KUMBUKIZI | Diamond Platnumz: Ukinifungia nyimbo, mimi hakunipunguzii Kitu, nita-perform Nchi nyingine

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz wakati akihojiwa na Kituo cha Redio cha Times FM mwaka 2017 alionyesha kusikitishwa na kitendo cha BASATA kufungia nyimbo zake kwa kisingizio kuwa hazina maadili.

"Mkinifungia nyimbo hainipunguzii kitu. Nyimbo ikiwa imefungiwa naenda nayo nje nitai-perform tu. Nikiona hutaki ni-perform si naondoka nakaa nchi nyingine tu. Nabaki huko na-perform nyimbo zangu. Kwa sababu sheria inakataza nyimbo haichezwi Tanzania. Tamaduni za Kenya zinaruhusu, wewe unakataza nisi-perform kwa sababu gani? Kwa nini nisi-perform sasa? Unataka mimi nife na njaa? Unanilisha wewe? Tiffah utamnunulia pampers? Utanisaidia katika kulisha familia yangu? Unajua mimi nahangaika vipi? Kwa hiyo kukaa na kuona kwamba tunafanya kitu gani. Tuzungumze."

Akadokeza kuwa ikiwa hali hii anayokumbana nayo itaendelea, itabidi tu ahame nchi ambapo atakuwa huru kufanya sanaa yake bila bughudha wala kuingiliwa na mtu yeyote.

Your browser is not able to display this video.


Your browser is not able to display this video.


MAONI YANGU

Mimi namuunga mkono Bwana Diamond. Kama akiona Tanzania hawamuelewi, bora tu ahamie nchi nyingine, isiwe shida. Nabii hakubaliki kwao.
 
Ahame au arudi kwao kwani ni Mtanzania huyu?
 
Diamond mafii ya bata
 
eti mwanzilishi wa nini?
 
Akihama tu muziki wa bongofleva unakufa.
Hatuwezi kufa. Kabla hata diamond hajazaliwa tulikuwa na wasanii kibao na waliokonga nyoyo zetu, akina Marijani Rajabu, Mbaraka Mwinshehe, Ubi Ukwe Zawosa, na wengine akina Maalim Gurumo.

Dogo diamond asitake kupima kina cha maji ya bahari kwa dole lake bhana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…