Tusibishane mkuu; fanya hivi; Biblia za Kiarabu zipo na kama wewe ni Muislamu that much will make our debate easy kwasababu unaweza kusoma maandishi ya Kiarabu zaidi kuliko Wakristo wengi, tafuta kila sehemu yenye Biblia ya Kiswahili mahali palipo andikwa Yesu then angalia kwenye Kiarabu jina hilo limeandikwaje, hilo moja but la pili ni hili, siku za Jumapili jioni nadhani kuanzia saa 12 jioni, TV ya ATN hua ina kipindi cha Waarabu ambao ni Wakristo, hua wanaimba na kuzungumza mambo kadhaa kwa lugha yao, sikiliza NENO YESU wanatamkaje!? Angalizo, usisikilize Waarabu ambao ni Waislamu, sikiliza wale ambao ni Wakristo, nasema hivyo kwasababu Qu-raan (samahani kama nimekosea spelling) inatumia neon Issa badala ya YASU. Kuhusu NENO Biblia, hilo nakubaliana na wewe kwa 100% kwasababu hata ukifungua ndani ya maandiko yote ndani ya "Biblia" hutalikuta hilo NENO Biblia hata sehemu moja zaidi ya kwenye GAMBA lake tu; sababu ni hi (wengi wanapotosha sana kuhusu hilo). Mwanzoni kabisa, vitabu hivyo vilikua separate, yaani vilikua kimoja kimoja vinajitegemea, yaani Kitabu cha Mwanzo, Kutoka, Kumbukumbu la Torati, Mambo ya Walawi Hesabu na vyote hadi 66/72 vilikua vinajitegemea; yaani ni kamam hivi, ukitaka kununua kitabu cha KUTOKA then unakinunua hivyo kilivyo chenyewe tu na vingine ni hivyo hivyo, baadae hivyo vitabu 66 au 72 vikaunganishwa na kua kitabu kimoja, baada ya kufanya hivyo then waunganishaji wakajiuliza hili BUNDA la KITABU tuliiteje!? Ndio wakasema, well, tuite "MKUSANYIKO WA VITABU" now remember wakati huo lugha ya Kiyunani/Kigiriki ndio ilikua Kingereza cha wakati huu, yaani sehemu kubwa ya dunia kwa maana ya LUGHA ya kimataifa ilikua hiyo of course hata Agano lote JIPYA liliandikwa kwa LUGHA hiyo pia, kwa bahati moja hiyo sentensi ya "MKUSANYIKO WA VITABU" kwa Kiyunani wao lipo neno moja tu yaani Biblos, so huo mkusanyiko wa hivyo vitabu 66 au 72 ukaitwa Biblos then Waingereza wakaita Bible na sisi Waswahili tukaita Biblia, you can call it MAKTABA if you want.