KUMBUKIZI: Mada maalum ya kumuenzi Munga Tehnan na kazi zake

***** yale mafuriko ya 2018 sitokaa niyasahau maishani. Yalipoteza kumbukumbu zangu nyingi sana... Nimemwachia Maulana
[emoji872][emoji848][emoji3064][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Gazeti lake lilikua linatoka j4 na alhamisi ,miongoni mwa vitu muhimu sana kwangu kipindi iko ni Gazeti la jitambue .
Jambo kubwa kupita yooooote nilijifunza kupitia makala ni hiii.
JE UNAJUA KUA NA WANAUME WANA SIKU ŹAO KAMA WANAWAKE ,ISIPOKUA HAWANA HADHI.
Zilipokuwa ofisi za Jitambue Ubungo Kibo kituo cha BoschView attachment 1724008
 
Kumbee..

Nami niliwahi kuandika pia Hata wanaume huingia period
 
Kazi zake Munga

Ili kufanikiwa kwenye lengo lolote katika maisha, ni lazima uamini kwamba utafanikiwa. Kama usipofanya hivyo, una nafasi kubwa ya kushindwa.
Unaweza kuwa na malengo mapya uliyoyapanga na ambayo unaanza kujaribu kuyatekeleza. Lakini ni lazima ufanye hivyo ukiwa na imani kubwa kwamba utafanikiwa.
Waweza kuona kazi uliyo nayo hivi sasa haikusaidii sana na hivyo kuamua ghafla kuiacha.
Waweza kufanya hivyo huku ukiwa hujaamua kitu gani cha kufanya, na hivyo kulazimika kutumia kipindi cha pengine miezi sita ama hata zaidi inayofuata kujaribu kufikiria nini cha kufanya.

Huwezi kufanikiwa katika kile unachokitaka kufanya ikiwa hutaamua kuyafanya mawazo yako hayo uliyonayo kuwa vitendo. Hata ukiwa na kiu na hamu kubwa kiasi gani ya kufanikiwa, bila kuhamasisha nafsi yako na kuanza kufuatilia lile unalotaka kulifanya, kufanikiwa itakuwa ndoto kwako. Hilo litashusha ari yako na kujikuta unarudi kulekule ulikotoka, kwenye kazi ya kuajiriwa.
Lakini wakati wote huu, vyanzo vya mafanikio huwepo karibu nawe tayari kutumiwa nawe kwa ajili ya kukuletea mafanikio unayoyataka. Lakini bila kuiamini nafsi yako kwamba unaweza kufanikiwa, huwezi kufanikiwa.

Hivyo ni lazima ujifikirie katika mambo unayoyafanya, unafanya mambo yako yanayokuelekeza kwenye malengo yako ukiwa na imani kwamba utafanikiwa. Je, unayo picha ya mafanikio yako akilini mwako na hisia kwamba hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa?
Hebu kaa chini na ufikirie kuhusu mambo uliyowahi kuyafanya na ukashindwa katika kipindi cha miaka michache iliyopita. Jiulize ikiwa kweli ulijiamini kwa dhati kwamba utafanikiwa.

Mara nyingi utakuta katika matukio hayo ulikuwa na mashaka ndani yako kuhusiana na uwezo wako wa kufanikiwa na hivyo iko haja ya kujihamasisha kabla ya kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye lengo lako. Unatakiwa kuamini kwamba utafanikiwa.
Ni kwa nini imani hiyo ni muhimu kiasi hicho? Kwa kawaida huwa tunaanza kujenga imani tangu tukiwa wadogo. Mara baada ya kuzaliwa kwetu, huanza kujenga au kujengewa imani.
Na baadaye tunaendelea kujijengea imani wakati tukiendelea kukua na huwa tunabadili imani kutoka za zamani na kujenga mpya, kutegemea vitu vingi. Tunahitaji kufanya haya ili kuyafanya maisha yetu hapa duniani yawe rahisi na ya kweli.

Siku zote tunaamini kwamba tunapoamka vitandani mwetu asubuhi, tunahitajika kuweka miguu yetu chini ili kuweza kusimama ardhini kabla ya kuendelea na shughuli zetu nyingine na si kuruka hewani hadi kwenye dari ili kuweza kutoka vyumbani mwetu kwa shughuli zetu za kawaida.
Tumejifunza hili tangu tukiwa wadogo kabisa na sasa hatuna haja hata ya kufikiria kila siku kwamba hivyo ndivyo tunavyotakiwa kufanya. Vivyo hivyo, pia hatuna haja ya kufikiria ni kwa kiasi gani nguvu ya uvutano ina mchango gani katika kusimama kwetu kila asubuhi tangu tunapoamka vitandani mwetu.
Wakati unapofungua mlango wa nyumba yako, unageuza ufunguo wako kuelekea upande uliko ubao wa kufungia mlango ama upande wa tofauti na mwenendo wa mikono ya saa.
Hiyo ni imani tunayojijengea tangu tukiwa watoto wadogo kabisa, tunapoanza kujifunza kufungua na kufunga milango.

Kila unapokutana na mlango mpya hatuwi na wasiwasi kwamba tunajua vile mlango unavyofunguka kwani tunakuwa na hakika (akilini mwetu) na namna mlango huo utakavyofunguka. Tunazunguusha funguo kuelekea upande uliko mlango tu! Ni rahisi. Hiyo ndiyo imani tuliyonayo.
Huoni sababu ya kufikiria uwezekano wa kukutana na mlango unaofunguka vinginevyo. Lakini hakuna atakayekataa kwamba wengi tumewahi kukutana na milango inayofunguka kwa mwelekeo tofauti na ule tunaoamini ndio utaratibu ‘unaokubalika.’ Inaudhi sana unapokutana nao kwa mara ya kwanza.

Hata baada ya mwaka mzima wa kufungua mlango kwa mwelekeo huo, bado imani uliyojijengea kutokana na uzoefu wako kwamba mlango haufunguki kwa mwelekeo huo, utakuwa nayo, na hivyo utakuwa ukikasirika kila mara utakapofungua mlango huo. Imani unayojijengea moja kwa moja huathiri tabia yako, hata kama imani hiyo si sahihi kama unavyofikiria.
Hebu tufikirie kitu kingine! Dunia ni duara ama si duara? Umelijuaje hili? Si kwamba umeambiwa na watu tu? Una uhakika gani? Wapo wanaoamini kwamba dunia ni ya ubapa kutokana na wanavyoiona kila wanapochungulia madirishani.
Kama ungeamini kwamba dunia ni ya ubapa, ni wazi ungepatwa na wasiwasi mkubwa wakati unaposafiri kwenye mashua kwamba huenda mngefika mwisho na kuangukia nje ya dunia.

Lakini hivi ndivyo watu walivyokuwa wakifikiria. Kilikuwa ni kikwazo kikubwa kwa ugunduzi kwa miaka mingi ya mwanzoni. Imani waliyokuwa nayo watu moja kwa moja iliathiri vitendo vyao, na hilo lilikwaza matokeo yao.
Fahamu tena kwamba imani si lazima zioneshe ukweli uliopo duniani. Si kila siku milango hufunguliwa kuelekea mwelekeo uliko mlango.
Imani kuhusu dunia kuwa ubapa ilibadilishwa mara wagunduzi walipoanza kuzunguuka dunia. Imani huathiri moja kwa moja matendo yetu hata hivyo. Wakati mwingine, tunachukua hatua hata imani zetu zinapokuwa si sahihi, na hii yaweza kutukwaza. Hii ni kweli kuhusiana na imani tulizonazo kuhusu nafsi zetu na uwezo wetu.

Vipi kuhusu nafsi zetu? Kama tufanyavyo mambo tuliyoyazoea bila kufikiria kutokana na imani tunazojijengea kama vile kufungua mlango, tunafanya hivyo hivyo kutokana na imani tunazojijengea kuhusu nafsi zetu.
Ikiwa tutajenga imani za kutukwaza kuhusiana na nini kinawezekana kufanikisha, jibu letu litakuwa kukwamisha matokeo ya vitendo vyetu tunavyochukua. Matokeo yake tunakwaza pia matokeo tunayoyapata.

Ikiwa tunaamini kwamba kuna kila uwezekano wa kushindwa katika kile tunachofanyamawazo yetu ya kina (subconscious mind), itafanya kazi ya kujenga mazingira yatakayounga mkono imani yetu hii. Wakati mambo yanapokuwa magumu, hatutakuwa na haja ya kufanya jitihada zaidi iliyo muhimu katika kufanikiwa; kushindwa kwa mara ya kwanza kutaunga mkono imani yetu hiyo na hivyo kutufanya tukate tamaa na kuachana na kile tunachofanya.

Kwa upande mwingine, ikiwa tutaamini kwamba tutafaulu, ni lazima tutafaulu. Mohamed Ali aliyekuwa akifahamika kama mwanamichezo aliyefanikiwa kushinda wote waliowahi kutokea duniani, mbali ya ari aliyokuwa nayo, kipaji na nguvu zake, moja ya sababu kuu zilizomsadia kufanikiwa na kuwa maarufu kiasi alichokuwa ni kwamba alikuwa na imani nzito kuhusiana na kila alichotaka kufanya.

Wengi tumewahi kuona picha zake za televisheni wakati akiwa ulingoni, alipokuwa akidai kwamba yeye ndiye bondia bora kushinda wote waliowahi kutokea duniani. Wakati alipokuwa akiieleza dunia hivi, ni kweli alikuwa bondia bora kushinda wote duniani? Wakati ule hakuwa hivyo, kwani alikuwa bado ana mambo ya kuionesha dunia ili kuthibitisha hilo. Alichokuwa nacho hata hivyo ni kujiamini moja kwa moja katika uwezo wake. Imani hiyo ilithibitishwa na matokeo aliyoyapata licha ya kuvuliwa mkanda wake wa dunia mwaka 1967, baada ya kukataa kwenda kupigana vita Vietnam akiwa askari wa jeshi la Marekani, hakukata tamaa.

Alirudi tena miaka saba baadaye na kushinda ubingwa huo alioendelea kukaa nao kwa miaka minne zaidi. Imani yake kwamba yeye ndiye bora kuliko wote waliowahi kutokea duniani, si kwamba ilimsaidia kufikia kiwango cha juu cha masumbwi, bali kiwango cha juu cha michezo kwa

Credit kwake Mtambuzi
 
Nalikumbuka sana hili gazeti la jitambue.
Nilikuwa msomaji mkubwa wa gazeti hili.
Mimi nilikuwa napenda zile simulizi zake ambazo Mtambuzi alikuwa anatuwekea humu.
Afu kama sijakosea kulikuwa na ukurasa wa yale mambo ya ajabu yanayotokea...na moja ambalo nakumbuka mpaka leo ni jinsi baba mmoja alipoamka asubuhi na kukuta bati lake lina taswira ya Yesu...yaani limejikunja na kuweka taswira hiyo.
Kingine ni ule mti uliojichora sanamu ya bikira maria n.k

Story ya yule mtoto aliyepata ajali na kupoteza wazazi wake, zote nilisoma kwenye gazeti la jitambue enzi hizo za Y2K
 
Kumbe huwa wewe kaongokaongo, hakujawahi kuwa na safu yenye jina hilo, labda unamaanisha "Jinsi nilivyofedheheka"
 
Huyu jamaa, nilifanya nae kazi pale Business Times,tukiandaa magazeti ya S
 
Huyu jamaa tulifanya nae kazi pale Business Times mwishoni mwa miaka ya Tisinina mwanzoni mwa miaka ya elfu elfu mbili. Jamaa huyu alikuwa ndiye masters wa kuandika habari zote pale Business Times. Yaan alikuwa kama mhariri mkuu kwani, wahariri wote, wakiwemo wakuu alikuwa anawafundisha kazi bila kinyongo. Ingawa hawakumpa cheo cha uhariri mkuu. Kwa ufupi jamaa huyu alikuwa anajua sana. Alikuwa anahariri gazeti la majira, gazeti la Sanifu, Dar Leo na mengine ya ile kampuni. Wakati huo mm nilikuwa najifunza kazi ya kuandika habari. Tulikuwa na watu wengi pale:Juma Pinto, John Mapinduzi, Masod Kipanya, Amina Chifupa, Maboure Martinyi. Na wengine wengi tu. Nakumbuka alipoacha kazi Business Times, alinambia hivi. Naacha kazi hapa Business Times, nakwenda kuanzisha kampuni yangu na gazeti langu. Sitarudi tena hapa Business Times. Nikirudi hapa tena, kuomba kazi, nitageuka kuwa jiwe. Maneno hayo alisema, tukiwa tumesimama nje ya ofisi za Business Times kwenye magari, mwaka 1999.Kutoka muda huo alianzisha gazeti la Jitambue na pia alitunga vitabu vya meditation.
Mshana hilo gazeti la mwaka gani???

Kingsmann

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa mapenzi mkubwa sana wa gazeti la Jitambue. Sikuwahi kosa nakala ya gazeti lile kila Jumatano kama sikosei. Nilishawahi andika makala kwenye nakala mojawapo ya gazeti lile. Nitapitia mails zangu nione kama nitapata kopi ya nilichomtumia Munga (RIP) nikiweke humu
 
Yaani kama ni chai, basi niliinywa haswa... ahahahaa
 
Umenikumbusha mbali. Magazeti yake nimeyasoma sana yalikuwa na mambo mazuri. Vipindi vyake vya televisheni nilikuwa sikosi kutazama. Niliumia sana niliposikia kafariki. Rip Munga
 
Alianza kwenye gazeti la Cheche. Kuna gazeti jingine la Baraza kulikuwa na waandishi akina Sultan Tamba nao waliandika masuala magumu sana Mshana Jr naomba utafungua uzi mwingine kuwahusu hao.

Sent from my N20 using JamiiForums mobile app
Yeah huyo Sultan Tamba alikuwa rafiki yangu sana, wakati huo akiwa Global Publishers, akaandika simulizi za kuvutia kupitia gazeti la UWAZI, wakati huo likiuzwa sh.100, Maslahi ndio yaliyomtoa huko
 
Story ya yule mtoto aliyepata ajali na kupoteza wazazi wake, zote nilisoma kwenye gazeti la jitambue enzi hizo za Y2K...!

Hiyo story mpaka leo inanisisimua damu, tuliwahi ijadili hapa na ile ya yule kibaka wa Temeke
 
Umenikumbusha mbali. Magazeti yake nimeyasoma sana yalikuwa na mambo mazuri. Vipindi vyake vya televisheni nilikuwa sikosi kutazama. Niliumia sana niliposikia kafariki. Rip Munga
Alikuwa na vipindi kila week TVT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…