Uchaguzi 2020 Kumbe Mheshimiwa Membe ni laghai wa kisiasa!

Hii movie ya Bernard Membe na wakili Mwesiga Zaidi, wanachama waliohamia juzi mwezi August 2020 ACT-Wazalendo kuwa na uchungu kupita wanachama walioanzisha chama hiki cha kikuu cha upinzani kinaleta maswali mengi yenye majibu kuwa wana agenda ya kudhofisha upinzani kutokea ndani ya chama (ACT-Wazalendo) walichojiunga nacho.
 
4 Julai 2020

MNYIKA AMESHA JIFIA HIVYO NATIA NIA KIBAMBA SIO KWA AJIRI YA MNYIKA : MWESIGWA ZAIDI

Tarehe 4 ya mwezi Julai mwaka huu 2020, Mwesiga Zaidi alipotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia chama cha Mapinduzi CCM akitamani sana apambane na John John Mnyika wa CHADEMA kama mbunge huyo aliyemaliza muda wake atasimama tena kuwania jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania.

Hapa kada na mwanachama wa CCM wakili Mwesiga Zaidi alikuwa anatangaza nia yake baada ya kuchukua fomu Julai 4 2020 akisubiri mchujo ndani ya CCM atakapo omba ridhaa za wajumbe wa mkutano Mkuu wa Jimbo la CCM Kibamba Dar es Salaam.
 
15 September 2020
Picha kali la Movie ya Membe, Dubai to Dar es Salaam Airport : scene / location : Julius Nyerere International Airport : Plot - Mgombea anatisha 2020

................................ ............................
17 September 2020
Dar es Salaam, Tanzania

SAKATA LA KUTEKWA KWA MSAIDIZI WA MEMBE, KAMANDA MAMBOSASA ATOA TAMKO...

on 17 Sep 2020
SAKATA LA KUTEKWA KWA MSAIDIZI WA MEMBE, KAMANDA MAMBOSASA ATOA TAMKO... KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, leo Septemba 17, 2020, amesema msaidizi wa mgomba urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe, aitwaye Jerome Luanda, yuko mikononi mwa polisi akiwa ni mzima wa afya na hakutekwa.

Amesema hayo akiwa anazungumza na East African Radio ya jijini Dar es Saalam, ambapo amethibitisha msaidizi huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na akakanusha habari za kutekwa.

“Huo ni uongo na uzushi; tumemkamata akiwa airport pale Julius Nyerere, nasikia wengine wanasema wamemtafuta vituo vyote hawajamuona.

Ni uongo, sisi tupo naye na ni mzima wa afya, tunamshikilia kutokana na kesi zake ambazo hatuwezi kuzitaja,” amesema na kuongeza: “Na huyu nasema amekamatwa, anatuhumiwa kwa kosa la kutakatisha fedha, kwa hiyo anayetaka kuthibitisha hilo ni suala la kuja tumueleze ukweli wa jambo hilo.” Tukio hilo limejiri baada ya mgombea urais huyo, kuandika katika ukurasa wake wa Twitter Septemba 16, 2020, kuwa msaidizi wake amechukuliwa na watu wasiojulikana, na hivyo akatoa masaa kadhaa ili awe amepatikana.
 
Nafanya kijasusi
 
Hapa kuna kiini macho kikubwa sana
 
.Chadema and Tundu Lissu need to reach out to Bernard Membe and give him an opportunity to exit the race gracefully.
Dakika ya 89....labda watampandisha jukwaani tarehe 27 Oct.
 
Membe kama kulikuwa na heshima imebaki baada ya hapa huyu mtu nihatari kuliko corona. Nahisi watu wamemshtukia mapema huyu ni mtu hatari sana yuko pale kwa kazi maalumu na kama jasusi basi ni wa CCM.

CDM walijifunza 2015 na wana mtandao mzuri wa kijasusi ndani ya chama ACT sijui kama walikuwa serious mwanzo wamemshtukia baada ya kuanza mchakato. CCM wanaogopa zaidi Zanzibar sio bara naona mzee kashtukiwa mapema sasa jasusi hapeleki info zakusaidia uchaguzi Zenji.
 
Mtajuana wenyewe. Mliambiwa mkajifanya kutia pamba sikioni. Mnalialia nini sasa?
 
Huyu bwana mkubwa moyo wangu ulisha mtilia Shaka Sana tangu kipindi Cha huakiki nec aliposema ameamua kwenda kuhakiki form za wadhamini ili asiletewe zengwe na nec kipindi hicho mgombea wa chadema ilikua bado na ikumbukwe lissu hakupeleka form zake kuhakikiwa kabla alizipeleka siku ya kuteua wagombea wa urais,
 
Huyo hana lake amejuulikana mapema.
Uzuri ni kwamba hana nafasi yoyote yenye maamuzi katika chama. Mshauri hana issue na si mjumbe wa halmashauri kuu.
 
Bao la dakika ya 89 analofunga Membe ni la kujifunga kwny timu yake aliopo kwa Mkopo sio timu yake ya kudumu

Baada ya Uchaguzi na kutangazwa matokeo na kumuapisha Hussein Mwinyi Rais mteule wa Znz, kazi ya Seif na Kina Jussa itakuwa kuja mahakama kuu kupigania Uanachama wake wa ACT usifutwe kutokana na kesi zitazofunguliwa na umoja wa Wagombea Ubunge na udiwani wa ACT Nchi nzima waliokerwa na uvunjifu wa Katiba na usaliti uliofanywa na hawa kina Seif na Zitto dhidi ya Mgombea halali wa Chama chao hadharan

Seif alimsalitigi Jumbe tukajua kishakoma kumbe bado safari hii kamsaliti tena Membe…kweli Usaliti ni tabia ya kwny DNA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…