GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Nimejaribu hii Mikwara Miwili ndani ya Siku Mbili tofauti ambapo Vibaka walitaka Kunichania Nyavu Ghettoni Kwangu waniibie hii Simu yangu ya Kimasikini ya Tecno F1 na imesaidia Kuwatoa Baru ( Kuwakimbiza ) ila Hofu yangu Siku wakija Kushtukia kuwa sina lolote nahisi Watanipanya Rodi vibaya mno.
Jumamosi iliyopita mida ya Saa 10 Alfajiri Kibaka alikuja Dirishani Kwangu Uswahilini na nilipojua kuwa eneo hilo nikaamka huku nikijifanya naongea na Simu na Mjeda ( Mwanajeshi ) nikisema.."Afande Kobelo hii Bunduki uliyonikabishi si inaweza ikarusha Risasi kwa haraka hata kama Adui yuko kwa mbali kama ambavyo tuliua Yule Jambazi Keko?"..... na nilipomaliza tu Kuongea hivyo nikakuta Mtu hayuko Kakimbia na kaniachia tu Bisibisi yake na kubaki Kucheka tu Mwenyewe.
Juzi Jumatatu mida ya Saa 9 hivi alikuja tena Kibaka kutaka Kuniibia Dirishani na nilichoamua kufanya kwa huyu ni Kwanza kufungua Pazia la Ghettoni Kwangu nikijua kuwa Kajibanza na Kuwasha Taa Kimakusudi.
Kilichofuata baada ya hapo ni Mimi Kujifanya ni mwana Karateka ( Mdogo wake Bruce Lee ) na kuanza Kuonyesha Styles zote za Karate nilizozikariri kutokana na Kutizama mno Sinema za Bruce Lee ambapo kuna Style Moja ya kupiga Ukuta na Kichwa niliifanya huku nikilia kwa Mzuka wa Wanakarateka na kumsikia Yule Kibaka akinisonya na kunitukana kisha Kuondoka zake ndiyo ikawa pona yangu.
Hata hivyo pamoja na Kujitutumua kote kule mbele ya Kibaka na kujifanya mwana Karateka kwa Kupiga Ukuta kwa Kichwa hivi sasa nauguza Nundu na Asante kwa Barafu za Jirani kwa Kuniponya hii Nundu.
Asikuambie Mtu Mikwara inalipa!!!!!!
Cc: adriz, Bila bila, Bujibuji Simba Nyamaume, Sky Eclat, Frank Wanjiru, Daudi Mchambuzi etc.