliwa na rais lakini kuwepo n vigezo vilivyoainishwa mapema. Na akishateuliwe kuwepo na chombo tofauti kama bunge kinachoweza kumjadili ili kupima neutrality yake. Halafu wajumbe wa tume watoke kwa wadau mbalimbali - vyama vya siasa, NGOs, dini/madhehebu mbalimbali nk wote wawakilishwe. Na uwakilishi huu uende down hadi ngazi ya jimbo. Kama kweli CCM inashinda kihalali kabisa basi itaendela kushinda hata ukiwepo uwazi wa aina hii maana uwazi huu hauondoi imani ya watu kwa CCM - woga wa nini?
Mbowe kasema hali inaweza kuwa mbaya zaidi 2015 endapo katiba haitarekebishwa - ni kweli - kwa nini kuendelea kuwepo kwa hofu, si ushirikishwaji wa kutosha uwepo ili hofu zipungue?. Mimi kama najiamini kuwa nashinda kihalali basi hata ukimleta refa toka wapi nitashinda, lakini kama naendelea kung'ang'ania refa na linesmen wawe wangu ndipo nishinde, niwazi ushindi huo utakuwa na kasoro.
Hivi kweli W.J.Malecela unaamini kwa dhati kabisa kuwa ni haki kwa rais kumteua mwenyekiti wa NEC na hakuna wa kuhoji uteuzi huo, na mwenyekiti huyo huyo akimtangaza huyo aliyemteua kuwa ndiye kashinda urais hakuna wa kuhoji?
Je katika suala la mihimili mitatu, Rais kwa kofia ya mwenyekiti wa CCM anamteua fulani kuwa kiongozi wa mhimili wa bunge (spika) - wale wengine wawili walikuwa geresha tu, na pia kwa kofia ya urais anamteua kiongozi wa mhimili wa mahakama - jaji mkuu, je unaamini kwa dhati kabisa kuwa wiongozi wa mihimili hii miwili hawatakuwa chini ya aliyewateua?
Kuendelea kuwa na katiba mbaya ari mradi walio madarakani katiba hiyo inawasaidia kuendelea kuwepo madarakani ni jambo la hatari. Akija penya dikteta mmoja hakika atatumia katiba hiyo hiyo kutuumiza sote. Unakumbuka suala la Balali - kwamba mengi aliyofanya sheria za fedha zilimruhusu kufanya hivyo na katumia sheria hizo hizo kufisadi fedha nyingi sana. Je akitokea mtu kama huyo ngazi ya urais si itakuwa hatari?
TAHADHALI KABLA YA HATARI!
 
Unaongelea ulichokiona kwenye mdahalo ,hata ungeona matusi ungeyaleta hapa!?kwa hiyo ulitaka mbowe ajibu hata upuuzi!?
 

Tatizo ni kuwa media ikiwa upande mmoja nasi hauwezi kuwabalance media ikiamua kushabikia chama au mtu ujue ukweli wa upande wa pili hutaupata kwani mmesahau sakata la CCJ kwenye vyombo vya habari ilivyokuwa ina draw intentions za watu. Mie nilikuwa nakiona CCJ kama chama kikubwa sana kwa jinsi kilivyokuwa kinaripotiwa lakini hata leo hii ukimuuliza yule jamaa aliekimbia kutoka CCM kwenda CCJ na baadae CDM hajui ukubwa wa CCJ.
 
- The FACT ni kwamba yote Mh. Hamad aliyosema ambayo sio kweli Mh. Mbowe alijibu, lakini hili hakujibu hiyo ni FACT sihitaji zaidi in that case of the FACT, as a FACT!

William.

Willy, Hamad Rashid ndo source ya kuaminika? Why not CCM ambao kama Wachadema hao wasingetoka reaction isingekuwa zile walizozitoa kina Chiligati na Makamba, lazima wangezigusia tena hata JK aliyekuwa anatoa hotuba siku ile asingehamanika vile. Naamini Hamada Rashid ana agenda yake katika taarifa hiyo na kama si hiyo basi kauli yake mliyoinukuu kutoka kwenye mdahahalo mmeitafsiri vinginevyo.

Kwa mwenye ushabiki wa vyama hii ni habari ya kuaminika, lakini kwa mchambuzi wa mambo kauli hiyo ina malengo. Hata hivyo tujiulize, mbona nafasi rasmi ya Upinzani ilibaki wazi? Tena mbona CUF walikwenda kuikalia? Kama wangebaki Wabunge wa CHADEMA 10, CUF wasingeenda kuchukua nafasi ya upinzani, wangeendelea kuwepo walipokuwa wakati JK akihutubia.
 
 
Kuna watu wanajifanya wagumu kuelewa, wanajifanya kuwa Hamad ndo siku zote yupo sahihi. Ila juzi tuu walikuwa wanaita CUF chama cha kidini.
 
Hamad amegeuka kuwa mtu mwongo na mlaghai hasa kwa watu wenye uelewa mdogo kama hao waliolipokea hili kama ndiyo ukweli wenyewe. HAMAD KUSEMA KWAMBA WABUNGE 10 WA CHADEMA HAWAKUTOKA WAKATI WENZAO WALIPOTOKA, ALITOA KAULI HIYO MAKUSUDI AKIJUA KUTAKUWA NA WATU WENYE AKILI NYEMBAMBA AMBAO WATAONA AMEWALETEA HABARI MPYA. UKWELI NI KUWA HAMAD KUITOA HABARI HIYO NI UJINGA NA ULAGHAI WA HALI YA JUU KWA VILE WABUNGE HAO 10 AMBAO ANASEMA HAWAKUTOKA, WASINGEWEZA KUTOKA WAKATI HAWAKUINGIA UKUMBINI. Ametoa kauli hiyo makusudi kwa nia ya kupotosha watu wenye upeo mdogo kama hawa walioileta hii hapa wakiamini kauli aliyoitoa Hamad ilikuwa kama walivyoelewa wao.

Anayekupinga anaweza kuwa ni adui yako lakini mtu anayetumia hila na uwongo kuwadanganya watu ili tu kutaka kukubalika ni hatari sana. Tunashukuru sana kwa CUF kukosa uongozi wa kambi ya upinzani kwa sababu tumeweza kumwelewa vizuri Hamad, huyu ni hatari katika mabadiliko tunayoyataka kuliko CCM.
 
dont discuss foolish propagandas! thats all!
 

Hamad Rashid ni kama alikuwa akifanya jitihada kuwa Chadema ionekane ni Chama cha watu fulani tu. Tena akajaribu kuwagawa wakristo vipandevipande kwa kusema kuwa alimwambia Ndesa kuwa Chadema ni chama cha wakatoliki.
Ni jealous fulani hivi kwani CUF wanaona Chadema imechukua nafasi yao, hivyo wanatafuta jinsi ya kui-discredit Chadema.

Chadema ni chama cha watu wote wanaotaka mabadiliko, bila kujali jinsia, kabila, dini, rangi, wala chama (yes, wala uanachama wa Chama).

Amejiita kuwa ni kiongozi mkongwe, lakini alikuwa mwepesi kukimbilia kwenye issue za udini, akijifanya anaukemea, kumbe anatumia style ya Kikwete kuufanya ndio mjadala.
Viongozi wanaojaribu kutupeleka kwenye udini hawafai.

Je ni bora niwe na kiongozi wa dini yangu (jambo ambalo halinisadii chochote) mwenye sera za ukandamizi? (mfano Elimu na Afya vitalipiwa na wananchi moja kwa moja) au niwe na kiongozi ambaye ni tofauti na mimi kwa dioni, kabila, chama, rangi au jinsia ambaye atakuwa na sera zinazonufaisha wananchi wengi? (mfano wananchi hawatalipa kupata huduma za Elimu na Afya)
Bora nimchague huyu wa pili, awe dini za jadi au baniani.
 
Duu. mengine tutajadili madudu. Mbona hakuwataja. Ukijadili ya zuzu nawe utakuwa zuzu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…