Kumbe Menejimenti Team yote ya BAWACHA wamepata Ubunge wa Viti Maalumu

Kumbe Menejimenti Team yote ya BAWACHA wamepata Ubunge wa Viti Maalumu

Bawacha wapuuzi sana.. yani wamejichagua wenyewe.. wangewapa wanawake ambao hawajawahi kuwa wabunge wangekuwa wamefanya jambo la maana sana! Hicho walichofanya kinadhirihisha njaa na ubinafsi walionao!
 
Na hiki ni chama cha DEMOKRASIA.....
Lakini binadamu wote ni wabinafsi by nature especially pale linapokuja suala la maslahi manono
Chadema ilikuwepo kabla ya hao wanawake kuwepo...wafukuzwe tu...wapenda demokrasia watachangia chama
 
Nilidhani yale majina ya Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA yalizingatia uwakilishi kama wafanyavyo UWT ya CCM.

Kumbe hawa CHADEMA wamepeleka majina ya viongozi watupu ukiwemo uongozi wote wa BAWACHA yaani Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Mkuu, Mtunza Hazina nk.

Ni kama vile BAWACHA imehamia Bungeni.

Hongereni akina Mama wa CHADEMA kwa kujipendelea.

Maendeleo hayana vyama!
Bawacha wameamua kuasi
 
Unawaza upumbavu, utupe nchi we kama nani? Nchi ya babu yako hii? Kama unamiliki hii nchi tufukuzeni basi.
Hahaha imebidi ni cheke.
Narudia tena chadema imekufa toka tarehe 27/10/2020.
Sasa endelea kuona nawaza upumbavu.
 
Hahaha imebidi ni cheke.
Narudia tena chadema imekufa toka tarehe 27/10/2020.
Sasa endelea kuona nawaza upumbavu.
Babu yenu katumia kila mbinu lkn bado hajafanikiwa na hatafanikiwa kuiua chadema, muda si mrefu chama chake kitakuja kuomba maridhiano, ni suala la muda subiri utakuja kuona!
 
Ccm mnahaha ka nyau anayetaka kuzaa si msubiri hiyo kesho kilakitu kitakuwa wazi yaani thread za chadema zimejaa humu ka chawa hadi tunachoka sasa kuweni wavumilivu msubiri hiyo kesho
 
Babu yenu katumia kila mbinu lkn bado hajafanikiwa na hatafanikiwa kuiua chadema, muda si mrefu chama chake kitakuja kuomba maridhiano, ni suala la muda subiri utakuja kuona!
Kwambali naona umeanza kutoka kwenye muhemko na akili zimeanza kurudi.
Endelea na dua la kuku..
 
He wanawake Hawa wote kwa pamoja wametongozwa na polepole? Na wakamkubalia dah .wanaume wako vizuri kwa kutongoza
 
Unavyodai ya kwamba CHADEMA wamepeleka majina ya viongozi watupu ukiwemo uongozi wote wa BAWACHA, je kuna kikao cha kamati kuu ya chama kilifanyika ili kuidhinisha na kupitisha majina hayo?
Kwenye mazingira ambapo yawezekana katibu anagoma kuitisha kikao cha kamati kuu ya chama kwa ajili ya kutoa maamuzi muhimu, katiba ya Chadema aielekezi mamlaka hayo yakasimwe kwa nani!? Kumbuka katiba inasema mamlaka ya kamati kuu yanaweza kukasimiwa na sekretarieti ya kamati kuu. Mwenyekiti wa sekretariate hii ni Katibu Mkuu wa chadema. Rejea katiba ya Chadema ya mwaka 2006( ukrasa wa 77 na 67).
Hata hivyo, Katiba ya Chadema iliyoboreshwa mwaka 2006, Ukurasa wa 65 unatoa maelezo kwenye kipengele cha 7.7.16 kazi za kamati kuu ya chadema kitaifa. Kipegele hiki katika mafungu yake ya

1. 'y' kiko wazi na kusema kuwa Kazi ya kamati kuu itakuwa ni" kufanya uteuzi wa mwisho wa madiwani wa viti maalumu kutokana na mapendekezo ya Balaza la Wanawake Taifa"
2. 'v' kuandaa hoja za kupelekwa bungeni na wabunge wa chadema.

Ukurasa wa 70 wa katiba ya chadema unaeleza mabaraza ya chadema likiwemo na BAWACHA. Mabaraza yamepewa mamlaka ya kujitengenezea taratibu za kujiendesha na ni baraza kuu la chama litaidhinisha taratibu hizo.
=====
Nimepitia katiba ya chadema kwa haraka na nimetoa kwa ufupi kazi za kamati kuu kuhusu wabunge wa viti maalumu kwa lengo la kuonyesha kuwa Kamati kuu ya Chadema haihusiki na kuteua wabunge wa viti maalumu kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ya 2006. Labda kama imefanyiwa marekebisho hivi karibuni na mimi marekebisho hayo sijayapata. Kwa hiyo kunauwezekanao Katibu mkuu (Mnyika) anajificha kwenye kichaka cha kamati kuu kuficha aibu yake.

Pengine hiyo kesho, Kamati kuu ya chdema yaweza kuwa imewaita wabunge wa viti maalumu ili wakapewe hoja za kupelekwa Bungeni kwa mujibu wa katiba ya Chadema ya 2006 kipengele cha 7.7.16(v).

Yangu ni hayo nakaribisha kukosolewa.
 
Back
Top Bottom