Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Unaweka hisia kwenye facts ulipwe 4000 tzsh siku nzima tena kwa Dar? Anae fanya iyo kazi ni mwehu na ana upungufu wa kufikiri
Unampa chaguo lipi lingine ili akalipwe mapesa mengi?
Saa moja asubuhi mpaka saa Moja jioni wanaruhusiwa
Wanachoka sana.Sasa ni heri uwatafutie sehemu nyingine wafanye kazi kwa muda mfupi na walipwe vitita vinono.
NB:Hawawezi kumsusia kazi zake na kujiondokea?
 
Sasa unamlaumu wakati kazi yenyewe kibarua Tena ni unskilled workers!

Ukiona haitoshi tafuta pazuri ukafanye kazi, hii Dunia ni soko hulia. Hiyo unayoidharau Kuna mwingine Hana hata pa kuipata Toka asubuhi Hadi jioni.

Yeye analipa kulingana na anavyoweza, anzisha viwanda vyako uongeze ujira kwa wafanyakazi wako.
 
mkiambiwa kuwa ubaguzi umekithiri Tanzania mnakataa! Kulikuwa na haja gani ya kutaja uasili wake? Kwani yeye sio mtanzania kama wewe? Grow up wacha ubaguzi wa rangi! Kama unaona afanyalo ni kosa unahaki kulisema lakini sio kwa kutumia lugha za kibaguzi.
 
Si Kweli, MO Kibarua analipwa 7 na kitu kama 7500 hivi kwa siku na pia hawa sio waajiriwa wa MO bali kuna kampuni zinachukua hio Tenda wanakubaliana na MO wanapewa hela na wao ndio wanaoajiri hao Vibarua.
 
Exactly! Jamaa analalamika wakati yeye mwenyewe hawezi hata kumuajiri mtu mmoja lakini analaumu anaeajiri watu tele kufanya kazi zisizo na skill yeyote ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…