#COVID19 Kumbe Zanzibar imepata Tsh 200 bilioni tu katika ule mkopo wa COVID tofauti na inavyoelezwa na Wanasiasa uchwara!

#COVID19 Kumbe Zanzibar imepata Tsh 200 bilioni tu katika ule mkopo wa COVID tofauti na inavyoelezwa na Wanasiasa uchwara!

Sasa Zanzibar peke yake bil.200, Dar Es Salaam yenye watu mil.6 imepata kiasi gani?

Kwa mahesabu ya kawaida Dar inatakiwa kupewa billion 700 kulingana na uwiano wa billion 200. Kwa watu million 1
 
Hicho kimkoa chenye watu milioni 2 kinakula bilioni 230! Yani sijui kwanini hakaendelei kama Hong-Kong. Hovyo kabisa!

Hiyo wilaya haizidi watu million moja kulingana na takwimu rasmi hivyo wamepewa hela nyingi sana
 
Kwa mahesabu ya kawaida Dar inatakiwa kupewa billion 700 kulingana na uwiano wa billion 200. Kwa watu million 1
Job Ndugai alikuepo na haja ya kuona mkopo hauna Faida yeyote Ile kwasababu pesa nyingi zimepelekwa Zanzibar. Kwanini wapinzani wa sasa wanashindwa kuwa jasiri kama marehemu Mch Christopher Mtikila alivyokuwa anazungumzia haya masuala ya jinsi Tanganyika inavyoinufaisha Zanzibar

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo pesa ni nyingi sana

Dar es salaam ina watu wengi kuliko Zanzibar lakini hawajapewa hicho kiasi
Sio Dar es Salaam, wilaya tu moja ya Dar.

Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni, population 1.9 million, kuna watu wengi kuliko Zanzibar.

Wazanzibari wakipewa wagawane, hawawezi kujaza mashamba, nyumba, vyumba na viwanja vya Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni kwa sababu hawatimu 1.9 milioni people.

Tunawezaje kugawana maslahi sawa na ki tarafa kimoja tunakiita nchi ?

Nyerere alituuza kama nguruwe kuwatumikia Wazanzibar.
 
Bil 200!? Watuambie na wao wamejenga madarasa mangapi!? Usikute hawana uhitaji huo ila hela zimetumika tu.
 
Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr Sada Mkuya amesema wamepokea dolla milioni 100 za kimarekani sawa na tsh billion 200 na ushee ambazo zitatumika kuimarisha miundombinu.

Dr Mkuya amesema watajenga madarasa na hospitali katika wilaya zote Unguja na Pemba.

Mapinduzi Daima!
Mbona ndege zilizo agizwa na serikali mbili zimegaiwa zanzibar zitakuwa mali ya wazenji au ujui,
 
Kati ya Madeni yote aliyokopa karibu (Trillioni kumi) SSH ni alisimia ngapi zimeenda Zanzibar?

Kero za Muungano zimeondolowe,nyingi zimeisha, zimepunguzwa sana tunaambiwa.

Kwa makubaliano yapi, yalikuwa kati ya Wazenji wawili? Nini walikubaliana, tuwekewe wazi hivi vitu?
 
Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr Sada Mkuya amesema wamepokea dolla milioni 100 za kimarekani sawa na tsh billion 200 na ushee ambazo zitatumika kuimarisha miundombinu.

Dr Mkuya amesema watajenga madarasa na hospitali katika wilaya zote Unguja na Pemba.

Mapinduzi Daima!
Ngoja nikupe hesabu.

Jumla ya mkopo 1.3trillioni

Hizi ni sawa na 1,300billioni
Nusu ya hizi imetumika kulipa mkopo

Unabaki na bilioni 650
Toa bilioni 200 za zenji unabaki na bilioni 450.

Kwa hiyo zanzibar wamepata bilioni 200 na ushee.
Bara tumepata bilioni kama 400 hivi.
Hapa ni sawa kweli?
 
Kwa hiyo ujinga wa chato unafanya huu ujinga ndio uonekane ni ujinga mzuri?
Nani kakwambia kuwa njiwa anaishi kiota kimoja na shorwe?

Ndege wa rangi moja daima uishi pamoja.
 
Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr Sada Mkuya amesema wamepokea dolla milioni 100 za kimarekani sawa na tsh billion 200 na ushee ambazo zitatumika kuimarisha miundombinu.
Ina maana watu walifahamu tofauti wakati hilo suala lilikuwa ni public knowledge since day one? Na walidanganywa ZNZ walipewa kiasi gani?
 
Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr Sada Mkuya amesema wamepokea dolla milioni 100 za kimarekani sawa na tsh billion 200 na ushee ambazo zitatumika kuimarisha miundombinu.

Dr Mkuya amesema watajenga madarasa na hospitali katika wilaya zote Unguja na Pemba.

Mapinduzi Daima!
Mgawanyo wa mikopo mingine ambayo ilichukuliwa na JMT ilikuwaje?
Je! Kulikuwa na uwazi wowote katika kufanya hivyo?

Endapo kama upande Tanganyika umenufaika mno kwa kipindi cha miaka iendayo 58 ya uwepo wa JMT, Zanzibar nayo inapaswa kuanza kufanya hivyo sasa. Kwani tulipoingia kwenye huu muungano hatukujua kuwa Zanzibar ina watu wachache?

Bila kujali ina watu wangapi, Zanzibar ina hadhi yake ya asili ya kuwa nchi hata kama ipo ndani ya JMT, na pia haijawahi kupoteza hadhi yake ndani ya katiba. Ni mawazo finyu kuongelea uwiano wa mgawanyo wa mkopo husika bila ya kuangalia mgawanyo wa mikopo mingine iliyokwisha kutolewa hapo awali kwa JMT.

Hebu tufanye tathimini ya haraka haraka kuhusu jinsi nchi hizi mbili zimefaidika kwa miundombinu kupitia mikopo iliyotolewa kwa idhini ya JMT na kulifikisha deni la taifa kufikia kiasi chaTZS 75Tn.

Tanganyika wala haipo, haishi na wala haina hadhi ya kukopa yenyewe kwa jina lake. Hivyo basi mkopo wowote ule unaochukuliwa ili uinufaishe Tanzania Bara peke yake ni lazima uchukuliwe kwa jina la JMT. Zanzibar nayo kama nchi inayoishi na yenye kutambulika inaweza kukopa kwa kupitia jina lake, na pia inastahiki zake kwa kile chote kinachokopwa kwa jina la JMT.

Ndiyo maana watu wenye akili wanaona kuna haja ya kufanya mabadiliko ndani ya katiba mpya ambapo muundo wa JMT utafanyiwa mabadiliko. Kuna kila haja ya katiba kutambua uwepo wa serikali tatu ndani ya huu muungano, kwa mantiki hiyo kuna haja ya kuifufua hadhi ya nchi ya Tanganyika ndani ya muungano wetu na kutenganisha shughuli zake za serikali na iwe pia na bunge lake kama ilivyokuwa kwa Baraza la Wawakilishi kule upande wa wenzetu wa nchi ile ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom