Wakuu, recently nilisikia Mkulu akijisifu kuwa Baharia ambaye ni PhD holder akila 500,000 kwa mwezi na kwamba huyu Daktari alikua "vere komfotabo"!
Kwa sasa kwa Tz gharama za Masters si chini ya million tatu na PhD si chini ya 10m, sasa kama unafanya investment ya more than 15m pamoja na miaka uliyosoma yote kisha unalipwa laki tano na uko poa tu Basi either wewe ni tatizo au hio PhD yako ni ya kubumba.
Soma ili uweze kujitegemea na uweze kuwasaidia na wengine, kwa laki tano kamwe narudia kamwe utakua umeharibu muda wako na kuwapotezea wengine hizo bahati za kusoma na kuw productive, huwezi kuwa productive kwa salary ya laki tano.
Watu kama hawa unakuta hawawezi kuandika hata two pages Concept Note, narudia either yeye au hio degree yake ina matatizo.
Shukrani