Kumbe Yesu alikua mfuasi wa Buddha

Kumbe Yesu alikua mfuasi wa Buddha

Nijuavyo alikuwa seremala kwa baba yake wa kufikia Yusufu/Joseph kabla hajaanza kuhubiri
 
Hebu tuwe watu wa tafakuri kidogo kipindi cha Yesu Buddha alikuwepo? Jibu ni HAPANA sasa inawezekana vipi awe mfuasi wa kitu kisichopo?
Buddha kazaliwa miaka zaidi ya 400 BC...hivyo ni sawa kabisa kusema labda Yesu alikuwa mfuasi wake
...anyway mimi ni mkristo ila with open mind
 
Buddha kazaliwa miaka zaidi ya 400 BC...hivyo ni sawa kabisa kusema labda Yesu alikuwa mfuasi wake
...anyway mimi ni mkristo ila with open mind
Nakubaliana nawe kwenye kuzaliwa lakini kwenye ufuasi hapana... Kwakuwa hawa walikuwa wa imani mbili tofauti kabisa Mungu vs miungu
 
Taarifa za miaka 16 ya yesu kabla ya miaka 3 ya kuhubiri injili hazipatikani kwenye biblia pia hakuna kumbukumbu hizo.Pana nadharia Mbili maandiko yanasema alisurubiwa akafa,akazikwa akafufuka akapaa mbiguni kwa ushuhuda wa wanafunzi wake.Nadharia ya pili ina amini aliyesurubiwa sie Yesu,baada ya kutaka kuuwawa na Mayahudi alifanikiwa kutoroka na kuelekea India maeneo ya Kashmir Jirani na Pakistani ambapo aliendelea na utumishi hadi alipofia huko akiwa na miaka 80 na kaburi lake lingali hata sasa,na watu wanaenda kuzuru huko.
Aiseee "" dunia kweli ina mambo ""...Inaonekana " huyu mtu " ana nadharia nyingi mnooo"" kiasi kwamba " kuna nyingine zimepotoshwa kwaajili ya manufaa ya watu"""
 
Hebu tuwe watu wa tafakuri kidogo kipindi cha Yesu Buddha alikuwepo? Jibu ni HAPANA sasa inawezekana vipi awe mfuasi wa kitu kisichopo?
Dini ya Buddha ilianzia huko India miaka 500 BC/KY kwa maisha na mafundisho ya Buddha aliyeitwa GAUTAMA (enlighten one) ikimaanisha aliyeona nuru. Kulingana na vyanzo vya kale MWANA MFALME GAUTAMA (?563-483 BC/KY) alizaliwa kwenye maisha ya starehe, lakini baada ya kumuona mzee mmoja, mgonjwa na mwili wa mtu aliyekufa aligundua kuwa na yeye pia kuna siku moja atakuwa mzee aliyeshindwa na kufa. Alipokutana na mtu mwingine aliyetafuta ufumbuzi wa mambo ya maisha ya kiimani, Gautama alihamasika kuondoka nyumbani ili kupata ukombozi kutoka katika mzunguko usioisha wa kuzaliwa kuishi na kufa kupitia Yoga au Meditation.

Baada ya kufanikiwa kukomboka na mzunguko wa kuzaliwa kuumwa na kuwa mzee kisha kufa kwa kuona nuru Nirvana Gautama aligeuka jiwe la msingi la mafundisho ya Kibuddha. Kupitia Gautama dini ya Budha ilianza kupata wafuasi wa mwanzo kabisa miaka 500 kabla ya wakati wetu wa kawaida na makazi yao Sangha yaligeuka kuwa makazi ya watawa wa Kibuddha.

Dini ya Buddha ilianza kuenea kutoka kiini chake kuelekea maeneo mbalimbali zama za Mfalme Mauryan Mkuu wa Ashoka (272-232 BC) Na iliendelea kusambaa kuelekea kusini na mashariki mwa Asia. Ambapo matawi mawili makuu yalitokeza, Theravada (Mafundisho ya wazee) likipatikana Sri Lanka, Cambodia, Thailand pamoja na mataifa mengine ya Asia kusini na Mahayana (Gari kubwa) likienea China, Korea, Japani na Tibeti.

Kwa kupitia hiyo historia fupi utaweza kuona dini ya Budha ilianza mapema kabla ya UKRISTO na UISLAMU.

Chanzo: The Guinness Concise Encyclopedia (1993), London: Guinness Publishing LTD pp 290-91
 
Hoja zinazoibuka na kuhitaji majibu kutoka nje zipo nyingi na hushindwa kujibiwa na vitabu vyote vya dini, lakani za weza kujibiwa kwa kusoma vitabu vingine vya historia, kitu ambacho baadhi ya wanadini hawataki kukisikia japo ni vitu vyenye kuelezea dhana moja. Na ndio maana wafuasi wa dini zote hujikita kwenye kile walichorithi tu hata kama kina mapungufu kiasi gani. Na kwa sababu ya mapungufu ya kila upande yanayopeleke kukosekana kwa majibu ya maswali fulani fulani kila mmoja humuona mtu wa dini nyingine kama aliyepotea ilhali na yeye akiwa kwenye hali ileile.
Umesema " vizuri sana """
 
mkuu hayo ni maoni yake mazuri.
Bibilia haina shida yoyote wala haimilikiwi na dhehebu lolote kubwa, labda kama anazungumzia Douay version au dada yake latin vulgate ambayo inamilikiwa na imani ya kikristo huko rumi.

Kuhusu Yesu kuwa mbudha, nizo ni counterfeits tu hakuna ukweli.
Ukweli ni kwamba thomas alihubiri injili kuhusu Yesu hadi india. Na yesu alijulikana toka miaka ya zamani sana huko india. ndiyo maana hata vasco da gama alipoingia india na convoy yake akiwa na baadhi ya wamisionari wa kirumi walishangaa kukutana na wakristo huko St Thomas christians ambao hawakuwa affiliated na kanisa lolote mashuhuri.
Hao wabudha wanashindwa nini kumuintergrate kwenye story zao ili kuchochea confusion?

Conterfeit ni nyingi.
Yesu sijui alioa.
Mara hakuwepo
mara hakufa msalabani
mara aliishi India.
Mara alikuwa muislam
mara alikuwa philosopher kama wakina plato
Mara hajaja yule aliyekuwepo ni msanii tu wa nazareti
Mara hakuwepo hicho kinachofundishwa ni miungu ya misri, ugiriki na babeli
Mara kuna mavitabu na magombo ya siri huko vatican vakifichuliwa watu wataduwaa kuhusu yesu.

Vyote hivyo na mbabaiko wote huu ni ushahidi Yesu Yupo, alikuja, akafa, akafufuka na anakuja upesi Kuwahukumu Walimwengu.
Machafuko dhidi ya uhalisia wa Yesu ni Maandalizi ya tukio kubwa linalouijia ulimwengu (Modern babylon):Ufunuo 18:1-4,
 
Dini ya Buddha ilianzia huko India miaka 500 BC/KY Kwa maisha na mafundisho ya Buddha aliyeitwa GAUTAMA ikimaanisha aliyeona nuru. Kulingana na vyanzo vya kale MWANA MFALME GAUTAMA (?563-483 BC/KY) alizaliwa kwenye starehe, lakini baada ya kumuona mzee mmoja, mgonjwa na mwili wa mtu aliyekufa alifundua kuwa na yeye pia kuna siku moja atakuwa mzee aliyeshindwa na kufa. Alipokutana na mtu mwingine aliyetafuta ufumbuzi wa mambo Gautama alihamasika kuondoka nyumbani ili kupata ukombozi kutoka katika mzunguko usioisha wa kuzaliwa kuishi na kufa kupitia Yoga au Meditation.

Baada ya kufanikiwa kukomboka na mzunguko wa kuzaliwa kuumwa na kuwa mzee kisha kufa kwa kuoata nuru Nirvana . Kupitia Gautama dini ya Budha ilianza kupata wafuasi wa mwanzo kabisa miaka 500 kabla ya wakati wetu wa kawaida na makazi yao Sangha yaligeuka kuwa makazi ya watawa wa Kibuddha.

Dini ya Buddha ilianza kuenea kutoka kiini chake kuelekea maeneo mbalimbali zama za Mfalme Mauryan Mkuu wa Ashoka (272-232 BC) Na iliendelea kusambaa kuelekea kusini na mashariki mwa Asia. Ambapo matawi mawili makuu yalitokeza, Theravada (Mafundisho ya wazee) likipatikana Sri Lanka, Cambodia, Thailand pamoja na mataifa mengine ya Asia kusini na Mahayana (Gari kubwa) likienea China, Korea, Japani na Tibeti.

Kwa kupitia hiyo historia fupi utaweza kuona dini ya Budha ilianza mapema kabla ya UKRISTO na UISLAMU.

Chanzo: The Guinness Concise Encyclopedia (1993), London: Guinness Publishing LTD pp 290-91
Kuja kwa kristo ulimwenguni kulijulikana kwa kalamu na midomo,hata kabla hajazaliwa.
ndio maana hadi leo tunawashangaa wayahudi walishindwaje kufahamu mambo ambayo majusi waarabu walisoma kwenye vitabu vyao wakaja kushuhudia hilo tukio.
Kuzaliwa, mahala atakapozaliwa, kazi atakayofanya, mateso atakayopitia, kufa na kufufuka, kufanya kazi zake karpenaumu pale, hata kuja kuhukumu ulimwenguni.
kuwambwa msalabani.
kinachotusumbua wengi humu nimeona ni humanistic and myopic view of Jesus.
hivyo hata kabla mababu na mababu wa kihindi hawajajitambua Yesu alijulikana na habari za unabii wake zilizagaa sehemu nyingi kwa sababu hapo jerusalem ilikuwa ni njia panda ya kibiashara na watu wa mataifa karibu yote walipita hapo na wengine walisoma habari za Mungu wa waebrania na utabiri wa mambo yao.

haya mambo yanahitaji unyenyekevu ili yatuelee. Yesu kaelezewa zaidi ya mara 400 kwenye maandishi ya agano la kale mamia kama sio maelfu ya miaka.
 
Nakubaliana nawe kwenye kuzaliwa lakini kwenye ufuasi hapana... Kwakuwa hawa walikuwa wa imani mbili tofauti kabisa Mungu vs miungu
@mshana jr hebu rudi kwenye swali lako la awali. lisome ili ujue ulichouliza na ukajibiwa.
 
Limeshapata ufafanuzi... Buddha alimtangulia Kristo ila Kristo hawezi kuwa mfuasi wa Buddha kwakuwa doctrine zao hazifanani kabisa
me nadhani hata hili pia utapata jibu lake kama ulivopata jibu la swali lako la kwanza.
maana ulisema ulimaanisha kipindi cha yesu budha hakuwepo. umepewa jibu mwafaka.
 
Limeshapata ufafanuzi... Buddha alimtangulia Kristo ila Kristo hawezi kuwa mfuasi wa Buddha kwakuwa doctrine zao hazifanani kabisa
kwa ufahamu wako je unayo taarifa au maelezo kutoka kwenye biblia yanayoelezea historia ya yesu kipindi hicho akiwa na umri 13 mpaka 29 alikuwa wapi? biblia inatuambiaje maelezo ya kutosha
 
Dini ya Buddha ilianzia huko India miaka 500 BC/KY Kwa maisha na mafundisho ya Buddha aliyeitwa GAUTAMA ikimaanisha aliyeona nuru. Kulingana na vyanzo vya kale MWANA MFALME GAUTAMA (?563-483 BC/KY) alizaliwa kwenye starehe, lakini baada ya kumuona mzee mmoja, mgonjwa na mwili wa mtu aliyekufa alifundua kuwa na yeye pia kuna siku moja atakuwa mzee aliyeshindwa na kufa. Alipokutana na mtu mwingine aliyetafuta ufumbuzi wa mambo Gautama alihamasika kuondoka nyumbani ili kupata ukombozi kutoka katika mzunguko usioisha wa kuzaliwa kuishi na kufa kupitia Yoga au Meditation.

Baada ya kufanikiwa kukomboka na mzunguko wa kuzaliwa kuumwa na kuwa mzee kisha kufa kwa kuoata nuru Nirvana . Kupitia Gautama dini ya Budha ilianza kupata wafuasi wa mwanzo kabisa miaka 500 kabla ya wakati wetu wa kawaida na makazi yao Sangha yaligeuka kuwa makazi ya watawa wa Kibuddha.

Dini ya Buddha ilianza kuenea kutoka kiini chake kuelekea maeneo mbalimbali zama za Mfalme Mauryan Mkuu wa Ashoka (272-232 BC) Na iliendelea kusambaa kuelekea kusini na mashariki mwa Asia. Ambapo matawi mawili makuu yalitokeza, Theravada (Mafundisho ya wazee) likipatikana Sri Lanka, Cambodia, Thailand pamoja na mataifa mengine ya Asia kusini na Mahayana (Gari kubwa) likienea China, Korea, Japani na Tibeti.

Kwa kupitia hiyo historia fupi utaweza kuona dini ya Budha ilianza mapema kabla ya UKRISTO na UISLAMU.

Chanzo: The Guinness Concise Encyclopedia (1993), London: Guinness Publishing LTD pp 290-91
mkuu umemsaidia vizuri sana bwana Mshana Jr. kikubwa anatakiwa awe mtafiti wa kufatilia badala ya kujifanya anajua kumbe hajui.
 
Taarifa za miaka 16 ya yesu kabla ya miaka 3 ya kuhubiri injili hazipatikani kwenye biblia pia hakuna kumbukumbu hizo.Pana nadharia Mbili maandiko yanasema alisurubiwa akafa,akazikwa akafufuka akapaa mbiguni kwa ushuhuda wa wanafunzi wake.Nadharia ya pili ina amini aliyesurubiwa sie Yesu,baada ya kutaka kuuwawa na Mayahudi alifanikiwa kutoroka na kuelekea India maeneo ya Kashmir Jirani na Pakistani ambapo aliendelea na utumishi hadi alipofia huko akiwa na miaka 80 na kaburi lake lingali hata sasa,na watu wanaenda kuzuru huko.
Makubwa haya
 
Teh teh yaani Yesu atoroke kuogopa kifo daah. Mkuu usipotoshe kua habar za utoto wa Yesu hazipatikani, sema yaliyomo kwenye biblia yaliwekwa kwa mahususi ya kukuza imani. Zaid ya Injili 20 ziliachwa zikapatikana 4 tu Luke,Mathew,Marko,John.
Hivyo waweza vuta picha ni habar nyingi kiasi gani ziliachwa
CC
Palantir
Mwinjili YOHANA anasema mambo mengi yangeandikwa sizani kama.ulimwengu huu ungetosha sehemu ya kuhifadhia vitabu vyake, wapinga KRISTO wapo kazini
 
Back
Top Bottom