Kumbe Sultan Jamshid Alifurahia Kuuawa kwa Karume!. Alitaraji Kurejea Kama Sultani, Kumbe...

Kumbe Sultan Jamshid Alifurahia Kuuawa kwa Karume!. Alitaraji Kurejea Kama Sultani, Kumbe...

Nawatakia kumbukumbu njema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyovikomboa visiwa hivi.
P
 
Tuliozaliwa baada ya uhuru na mapinduzi ZNZ inabidi kweli kufanya research yakinifu, uzuri wote waliotajwa tumewasikia kuhusika, tatizo ukweli wenyewe ni upi?!
 
Kàtika makala yote Mimi nimeona haha ka Sentensi....Zanzibar,a semi autonomous Region of ... 🤣 🤣
 
Haya mambo kumbe yalianza enzi za Sultan Jamshid. Mijizi na Mafisadi ndio Masultan Jamshid wa leo. Si ajabu tumeona picha za familia ikisherehekea pasaka huku mkuu wa Kaya akiwa juu ya kiti ADC.
 
Huku bwana yule akiwa anaongoza malaika kama alivyosema mwenyewe.
Lisu hata apewe mi
Huku bwana yule akiwa anaongoza malaika kama alivyosema mwenyewe.
Lisu alitegemea sana uwepo wa Magufuli kujipatia umaarufu, kwa kua hayupo Lisu is no longer relevant,

Hata sasa anavyoendelea kumshambulia watu wanamwona kama mental case tu.

Your guy is no longer relevant deal with it.
 
Lisu hata apewe mi
Lisu alitegemea sana uwepo wa Magufuli kujipatia umaarufu, kwa kua hayupo Lisu is no longer relevant,

Hata sasa anavyoendelea kumshambulia watu wanamwona kama mental case tu.

Your guy is no longer relevant deal with it.
Wewe deal na mtakatifu wako aliyepewa umalaika mkuu kwa sasa,sisi tunadunda tu na maisha yetu kama kawa.
 
Wanabodi,
Kwanza tazama na kusikiliza mahojiano haya kwa kituo!.

Utangulizi: Somo la Historia ni somo la mambo ya kale kwa lengo la kujua yaliyotokea nyuma, kulinganisha na yanayotokea sasa, ili kujua kujua yale yatakayokuja kutokea siku za usoni!.

Hivyo katika kuperusi baadhi ya video za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, nimekutana na video nyingi zenye urongo wa kupikwa kwa kuuchanganya na ukweli kidogo tuu ili ku make believe kuwa kila kitu ni kweli tupu!.

Lakini miongoni mwa video hizo za urongo, nimekutana video hii ambayo ni ya kweli,
inaonyesha mahojiano ya Sultani wa mwisho aliyepinduliwa Zanzibar katika yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ya 1964, na kukimbilia uhamishoni!, huyu ni Sultan Jamshid!.

Baada ya mauaji ya Muasisi na Shujaa wa Mapinduzi yale Sheikh Abedi Amani Karume, mwaka 1972, BBC ilifanya mahojiano na Sultan huyu mkimbizi, jiji London. Sultan Jamshid alitamka wazi kufurahia mauaji yale na akawa anasubiria kwa matumaini kuitwa kurejea Zanzibar kuendelea kuwa Sultan!.

Jee hivi kweli kuna binadamu anayefurahia kifo cha binadamu mwingine?!. Mimi ni pro life, siungi mkono kifo cha aina nyingine yoyote zaidi ya kazi ya Mungu!, hata adhabu ya kifo, na sifurahii kifo chochote au kumwagika kwa damu yoyote kwa sababu yoyote ndio maana ni miongoni mwa tuliomlilia Osama, Saadam na Ghadafi!.
Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo
Adhabu ya Kifo: Jee kweli bado inahitajika? |
Wana JF tuungane kusema NO hukumu ya kifo
Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika ..
Karume Aliuwawa Na Utawala Dhalimu wa Sultan
[URL='https://www.jamiiforums.com/threads/iwapo-ccm-itashindwa-zanzibar-nini-majaaliwa-ya-muungano.838604/']Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano .
Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila .
Mapinduzi ya Zanzibar: Ukweli ni Upi?
Wananchi wakitaka kujua nani alimuua nani?[/URL]


Sasa jee wajua msingi wa furaha ya Sultan Jamshid kwa kifo cha Karume?!. Sikiliza kwa makini, ameeleza mwenyewe!.

Ila jee wajua baada ya kifo cha Karume, ni nini kilimkwamisha Sultan Jamshid asiitwe tena Zanzibar kuurejelea Usultani wake?!, ukikijua, naamini utajua kwa nini kuna mtu kila siku anashinda uchaguzi wa Zanzibar lakini hatangazwi!.

Sii wengi humu wanaojua kuwa miongoni mwa inteligensia kubwa zaidi duniani, ni intelijensia ya vinasaba!. Wanaintelijensia wamemaliza kazi yao zamani na kubaki kuangalia senema za siasa!.

Endeleeni kusubiria 2020 kujaribu tena, wenzenu wanaoijua historia hii na sababu zilizomo ndani ya mahojiano haya, wanawaangalia tuu jinsi watu wanavyoruhusiwa kujifurahisha kwa maigizo la uchaguzi hadi uchaguzi!.

Ukiujua ukweli utakuweka huru, ushauri wa bure, kwa 2020 badilisheni mgombea kuepuka visingizio vya taarifa za kinteligensia vya uhusiano wa vinasaba ya kuwa kumpa fulani ni kumrejelesha Sultan aliyepinduliwa kwa mlango wa nyuma!.

Pamoja na madhila yote ya Muungano yanayolalamikiwa na upande wa pili, ila kiukweli kuna maeneo fulani fulani, Muungano umesaidia!, maana just imagine, usingekuwepo Muungano huu adhimu, hali ingekuwaje?!.

Mapinduzi Daima!.
Muungano Milele.
Pasco

Kweli amesema kuwa amepata faraja kuondoka kwa Karume . Kwani alisema yeye ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu ya dhulma zilizotokea.

Na kasema ikiwa watu wanataka arudi atakubali kurudi. hajasema kurudi kama mfalme.
Hata Salmi Amour alitamka kuwa yupo huru kurudi.

Lakini ukweli usemwe. Alipokuja Jumbe raisi wapili
utawala wa sharia ulianza kurudi kidogokidogo.
Uchaguzi ulianza
Woga ulianza kuondoka
Ubaguzi ulianza kupunguwa
Elimu kwa wote ,khasa elimu ya juu, vijana wenye asili yakiarabu na yakiahindi walianza kupata fursa.
Scholar ship zikawa zinatolewa bila ubaguzi
Fursa za kazi bila ya ubaguzi ( nadhani isipokuwa polisi na jeshi)
 
Wanabodi,
Pamoja na madhila yote ya Muungano yanayolalamikiwa na upande wa pili, ila kiukweli kuna maeneo fulani fulani, Muungano umesaidia!, maana just imagine, usingekuwepo Muungano huu adhimu, hali ingekuwaje?!.

Mapinduzi Daima!.
Muungano Milele.
Pasco
Kero zote za Muungano zinakwenda kutatuliwa na kumalizika rasmi.
Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P
 
Ila jee wajua baada ya kifo cha Karume, ni nini kilimkwamisha Sultan Jamshid asiitwe tena Zanzibar kuurejelea Usultani wake?!, ukikijua, naamini utajua kwa nini kuna mtu kila siku anashinda uchaguzi wa Z
Huyu jamaa ambaye akishinda hatangazwi hayupo tena...huenda Sasa Wazenji wakatangaziwa mshindi halali kwenye chaguzi zijazo?
 
Huyu jamaa ambaye akishinda hatangazwi hayupo tena...huenda Sasa Wazenji wakatangaziwa mshindi halali kwenye chaguzi zijazo?
True, mfano wakimsimamisha huyu jamaa

Na jamaa huyu akaacha tabia yake ya kuuchokoa huu Muungano wetu adhimu kama hapa

Akisimamishwa, akishinda, anapewa!.
P
 
True, mfano wakimsimamisha huyu jamaa

Na jamaa huyu akaacha tabia yake ya kuuchokoa huu Muungano wetu adhimu kama hapa

Akisimamishwa, akishinda, anapewa!.
P
Una uhakika au ni hisia zako tuu.......kwani tatizo alikuwa ni mwenye vinasaba au chama tawala hawataki kuachia madaraka?...
 
Una uhakika au ni hisia zako tuu.......kwani tatizo alikuwa ni mwenye vinasaba au chama tawala hawataki kuachia madaraka?...
Siasa za Zanzibar ni ngumu sana!, vinasaba ni tatizo kubwa asije kuingia mtu wa kuonekana kama ni kumrejeleza Sultani. Hivyo ukimsimamisha Mbantu, hoja ya vinasaba inakufa.

2. Determinant ya mshindi wa urais wa Zanzibar ni mtu atakayedumisha Muungano wetu adhimu, hivyo huyu jamaa akiacha kuuchokoa Muungano, atapewa. Na ikitokea tayari ikiishapewa, kisha ndio akauchokoa muungano, tunamuita Dodoma, kule anakuja na msafara, baada ya kikao, anaondoka na gari moja, akisindikizwa nyumbani kwake na kamwe hutamsikia tena akizungumza lolote in public!.

P
 
Siasa za Zanzibar ni ngumu sana!, vinasaba ni tatizo kubwa asije kuingia mtu wa kuonekana kama ni kumrejeleza Sultani. Hivyo ukimsimamisha Mbantu, hoja ya vinasaba inakufa.
...hata utawala wa Ccm ni wa kisultani tu....sema unatumia koti la chama cha siasa kuuficha huo usultani.

Determinant ya mshindi wa urais wa Zanzibar ni mtu atakayedumisha Muungano wetu adhimu, hivyo huyu jamaa akiacha kuuchokoa Muungano, atapewa. Na ikitokea tayari ikiishapewa, kisha ndio akauchokoa muungano, tunamuita Dodoma, kule anakuja na msafara, baada ya kikao, anaondoka na gari moja, akisindikizwa nyumbani kwake na kamwe hutamsikia tena akizungumza lolote in public!.
Katiba mpya ni muhimu
 
Back
Top Bottom