Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze

Wanabodi.
Declaration of interest, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo na uzoefu wa muda mrefu kwenye newsroom hivyo kuweza Kufanya habari yoyote ya kiuchunguzi, ila kwa vile najitegemea nimeamua kujikita katika habari za kimaendeleo, developmental news zenye impact kwa maendeleo ya taifa. Hivyo siwezi kufutilia habari yoyote ambayo haina maslahi chanya kwa taifa.

Tangu kuibuka kwa Tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kughushi vyeti, savers za JF zimezidi kujazwa kwa ma thread na mathread kuhusu sakata hili.

Hata mimi niliwahi kumshinikiza Makonda ajitokeze kukanusha kwa hoja kuwa Uongo ulisemwa sana, bila kukanushwa haweza kugeuka ni ukweli.

Kiukweli uongo siku zote utabaki kuwa ni uongo tuu hata ukisemwa vipi au mara ngapi, hauwezi kugeuka ukweli.

Na ukweli siku zote utabaki kuwa ni ukweli hata usiposemwa. Ukituhumiwa kwa tuhuma zozote za uongo au kuzushiwa jambo baya lolote, as long as unajua ni uongo, huna haja ya kukanusha, wewe jinyamazie tuu kimya, ule msemo wa "tell the truth and the truth will set you free" ni msemo wa uongo, just keep the truth and the truth will remain the truth.

Sasa Tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizi za Makonda kughushi vyeti na kutumia majina bandia, nimekuja kugundua kuwa kumbe tuhuma hizi na shutuma zote ni uongo mtupu, ni za uzushi tuu kutaka kumfanyia fitna kwa kumpiga majungu, zinazazushwa na watu wenye wivu na kumuonea kijicho dhidi ya mafanikio yake lima Isha na jinsi alivyoshinda vita hii ya madawa ya kulevya kwa muda mfupi.

Wito wangu kwa Makonda ni kuendelea kutulia hivyo hivyo, kwa kunyamaza, usijibu kitu, just keep calm, endelea kuchapa kazi kwa sababu hawa watu watakusema mchana na usiku watalala, kesho yake wateandelea kusema, watasema wee, watasema wee mwisho watachoka.

Kanuni ya tuhuma zozote kwa kawaida ni "he who alleges must prove" waache waendelee kujifurahisha kwa kujaza severs za JF.

Yote yanayosemwa kuhusu Makonda Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Tuwapuuze! .

Na huu ni wito wangu kwa wazushi hawa, msiendelee kutujazia severs zetu. Kama tuhuma zenu zinaukweli wowote, kwanini mpaka leo mmeshindwa kuzithibitisha?!.

Ningeamua kufanya investigative piece ya hii story lakini...
1. Hakuna hata mtu mmoja aliyekwenda kijiji cha Kolomije kuuliza majina ya wazazi wa Paul Cristian Makonda kama hayo yao na kuuliza jina la mtoto wao wa pekee kama kweli ni Paul Christian Makonda?. Pia watawauliza wazazi wao Paul alizaliwa lini alipewa majina gani, alikulia wapi, alibatizwa wapi, alibatizwa wapi kws majina gani, aliandikishwa darasa la lini, shule gani kwa majina gani, katika simulizi hiyo ya wazazi wake, kusipoibuka majina ya Daudi Albert Bashite, wanaweza kuwauliza wazazi wake kama wanajua lolote kuhusiana na majina ya Daudi Albert Bashite.

Baada ya kupata taarifa hizo, hizo zinakuwa ni primary sources, ukitoka hapo unazitafutia collaborative sources za majirani hapo kijijini ku verfy taarifa za wazazi wake.

2. Hatua ya pili ni kuripoti shule ya Kolomije si bado ipo, wameshindwa nini kwenda kuwauliza jina la huyo mwanafunzi Paul Chirtian Makonda waliotajiwa na wazazi wake kisha wamuulizie na Daudi Albert Bashite aliandikishwa lini alimaliza lini na kwa majina gani na kama alifaulu au alifeli.

3. Baada ya hapo ni kwenda Shule ya Sekondari ya Pamba na kuulizia mwafunzi aliyefeli shule ya msingi, amewezaje kuingia Sekondari ya serekali. Kisha waulizie kuhusu mwafunzi Paul Christian Makonda na Daudi Albert Bashite walijiunga lini kwa majina yapi, wakamaliza lini na matokeo yao ni yapi.

4. Unakwenda chuo cha uvuvi Nyegezi unapata details na documentary evidence ya jina la Paul Christian Makonda alilojisajili na vyeti alivyo wasilisha wakati alijiunga na vyeti alivyo hitimu. Hapo Nyegezi ukikuta majina tofauti ya shule na vyeti, unafanya back to back ya shule ulizokuta na kuzipitia ku verfy Paul Christian Makonda alisoma hapo.
5. Unaripoti Mbegani unapata details za Paul Christian Makonda na documentary evidence ya majina aliyotumia kujiunga na vyeti aliyotumia na vyeti vya kuhitimu.

6. Unaripoti chuo cha Ushirika you do the same.
Mkumbuke hizo info zote ni public info ambazo ziko freely accessible. Kama Kuna any discrepancies zozote za majina kwenye hivyo vyeti kati ya Paul Christian Makonda na Daudi Albert Bashite then una launch secondary investigation kwa kuandika barua kutumia kipengele cha sheria ya "the right to information act ku access protected info kutaka

7.Vizazi na vifo alipozaliwa aliandikishwaje? .

8. Idara ya Uhamiaji ina file la DN Number alipoomba passport aliwasilisha nyaraka gani na za wazazi wake zikiwemo affidavits zao.

9. Unakwenda mamlaka yake ya ajira kuangalia aliwasilisha vyeti gani

10. Unamkabili Paul Makonda mwenyewe na vielelezo vyote kuthibitisha yeye ni Daudi Albert Bashite bila kusema kuwa ni mwizi wa jina wala amefanya forgery or fraud. Unamtupia mezani kwake na kumpa kamba ama ajinyonge yeye mwenyewe ama ajinasue.

Hata Makonda akigoma kutoa ushirikiano, you have facts to go on with the story with or without Makonda's imput. Kazi ya mwandishi ni kuwalisha facts only hivyo unaibuka na big headline "Uthibitisho Paul Chritian Makonda ndiye Daudi Albert Bashite " huku umetutundikia hizo evidence.

Kinyume cha hapo sisi akina Tomaso wote tunaendelea kuamini kuwa kumbe tuhuma zote hizi dhidi ya Makonda ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!.

Uthibitisho wa uzushi ni huu ukweli bayana uliopo hadi sasa kuwa Mhe. Paul Christian Makondo ni mteule wa rais wa JMT aliyefanyiwa vetting na vyombo husika na kuthibitisha pasipo shaka wasifu wake hivyo akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na mpaka sasa huu ndio ukweli bayana na halisi uliopo. Kati ya wazushi hawa na rais wetu aliyemwamini na kumteua nani mkweli? . Mkweli ni Rais, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli ndio maana katulia tuu nyie endeleeni kupiga kelele.

Watanzania tupunguze kushadadia uzushi, tujiunge na rais wetu kumtia moyo Mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda endelea kuchapa kazi, na sisi wengine wote katika umoja wetu, tuwapuuze kabisa watu hawa wasiolitakia mema taifa letu.

Nawatakia Jumatano Njema ya Majivu, leo ni siku ya kufunga kwa sisi Wakristo Wakatoliki, tunaanza mfungo wa siku 40 za Kwaresma.
Kwaresma Njema
Paskali

Nimefungua uzi wako fasta fasta nikijua UTAKUJA NA USHAHIDI. Kumbe ni blah blah tu kwasababu Daudi Bashite ni msukuma mwenzako.

Daudi Albert Bashite Ajitokeze aweke vyeti vyake hadharani
 
Nimepitia aisee..Wakati tunasubiri hatua kuchukuliwa(kama kweli kuna hatua zozote zitachukuliwa) hivi ndo vitu tunavyotaka kusikia atleast kujiridhisha kwa tuhuma zinazomkabili...Wakitokea na maclassmates,majirani na watu wengine wa karibu kuthibitisha hili itakua poa zaidi..Hata kama hatua zozote hazitachukuliwa tutakuwa tunajua ukweli ni upi..
Yaani huyo Mama anaonekana anamfahamu Makonda vizuri ile mbaya lakini sio mtu wa maneno!!! Stori ya kutunga utaijua tu lakini maelezo ya huyo mama yanaonekana ni very pure!!!!
 
M
Pasco mayala kajitoa fahamu yy hujui chochote kwa sasa zaidi ya kumtetea makonda tu hataki kujua udhaifu na mapungufu ya boss wake Daud Albert.
Waandishi wanaambiwa watafute ushahidi sio kubwabwaja. Uzushi ni mbaya sana yaani bora watu waendele na madawa ya Kulevya.
 
Yaani huyo Mama anaonekana anamfahamu Makonda vizuri ile mbaya lakini sio mtu wa maneno!!! Stori ya kutunga utaijua tu lakini maelezo ya huyo mama yanaonekana ni very pure!!!!
Maelezo ya huyo mama sina shaka nayo,Ukizingatia aliyaongea haya wakati hakuna vuguvugu lolote la hiki kinachoendelea..
 
Utumwa wa fikra huo.....

Wapo waliokwenda kwa wazazi wao na kuwahoji ... majibu yapo.

Kijijini kwao sio mbali, tulioko jijini Mwanza tumeishapewa ukweli wa kila kitu ...

Muulize kama hawafahamu akina Poneja ... wanamfahamu vizuri sana hata yeye anajua hilo.

Kama unataka akujali kwenye maslahi yako binafsi useme ila hatutaki uongo hapa JF.
Mkuu Tutor B,Paskali hajatetea ila ameonesha njia mbadala ya kutuhumu nayo ni kuthibitisha tuhuma kwa kupitia njia alizoainisha!
Kwa utaratibu wa sasa juu ya kadhia hii itaonekana ni uzushi tu,sasa huyo aliyekuja na madai kwamba kaongea na ponela sijui wazazi asiishie hapo akatafute vifungashio vingine vya tuhuma zake ndipo ampige navyo usoni mkuu wa mji!
Zaidi ya hapo naungana na Pasco kuwa ni uzushina upuuzwe hata kama Makonda hata kanusha kwani hiyo burden ya kuthibitisha haiko kwake !
 
Mamaphilipo,

Tafadhali sana popote pale ulipo njoo ututetee dhidi ya Pascal Mayalla!!! Nakuomba wewe kwa sababu, baada ya kufanya utafiti wa haraka haraka nimegundua wewe ni mtu wa mwanzo au miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kufichua jina la Daudi Bashite kupitia post yako ya December 2015 ambayo ni hii hapa:Wakati huo, hata haya mambo ya wauza mihadarati yalikuwa bado manake kuna wengine wanasema ni njama za wauza mihadarati!! Post yako nyingine ni hii hapa:

Kwenye post ile Mamaphilipo pia ukaelezea mshangao wako ambao uliupata pale uliposikia Makonda amekula uteuzi:

Sie wengine tunasingiziwa kwamba eti tuna wivu, chuki na roho ya ndoano!! Nimepitia profile yako Mamaphilipo! Wala hulekei kwamba una elements za ushabiki wa kisiasa au chuki yoyote dhidi ya Makonda!!

Pia nimepitia profile yako na una muda mrefu sana hujaingia JF at least kwa kutumia hiyo ID!!! Hebu Mungu akulete hapa JF... ni kweli tuna chuki?! Ina maana Mamaphilipo na wewe una chuki?! Kama nawe ni mwingi wa chuki; unataka kumfundisha nini Philipo?!!!!
Kweli kabisaaa, mamaphilipo fanya uje huku kituokoa tumalize mechi...basi hata kwa ID fake...utusaidie na uwasaidie waandishi wa habari za kiuchunguzi

Please Mama philipo...hata tukipata circumstancial evidences inatutosha...mfano watu waliosoma nae, wasiogope tutawaziba suraaa....

Wako katika ujenzi wa Dar salaam
1315ceb23ccca90444be4abf4b1dd754.jpg
 
Asante sana Pasco.

Ushauri kwa kuwa wewe ni mdau mkubwa wa Jf ningeomba post zooote zinazohusiana na ishu hiyo ya kizushi ima ziunganishwe au zifutwe na ibakie moja tu. Ili yeyote anayetaka kuendelea na upuuzi huo au wapuuzi wote wakusanywe pamoja. Fikisha Maombi kwa Max na timu yake. Haiingii akilini Jf nzima ionekane hakuna mambo mengine ya kitaifa yanayoendelea
 
Hata mi nashangaa kwenye jf wanazungumziwa watu wawili tu makonda na mh magufuli basi karibu wiki mbili sasa kana kwamba hakuna jambo lingine muhimu
 
Labda asingetaja wauza unga akataja group lenye dhambi tofauti isingefika hapa,hii yote ni dalili kwamba vita ya madawa ya kulevya Tanzania ni ngumu,hivi nani mkamilifu nchi hii ilivyokuwa imeoza?asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe,,maneno ya Yesu,vyeti vilikuwa vinauzwa hadharani hasa pale shule ya uhuru railway quoters,kila mtu anajua hilo ni nani hajawa victim wa vyeti bandia nchi hii? Nimefanya kazi na watu wengi sana wanatumia vyeti sio vyao,tuache unafiki hili sio kosa la Makonda ni system iliruhusu upuuzi huu kuwepo,kwa nini tumlaumu Makonda kiasi yeye ni binadamu mwenye dhambi kama wote mlivyo na dhambi,yote haya ni kwa sababu ya ujasiri wake wa kutaja wahusika washutumiwa??hivi nchi yetu imeongozwa na watu wangapi wenye vyeti vya kutisha na maisha ni yaleyale afadhali ya jana??jamani watanzania tuna matatizo mengi sana na uchumi umeharibika sana na hali za maisha zimekuwa mbaya tusijifanye hatuoni mambo muhimu,mngekuwa na nia nzuri mngejadili jinsi ya kuiondoa ccm iliyotufikisha hapa kumjadili MTU is too late my people,
Acha porojooo, ishu ya utata wa majina ya daud bashite imeanza kitambo, msijidanganye imeanza baada ya madawa ya kulevya
338ccb2cde03218d7bacdb761c35d109.jpg

[HASHTAG]#Mamaphilipo[/HASHTAG] upo wapi????
 
Wanabodi.
Declaration of interest, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo na uzoefu wa muda mrefu kwenye newsroom hivyo kuweza Kufanya habari yoyote ya kiuchunguzi, ila kwa vile najitegemea nimeamua kujikita katika habari za kimaendeleo, developmental news zenye impact kwa maendeleo ya taifa. Hivyo siwezi kufutilia habari yoyote ambayo haina maslahi chanya kwa taifa.

Tangu kuibuka kwa Tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kughushi vyeti, savers za JF zimezidi kujazwa kwa ma thread na mathread kuhusu sakata hili.

Hata mimi niliwahi kumshinikiza Makonda ajitokeze kukanusha kwa hoja kuwa Uongo ulisemwa sana, bila kukanushwa haweza kugeuka ni ukweli.

Kiukweli uongo siku zote utabaki kuwa ni uongo tuu hata ukisemwa vipi au mara ngapi, hauwezi kugeuka ukweli.

Na ukweli siku zote utabaki kuwa ni ukweli hata usiposemwa. Ukituhumiwa kwa tuhuma zozote za uongo au kuzushiwa jambo baya lolote, as long as unajua ni uongo, huna haja ya kukanusha, wewe jinyamazie tuu kimya, ule msemo wa "tell the truth and the truth will set you free" ni msemo wa uongo, just keep the truth and the truth will remain the truth.

Sasa Tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizi za Makonda kughushi vyeti na kutumia majina bandia, nimekuja kugundua kuwa kumbe tuhuma hizi na shutuma zote ni uongo mtupu, ni za uzushi tuu kutaka kumfanyia fitna kwa kumpiga majungu, zinazazushwa na watu wenye wivu na kumuonea kijicho dhidi ya mafanikio yake lima Isha na jinsi alivyoshinda vita hii ya madawa ya kulevya kwa muda mfupi.

Wito wangu kwa Makonda ni kuendelea kutulia hivyo hivyo, kwa kunyamaza, usijibu kitu, just keep calm, endelea kuchapa kazi kwa sababu hawa watu watakusema mchana na usiku watalala, kesho yake wateandelea kusema, watasema wee, watasema wee mwisho watachoka.

Kanuni ya tuhuma zozote kwa kawaida ni "he who alleges must prove" waache waendelee kujifurahisha kwa kujaza severs za JF.

Yote yanayosemwa kuhusu Makonda Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Tuwapuuze! .

Na huu ni wito wangu kwa wazushi hawa, msiendelee kutujazia severs zetu. Kama tuhuma zenu zinaukweli wowote, kwanini mpaka leo mmeshindwa kuzithibitisha?!.

Ningeamua kufanya investigative piece ya hii story lakini...
1. Hakuna hata mtu mmoja aliyekwenda kijiji cha Kolomije kuuliza majina ya wazazi wa Paul Cristian Makonda kama hayo yao na kuuliza jina la mtoto wao wa pekee kama kweli ni Paul Christian Makonda?. Pia watawauliza wazazi wao Paul alizaliwa lini alipewa majina gani, alikulia wapi, alibatizwa wapi, alibatizwa wapi kws majina gani, aliandikishwa darasa la lini, shule gani kwa majina gani, katika simulizi hiyo ya wazazi wake, kusipoibuka majina ya Daudi Albert Bashite, wanaweza kuwauliza wazazi wake kama wanajua lolote kuhusiana na majina ya Daudi Albert Bashite.

Baada ya kupata taarifa hizo, hizo zinakuwa ni primary sources, ukitoka hapo unazitafutia collaborative sources za majirani hapo kijijini ku verfy taarifa za wazazi wake.

2. Hatua ya pili ni kuripoti shule ya Kolomije si bado ipo, wameshindwa nini kwenda kuwauliza jina la huyo mwanafunzi Paul Chirtian Makonda waliotajiwa na wazazi wake kisha wamuulizie na Daudi Albert Bashite aliandikishwa lini alimaliza lini na kwa majina gani na kama alifaulu au alifeli.

3. Baada ya hapo ni kwenda Shule ya Sekondari ya Pamba na kuulizia mwafunzi aliyefeli shule ya msingi, amewezaje kuingia Sekondari ya serekali. Kisha waulizie kuhusu mwafunzi Paul Christian Makonda na Daudi Albert Bashite walijiunga lini kwa majina yapi, wakamaliza lini na matokeo yao ni yapi.

4. Unakwenda chuo cha uvuvi Nyegezi unapata details na documentary evidence ya jina la Paul Christian Makonda alilojisajili na vyeti alivyo wasilisha wakati alijiunga na vyeti alivyo hitimu. Hapo Nyegezi ukikuta majina tofauti ya shule na vyeti, unafanya back to back ya shule ulizokuta na kuzipitia ku verfy Paul Christian Makonda alisoma hapo.
5. Unaripoti Mbegani unapata details za Paul Christian Makonda na documentary evidence ya majina aliyotumia kujiunga na vyeti aliyotumia na vyeti vya kuhitimu.

6. Unaripoti chuo cha Ushirika you do the same.
Mkumbuke hizo info zote ni public info ambazo ziko freely accessible. Kama Kuna any discrepancies zozote za majina kwenye hivyo vyeti kati ya Paul Christian Makonda na Daudi Albert Bashite then una launch secondary investigation kwa kuandika barua kutumia kipengele cha sheria ya "the right to information act ku access protected info kutaka

7.Vizazi na vifo alipozaliwa aliandikishwaje? .

8. Idara ya Uhamiaji ina file la DN Number alipoomba passport aliwasilisha nyaraka gani na za wazazi wake zikiwemo affidavits zao.

9. Unakwenda mamlaka yake ya ajira kuangalia aliwasilisha vyeti gani

10. Unamkabili Paul Makonda mwenyewe na vielelezo vyote kuthibitisha yeye ni Daudi Albert Bashite bila kusema kuwa ni mwizi wa jina wala amefanya forgery or fraud. Unamtupia mezani kwake na kumpa kamba ama ajinyonge yeye mwenyewe ama ajinasue.

Hata Makonda akigoma kutoa ushirikiano, you have facts to go on with the story with or without Makonda's imput. Kazi ya mwandishi ni kuwalisha facts only hivyo unaibuka na big headline "Uthibitisho Paul Chritian Makonda ndiye Daudi Albert Bashite " huku umetutundikia hizo evidence.

Kinyume cha hapo sisi akina Tomaso wote tunaendelea kuamini kuwa kumbe tuhuma zote hizi dhidi ya Makonda ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!.

Uthibitisho wa uzushi ni huu ukweli bayana uliopo hadi sasa kuwa Mhe. Paul Christian Makondo ni mteule wa rais wa JMT aliyefanyiwa vetting na vyombo husika na kuthibitisha pasipo shaka wasifu wake hivyo akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na mpaka sasa huu ndio ukweli bayana na halisi uliopo. Kati ya wazushi hawa na rais wetu aliyemwamini na kumteua nani mkweli? . Mkweli ni Rais, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli ndio maana katulia tuu nyie endeleeni kupiga kelele.

Watanzania tupunguze kushadadia uzushi, tujiunge na rais wetu kumtia moyo Mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda endelea kuchapa kazi, na sisi wengine wote katika umoja wetu, tuwapuuze kabisa watu hawa wasiolitakia mema taifa letu.

Nawatakia Jumatano Njema ya Majivu, leo ni siku ya kufunga kwa sisi Wakristo Wakatoliki, tunaanza mfungo wa siku 40 za Kwaresma.
Kwaresma Njema
Paskali
Kaka kipindi hicho Pamba sec haikuwa ya serikali bado na wewe unabashiri tu hujatafiti!
 
Sasa Pascal kweli unaamini haya yote watu wameyapataje? Gwajima mweneywe kakuambia wanatoka kijiji kimoja. Sasa atashindwaje kupata taarifa zake! kama uchunguzi huo usingekuwa umefanywa watu wangewezaje kuja na details zote hizo kuhusu Makonda? Tuhuma zote hizi hakuna hata mtu mmoja amejitokeza kuzikanusha kwa vielelezo? Au ndio vielelezo vinatengenezwa? Mbona Mwigulu alikuja fasta kutolea maelezo jina lake na kwa kiasi fulani akaeleweka? Kwa nini Makonda? Ni arrogance tu na kujisikia yeye ni kipenzi cha mkulu kunakompa kiburi hiki! huwezi kutuhumiwa kwenye vyombo vya habari kama kiongozi halafu eti upotezee! The rule says, "silence means Yes"!
 
Paskali bora hukuchagua kazi ya ualimu, maana ungekuwa unatunga mitihani migumu kiasi cha kulisha sup darasa zima.
Nimesikitika kuona hata wakongwe wa jf ninao waamini leo wameingia chaka
 
Asante sana Pasco.

Ushauri kwa kuwa wewe ni mdau mkubwa wa Jf ningeomba post zooote zinazohusiana na ishu hiyo ya kizushi ima ziunganishwe au zifutwe na ibakie moja tu. Ili yeyote anayetaka kuendelea na upuuzi huo au wapuuzi wote wakusanywe pamoja. Fikisha Maombi kwa Max na timu yake. Haiingii akilini Jf nzima ionekane hakuna mambo mengine ya kitaifa yanayoendelea
Max si mpumbavu kama wewe au mwenye njaa kama ya Pasco.
 
Kuna watu ni wanafiki mno leo anasema hili alafu kesho amabadilika.
Muda mwengine inatia kinyaa kusoma baadhi ya nyuzi za watu maana ni wanafiki mno
Nafikiri hamjamuelewa Paskali. Anachofanya hapa ni kumuonesha VICTIM kuwa hamna pa kujificha ikiwa watu wataamua. Na ujumbe huu pia utamshtua Mteuzi
 
Back
Top Bottom