Kwa watu walioishi Kasulu Miaka ya 2000 siku za siku kuu tulikuwa tunaenda kuruka majoka pale FM CLUB karibu na shule ya Kiganamo hizi ngoma ndio zilikuwa habari ya mujini.......Nakumbuka siku kuu moja nilivaa nguo za kufanana suruali na shati rangi ya kijani ya jeshi ile suruali ukiamua unaikata inakuwa pensi kwa kutumia zipu,faza alitoka nazo Uganda miaka hiyo Uganda ndio habari ya town ilikuwa brand ya ECKO ina picha ya tembo kama sijakosea,zama zimepita unaweza kulia machozi kwa kumbukumbu....Abby skillz alikuwa mkali sana.