Kwanza hata hiyo kuita awamu siyo hitaji la kisheria wala kikatiba. Kisheria na kikatiba, neno linalotambulika ni muhula. Huu ni muhula wa kwanza wa Rais Samia.
Neno awamu kwa mara ya kwanza lilianza kutumika wakati wa Mwinyi ili kutofautisha uongozi wa Mwalimu Nyerere na Mwinyi.
Katika matumizi, awamu haiangalii idadi ya miaka au mihula. Mwalimu aliongoza kwa miaka 24, ni awamu moja. Waliofuatia miaka 10 kila mmoja, ni awamu kamili. Magufuli miaka 5 na kidogo, ndipo awamu yake ilipoishia.
Kwa nini tusihesabu viongozi kabla ya uhuru - kabla ya uhuru hakukuwa na nchi, lilikuwa koloni la Mwingereza, na mkuu wa makoloni yote ya Uingereza alikuwa malkia. Kabla ya ukoloni, hakukuwa na nchi bali chiefdoms.