Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Passo Ni cc 900 na sio 1290
Yes hii ndo Passo ya piston 4
Gharama kubwa kwenye gari ni maintanace! Service za kawaida haziumizi sana pesaKwahiyo gharama za gari ni mafuta tu? Mwaka mzima wa kumiliki passo nilijua ushamba ushakutoka kumbe bado [emoji1][emoji1]
Kuna mahali niliona mtu kaandika kuwa passo yenye piston 4 (cc 1290) ina injini ya 2kr, sijui kama ni kweli1KR ya Cc izo haipo...
Labda kama ni 2NZ au 2SZ...
Hyo ni passo racy ina cc 1290, usikatae passo zipo za aina mbiliPasso Ni cc 900 na sio 1290
Umemaliza mjadala
Ni kweli kabisa mkuuGharama kubwa kwenye gari ni maintanace! Service za kawaida haziumizi sana pesa
Unaweza kupunguza matengenezo mengi kwa kuwa makini na uendeshaji wako , kuna wanaotumia magari kwa miaka mingi na hisikii kama kabadilisha ball joints au bush yoyote ,
Kuna mahali niliona mtu kaandika kuwa passo yenye piston 4 (cc 1290) ina injini ya 2kr, sijui kama ni kweli
Kipimo cha maendeleo ni kulala nyumba za nyasi Mkuu ...Maendeleo ya watu au Nchi ni wananchi wake kutumia vitu bora ambavyo vinawarahisishia utendaji kazi na wanakula lishe bora na pia hawaumizi kichwa saana kupata mahitaji muhimu...gari ni kama simu tuu ni vile tumechelewa ndio maana tumeweka kwenye kundi la starehe..Nchi za wenzetu gari ni part and parcel ya basic needs, yani kununua gari hakumpi mtu stress kama sisi huku.
Wabongo tunanunua gari sababu ya ufahari tuu.
Na kwa umbumbumbu wetu wabongo tukiona mtu kanunua gari basi ndo tunafanya kama kipimo cha maendeleo kumbe sio kweli.
Hio ni passo Racy ndio ina cc hizo sawa tu na Vits RSPasso zipo mpaka cc 1495
Engine za 2KR zipo Yamaha 250 ina 2KR engine hata engine za boat zipo pia...Hakuna engine inaitwa 2kr....
Hii toy itakuwa ni 4wd maana inakula sana wese.Umetimia mwaka sasa tangu ninunue gari yangu hii ya kwanza. Babywoka safi inanitosha, 1290cc engine 1KR.
Tangu ninunue hii babywoka nilikua sijawahi kukaa na kufanya 'cost-analysis' upande wa mafuta nayotumia.
Zaidi nilikua nahisi kama gari 'inanifilisi' vile navokua natoa 20,000 au 30,000 kwa mkupuo napoingia "sheli".
October 2, 2021 Jmosi saa mbili usiku niliweka mafuta ya 50,000.
Sio kawaida yangu maana hata jamaa wa pale Petrol Station (GUDAL) napo-endaga kuweka alinitania "naona leo umeamua kaka..."
Kabla ya kuweka nilisoma ODOMETER nikaweka record kwenye 'sticky note' ya simu.
Basi nikaendelea na mizunguko yangu weeee... Mwenge, Sinza, Kariakoo mara chache, Mbagala Chamazi, Bunju kidogo, Bahari beach kule nakadhalika.
By the way, kwa sasa nakaa pande za Makongo. Office location ipo pale Shekilango Ubungo Business Park (kule ndan kwenye ma-godown yale). So you can imagine my daily routes.
October 25 2021, Jtatu saa mbili usiku 'gauge' ya mafuta ikarudi ilipokua tarehe 2. Nikachukua kalamu na karatasi.
Katikati hapo nilishaongeza mafuta ya 15,000 halafu 20,000. Sio kwamba yalikua yameisha. Nilipata safari ambazo hazikuwa kwenye 'monitoring process'.
Kwahiyo basi;
Mafuta nilinunua jumla 85,000/=
Bei kwa lita: 2,427/=
Jumla lita: 35 ltrs
No. of days: 23 days
Total distance covered: 344 km
Average Consumption:
Distance covered per litre: 344 km ÷ 35 litres = 9.8km/ltr.
Cost per day: 85,000 ÷ 23 days = 3,700/= per day.
Tuseme roughly kwa siku natumia shilingi 4,000 kama gharama za mafuta (asante babywoka yangu).
Hii ni almost sawa na ningekua natumia bodaboda (kwenda 2,000 kurudi 2,000). Na hapo nime-assume ni strictly route ya maskani-ofisini-maskani.
Kumbe hamna tofauti kiviiile.
Tena naona afadhali kwangu, maana naweza kwenda popote, muda wowote.
Naweza kumpa mtu/watu lift. Sinyeshewi mvua. Sipigwi jua.
Hata demu wangu nahisi nilimpata sababu ya hii babywoka. Japokua amenipiga kibuti.
View attachment 1987573
Ame upgrade her status, ameachana na mwenye Sedan, amempata mwenye Van, kitambo kidogo atakutana na mwenye station wagon etc....Hata demu wangu nahisi nilimpata sababu ya hii babywoka. Japokua amenipiga kibuti.