Kumbe Menejimenti Team yote ya BAWACHA wamepata Ubunge wa Viti Maalumu

Kumbe Menejimenti Team yote ya BAWACHA wamepata Ubunge wa Viti Maalumu

CDM ni genge la wajanjawajanja wanaotafuta ugali. Upinzani nchi hii bado, watu wana njaa sana.
Njaa ni nini? Wabunge wa viti maalumu wamechaguliwa kuwa kwenye nafasi ambazo zipo kikatiba, na wakilipwa mishahara, ni haki yao kwa kazi wanazofanya! Na wakati ukitumia viti maalumu CHADEMA kuuponda upinzani, kumbuka ccm wa viti maalumu 94 vilivyopatikana kupitia ’uchafuzi’ huu huu! Hapo hatujaongelea urais, ubunge na udiwani, ambapo palipigwa vibaya, haikua njaa hiyo?!
 
Unavyodai ya kwamba CHADEMA wamepeleka majina ya viongozi watupu ukiwemo uongozi wote wa BAWACHA, je kuna kikao cha kamati kuu ya chama kilifanyika ili kuidhinisha na kupitisha majina hayo?
Huijui michezo hii; Mbowe katulia tuliii, Mwalimu anacheka, mnyika anafula. Muulizeni Mwalimu aliyegonga muhuli nani, anajua!
 
Bora kwa hao wameenda kwa kigezo cha nyadhifa kwenye Chama chao, wale waliokuwa wanaenda kwa kuchunguliwa na Mwenyekiti kwanza
Nilidhani yale majina ya Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA yalizingatia uwakilishi kama wafanyavyo UWT ya CCM.

Kumbe hawa CHADEMA wamepeleka majina ya viongozi watupu ukiwemo uongozi wote wa BAWACHA yaani Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Mkuu, Mtunza Hazina nk.

Ni kama vile BAWACHA imehamia Bungeni.

Hongereni akina Mama wa CHADEMA kwa kujipendelea.

Maendeleo hayana vyama!
 
Huijui michezo hii; Mbowe katulia tuliii, Mwalimu anacheka, mnyika anafula. Muulizeni Mwalimu aliyegonga muhuli nani, anajua!
Mbowe na Mwalimu wameivusha Chadema.

Bila hawa wabunge 19 mishahara ya akina Mnyika itatoka wapi?!!
 
Najaribu kuwaza... Inamaana Ndugai achague viongozi wote na hao viongozi wakubali kuchaguliwa tena bila uongozi wao kujua.

Hii ni dalili kuwa hata tungewapa nchi bado tungeongozwa na Mabeberu bila hata wao wenyewe kujua
Unawaza upumbavu, utupe nchi we kama nani? Nchi ya babu yako hii? Kama unamiliki hii nchi tufukuzeni basi.
 
98% ya wanasiasa wote ni njaa tu imewafanya kuwa wanasiasa.
 
Unadhani ili lengo la dola la kuimaliza chadema litimie (wajinga wanavyodhan) wangefanyaje?
 
Hao wabunge haijachagua CHADEMA, hao ni wabunge wa Ndugai
Wawe wa ndugai
Wawe wa magufuli
Wawe wa mbowe
Haina maana yoyote.

Cha muhimu ni kwamba watanzania mnapaswa kujitambua na mjitambue kweli kweli. Mkiendelea kuwataka wanasiasa wateseke kwa ajili yenu huku nyie mpo zenu busy mnakula bata, mtapata taabu sana.
 
Naunga hoja mkuu, binafsi yalipoitishwa maandamano ya kupinga uchafuzi mkuu, nilijikuta nipo road peke yangu, kuanzia sasaiv natarajia kujiunga ccm nikasake fursa za kuitafuna nchi kadiri niwezavyo!!
 
Unavyodai ya kwamba CHADEMA wamepeleka majina ya viongozi watupu ukiwemo uongozi wote wa BAWACHA, je kuna kikao cha kamati kuu ya chama kilifanyika ili kuidhinisha na kupitisha majina hayo?
Sisi hayo hayatuhusu.
Kilichopo hao akina mama, wako bungeni, full stop.
 
Back
Top Bottom