????????
Je, historia imekuwa sio sahihi kwa miaka 2000—kulikuwa na Mrs. Yesu Kristo? In, “Kaburi la Familia ya Yesu,” mkurugenzi wa (makala ya Chaneli ya TV ya Discovery) Simcha Jacobovici anadai kuna “ushahidi” kwamba Yesu na Maria Magdalena walioana na walikuwa na mtoto aliyeitwa Yuda.
??????
Msomi wa Agano Jipya Norman Geisler anaandika “Maandiko ya Siri ya Wachache (Wanostiki) hayakuandikwa na mitume, bali na watu katika karne ya pili (na baadaye) wakijifanya kutumia mamlaka ya kitume kuendeleza mafundisho yao wenyewe. Leo tunaita suala hili uongo na uzushi wa kufoji.
????
Wazo kwamba Maria Magdalena alikuwa mtu maalum kwa Yesu inachukuliwa hasa kutoka Injili ya Maria. Injili hii ya Kinostiki (Kijuaji) si sehemu ya Agano Jipya, na iliandikwa na mtunzi asiyejulikana katika nusu ya karne ya pili, au karibia miaka mia na hamsini baada ya kifo cha Yesu. Hakuna mashahidi wa macho, akiwamo Maria mwenyewe wangekuwa hai wakati ilipoandikwa (karibia miaka 150 A. D.). Tarehe hiyo ya mwishoni inamaanisha Injili ya Maria haikuandikwa na shahidi wa macho wa Yesu, na hakuna anayejua aliyeiandika.
Machache tu kati ya mengi yanayochanganya