Kumbe Yesu alikua mfuasi wa Buddha

Vipi kuhusu mzee Ibrahim na manabii wengine mbona na wao walipozaliwa mpk kufika miaka 10 na kuendelea hawajatajwa walikuwa wapi wakati huo na walikuwa wanafanya nn. Sijuih na wao Mnataka kusema walikuwa Buddha wanafundishwa
 
Uzi umeshiba kwelikweli
 
Vipi kuhusu mzee Ibrahim na manabii wengine mbona na wao walipozaliwa mpk kufika miaka 10 na kuendelea hawajatajwa walikuwa wapi wakati huo na walikuwa wanafanya nn. Sijuih na wao Mnataka kusema walikuwa Buddha wanafundishwa
Toa mawazo yako ndio uulize swali hii tabia ya kujibu swali kwa kutumia swali inakosesha watu faida ya kujifunza
 
Mkuu kwa faida ya wote kwanini unafkiri habari za ujana wa Yesu hazikujumuishwa kwenye new testament canon ama vulgate!!!

Funguka
Nadhani hawakuona haja ya kuweka kila kitu kuhusu Yesu hasa maisha yake binafsi ya ujana,zaidi ya lengo kuu la ujio wa Yesu la kuhubiri habari njema.
 
Biblia kwa asilimia kubwa ni maneno ya watu na sio ya mungu....kiasi ya kwamba vijihoja vya hapa na pale vinashindwa kujibiwa na BIBLIA na hata wafia dini wake.....na kwa kua BIBLIA inaendeshwa na dhehebu moja kubwa ina maana wakristo walio wengi hawamuabudu mungu halisi bali sheria za dhehebu hilo......BIBLIA NA UKRISTO ZINAUTATA
 
Vipi kuhusu mzee Ibrahim na manabii wengine mbona na wao walipozaliwa mpk kufika miaka 10 na kuendelea hawajatajwa walikuwa wapi wakati huo na walikuwa wanafanya nn. Sijuih na wao Mnataka kusema walikuwa Buddha wanafundishwa
Wametajwa mkuu huyo Ibrahim toka anazaliwa nyota kubwa iliwaka mashariki ya kati, akakimbilia pangoni sijui mpambano wake na Nimrod n.k labda ungesema bible ndio haijaweka ila taarifa zao zipo kupitia vitabu vilivyoachwa kuingizwa kwenye bible sasa kutokuweka hizi taarifa au angalau kuziweka available kwa wakristo wote ndio kunaleta hizi sintofahamu ndio maana watu mpka leo wanadebate kama Yesu alioa au hakuoa!!
 
Watatokea Makristo wengi wa uongo, YESU KRISTO tunayemuabudu alikufa msalabani, akazikwa siku ya tatu akafufuka na kwa sasa yuko juu Mbinguni akituombea na kutupatia msamaha wa dhambi. Huyu Yesu wako unamjua wewe na vitabu vyako. Na wengine wengi wa uongo watatokea.
 
popbwinyo mitale na midimu
 
Hizo zote ni hypothesis, yaani Yesu amekufa miaka 2000 iliyopita alafu baada ya miaka 1800 aje mtu na hadithi kuhusu maisha ya huyo mtu? Hiyo hadithi ina defy logic. Maandiko ya kuaminika yapo na yameanza kutumika immediately baada ya kifo na ufufuko wa Yesu (Injili). Hayo mengine ni hadithi tu kama science fictions nyingine
 
Hoja zinazoibuka na kuhitaji majibu kutoka nje zipo nyingi na hushindwa kujibiwa na vitabu vyote vya dini, lakani za weza kujibiwa kwa kusoma vitabu vingine vya historia, kitu ambacho baadhi ya wanadini hawataki kukisikia japo ni vitu vyenye kuelezea dhana moja. Na ndio maana wafuasi wa dini zote hujikita kwenye kile walichorithi tu hata kama kina mapungufu kiasi gani. Na kwa sababu ya mapungufu ya kila upande yanayopeleke kukosekana kwa majibu ya maswali fulani fulani kila mmoja humuona mtu wa dini nyingine kama aliyepotea ilhali na yeye akiwa kwenye hali ileile.
 
Hebu tuwe watu wa tafakuri kidogo kipindi cha Yesu Buddha alikuwepo? Jibu ni HAPANA sasa inawezekana vipi awe mfuasi wa kitu kisichopo?
 
shida inakuja pale ambapo wafia dini wengi huwahawaukubali ukweli halisi na kubakia kuweka ubishi usio na hoja zenye mantiki zaidi ya maneno makavu au majibu yasiolingana na alichoulizwa.......DINI ni yako lakini wengi wetu hatuingii deeply kuzijua zaidi ya kuishia kukariri yale tuliokaririshwa na walimu na viongozi wa dini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…