Kumbe mafuta nayotumia kwenye gari ni sawa na ningekua napanda bodaboda!!

Kumbe mafuta nayotumia kwenye gari ni sawa na ningekua napanda bodaboda!!

IMG_1759.jpg

sifa ya huyu mnyama wish new model .

ina button mbili ambazo ni Eco na sport ,ukiondoa hizo buttom inabaki kama wish yenye kwenye sifa zake.

Button ya Eco
hii unaweza kuwa kama carina TI yani mafuta elfu kumi unatembea na safari fupi.

Sport
hii wala wanaofahamu mlio subari na nduki za ali kateleza(altezza) ila wese hapa utakimbia maana inafumua advance turbo na cc inakuwa na uwezo mkubwa.

kapo kanukula maji [emoji97][emoji97]

kwa mwezi eco button na tumia elfu 60000
 
Kuna mahali niliona mtu kaandika kuwa passo yenye piston 4 (cc 1290) ina injini ya 2kr, sijui kama ni kweli
Hamna engine ya 2KR mzee! Engine za 4 cylinder za Toyota unazoona common barabarani ni hizi hapa!

1KR 990cc (Passo, Vits)

2SZ 1290cc (Funcargo,Passo, Vits)

2NZ 1290cc(Ist, Vits,Porte)

1NZ
1490cc(Spacio,Ist,Raum,Rush,Vits,Runx,Rumion,Premio, Allion)

1ZZ 1794cc (Spacio, Wish,Isis,Opa,Vista,Rumion)

1AZ 1990cc(Opa,Noah mayai,Premio)

3S 1998cc( Noah dume/old, Altezza)

2AZ 2394cc (Harrier, Kluger, Vanguard)

Six Cylinder engines:
1G 1998cc (Mark 2, Chaser,Cresta,Altezza, Verossa)

1JZ 2490cc (Mark 2, Chaser,Cresta, Altezza,Progress, Brevis, Crown 90 series)

2JZ 2990cc(Altezza Gita,Brevis)

4GR 2490cc (Mark X, Crown GRS,Lexus IS250)

3GR 2990cc (Mark X,Crown GRS)
 
View attachment 1989252

sifa ya huyu mnyama wish new model .

ina button mbili ambazo ni Eco na sport ,ukiondoa hizo buttom inabaki kama wish yenye kwenye sifa zake.

Button ya Eco
hii unaweza kuwa kama carina TI yani mafuta elfu kumi unatembea na safari fupi.

Sport
hii wala wanaofahamu mlio subari na nduki za ali kateleza(altezza) ila wese hapa utakimbia maana inafumua advance turbo na cc inakuwa na uwezo mkubwa.

kapo kanukula maji [emoji97][emoji97]

kwa mwezi eco button na tumia elfu 60000
Hii gari naihusudu sana! Ina ValveMatic system ambayo inacontrol ulaji wa mafuta ni new tech after VVT-i
 
Nchi za wenzetu gari ni part and parcel ya basic needs, yani kununua gari hakumpi mtu stress kama sisi huku.

Wabongo tunanunua gari sababu ya ufahari tuu.

Na kwa umbumbumbu wetu wabongo tukiona mtu kanunua gari basi ndo tunafanya kama kipimo cha maendeleo kumbe sio kweli.
Umenena vyemaa cheif

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 
Hamna engine ya 2KR mzee! Engine za 4 cylinder za Toyota unazoona common barabarani ni hizi hapa!

1KR 990cc (Passo, Vits)

2SZ 1290cc (Funcargo,Passo, Vits)

2NZ 1290cc(Ist, Vits,Porte)

1NZ
1490cc(Spacio,Ist,Raum,Rush,Vits,Runx,Rumion,Premio, Allion)

1ZZ 1794cc (Spacio, Wish,Isis,Opa,Vista,Rumion)

1AZ 1990cc(Opa,Noah mayai,Premio)

3S 1998cc( Noah dume/old, Altezza)

2AZ 2394cc (Harrier, Kluger, Vanguard)

Six Cylinder engines:
1G 1998cc (Mark 2, Chaser,Cresta,Altezza, Verossa)

1JZ 2490cc (Mark 2, Chaser,Cresta, Altezza,Progress, Brevis, Crown 90 series)

2JZ 2990cc(Altezza Gita,Brevis)

4GR 2490cc (Mark X, Crown GRS,Lexus IS250)

3GR 2990cc (Mark X,Crown GRS)
Kuna mdau hapo juu kasema passo yenye piston 4 injini yake ni K3, ni kweli maana hamna passo yenye 2nz ila vitz ziopo za kutosha tu
 
View attachment 1989252

sifa ya huyu mnyama wish new model .

ina button mbili ambazo ni Eco na sport ,ukiondoa hizo buttom inabaki kama wish yenye kwenye sifa zake.

Button ya Eco
hii unaweza kuwa kama carina TI yani mafuta elfu kumi unatembea na safari fupi.

Sport
hii wala wanaofahamu mlio subari na nduki za ali kateleza(altezza) ila wese hapa utakimbia maana inafumua advance turbo na cc inakuwa na uwezo mkubwa.

kapo kanukula maji [emoji97][emoji97]

kwa mwezi eco button na tumia elfu 60000
Iv wish old yenye 1zz na carina ti 5A ipi inatumia mafuta kidogo zaidi?

Maana ninavyoelewa injini ya VVT- I yenye cc 1790 inatumia mafuta kidogo zaidi ya injini za kizaman yenye cc 1490 kama vile 5A n.k..

Wataalam hapo mnasemaje?
 
Umetimia mwaka sasa tangu ninunue gari yangu hii ya kwanza. Babywoka safi inanitosha, 1290cc engine 1KR.

Tangu ninunue hii babywoka nilikua sijawahi kukaa na kufanya 'cost-analysis' upande wa mafuta nayotumia.

Zaidi nilikua nahisi kama gari 'inanifilisi' vile navokua natoa 20,000 au 30,000 kwa mkupuo napoingia "sheli".

October 2, 2021 Jmosi saa mbili usiku niliweka mafuta ya 50,000.

Sio kawaida yangu maana hata jamaa wa pale Petrol Station (GUDAL) napo-endaga kuweka alinitania "naona leo umeamua kaka..."

Kabla ya kuweka nilisoma ODOMETER nikaweka record kwenye 'sticky note' ya simu.

Basi nikaendelea na mizunguko yangu weeee... Mwenge, Sinza, Kariakoo mara chache, Mbagala Chamazi, Bunju kidogo, Bahari beach kule nakadhalika.

By the way, kwa sasa nakaa pande za Makongo. Office location ipo pale Shekilango Ubungo Business Park (kule ndan kwenye ma-godown yale). So you can imagine my daily routes.

October 25 2021, Jtatu saa mbili usiku 'gauge' ya mafuta ikarudi ilipokua tarehe 2. Nikachukua kalamu na karatasi.

Katikati hapo nilishaongeza mafuta ya 15,000 halafu 20,000. Sio kwamba yalikua yameisha. Nilipata safari ambazo hazikuwa kwenye 'monitoring process'.

Kwahiyo basi;

Mafuta nilinunua jumla 85,000/=
Bei kwa lita: 2,427/=
Jumla lita: 35 ltrs
No. of days: 23 days
Total distance covered: 344 km

Average Consumption:
Distance covered per litre: 344 km ÷ 35 litres = 9.8km/ltr.

Cost per day: 85,000 ÷ 23 days = 3,700/= per day.

Tuseme roughly kwa siku natumia shilingi 4,000 kama gharama za mafuta (asante babywoka yangu).

Hii ni almost sawa na ningekua natumia bodaboda (kwenda 2,000 kurudi 2,000). Na hapo nime-assume ni strictly route ya maskani-ofisini-maskani.

Kumbe hamna tofauti kiviiile.
Tena naona afadhali kwangu, maana naweza kwenda popote, muda wowote.
Naweza kumpa mtu/watu lift. Sinyeshewi mvua. Sipigwi jua.

Hata demu wangu nahisi nilimpata sababu ya hii babywoka. Japokua amenipiga kibuti.

View attachment 1987573
Unafanyia Sundar
 
Wakuu nimewasoma.

Kumbe bado ulaji wa mafuta uko juu sana kwa hii gari?

Kwahiyo angalau ilitakiwa ningetumia wese la kiasi gani kwa mwezi kwa mizunguko hiyo nilofanya
Kwa cc1290 zen unapata km 9.8 duh..inakula aisee. Hpo kuna vitu viwili

Inawwzekana kari haipo sawa kwenye mfumo au

Uendeshaji wako sio mzuri.

Kwa injin ya cc1290 kikawaida kwa mjini hapa unatakiwa kupata sio chini ya 12km/L.
 
Suala la kuchek mfumo nitafuatilia.

Labda kwenye suala la uendeshaji. Natakiwa niwe nazingatia nini kwenye kuendesha nisichome mafuta sana.

Niwe nakimbiza au naendesha taratibu.

Kuna mshikaji nikipandaga lift kwenye Harrier yake anakimbizaga hata kama umbali mfupi. Niwe nafanya hivo?
 
Hakikisha kwenye uendeshaji wako rpm iwe chini ya mbili acha gari ivhanganye yenyewe usiilazimishe kama huna haraka sana.

Speed nzuri inayotumia mafuta kidogo ni 50,60 hadi 70 labda kidogo 80 km/h
 
View attachment 1989252

sifa ya huyu mnyama wish new model .

ina button mbili ambazo ni Eco na sport ,ukiondoa hizo buttom inabaki kama wish yenye kwenye sifa zake.

Button ya Eco
hii unaweza kuwa kama carina TI yani mafuta elfu kumi unatembea na safari fupi.

Sport
hii wala wanaofahamu mlio subari na nduki za ali kateleza(altezza) ila wese hapa utakimbia maana inafumua advance turbo na cc inakuwa na uwezo mkubwa.

kapo kanukula maji [emoji97][emoji97]

kwa mwezi eco button na tumia elfu 60000
M8 si unaiachia mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameanza na mbwembwe kibao sijui babywoka wewe mkuu sema tu hiyo passo yako na bado haipo clear maana huo ulali ni mkubwa sana kwahyo unajisifia maumivuuu tuuu mkuu na sio ulajo Mzuri wa mafuta pia hakuna 1KR yenye hizo cc mkuu kwa hilo umefeli kiongoz uliza uelekezwe boss kujua kwingi mbele giza #mzeewababywoka [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
stoplight
 
Leo nimechungulia kwenye Bonet engine wameandika K3 - VE.
Lakin kwenye card ya gari wameandika 1NZ.
Hizo gharama ulizopiga ina maana unafanya kazi siku zote za mwezi hamna siku umepumzika?

Hakuna siku umekaa foleni engine ikiwa inanguruma?

Hufanyi service? Huoshi gari? Hujazi hata upepo? Hulipii parking? Tozo za madaraja?

Hizo zote ni gharama za kumiliki gari.
 
Back
Top Bottom