Uchaguzi 2020 Kumbuka: Karatasi za kupigia kura zitakuwa na picha ya Bernard Membe kama Mgombea Urais wa ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Kumbuka: Karatasi za kupigia kura zitakuwa na picha ya Bernard Membe kama Mgombea Urais wa ACT Wazalendo

Hiyo inajulikana mapema na tume walishasema ,kwahiyo hamna kipya ACT walishaamua kuunga mkono chadema ndo maana mgombea wao urais hafanyi kampeni
Kuna wapenzi wake watampa kura na wale wasiokubaliana na huo uamuzi wa kumuengua mtu wao waliyempitisha vikao vya ACT wazalendo vya kamati kuu na mkutano mkuu

Hayo makubaliano ni ya viongozi sio wanachama wa ACT wazalendo
 
kuteuliwa kisha usishiriki kinyangannyiro imekaaje kisheria?
Hivi kama Membe atahama chama kwa sasa na kujiuynga Chadema anaweza kumsaidia Lisu kwenye kampeni?
Je kuhama kwake kutahisabiwa je na Tume au Msajili wa Vyama vya Sisa?
 
Mleta mada ana point ya msingi sana. Kama watu wasipopewa elimu ya kutosha, kuna kura nyingi zitapotea kwa sababu ya watu kumpigia kura Membe kisa wameiona sura yake kwenye karatasi ya kupigia kura.

Lakini pia haya mambo yasichukuliwe kimzaa, itakuwaje endapo membe atapata kura nyingi kuliko wagombea wote wa urais, je atakataa kuapishwa kisa alimuunga mkono Tundu Lissu?
 
kuteuliwa kisha usishiriki kinyangannyiro imekaaje kisheria?
Hivi kama Membe atahama chama kwa sasa na kujiuynga Chadema anaweza kumsaidia Lisu kwenye kampeni?
Je kuhama kwake kutahisabiwa je na Tume au Msajili wa Vyama vya Sisa?
Kwa sasa hawezi kuhama chama ila anaruhusiwa kujitoa kugombea au kutofanya kampeni.
 
Kama ni hivyo na ambao rufaa zao zinakubalika inakuaje
 
Back
Top Bottom