Hapa nakuweka sawa kidogo. Kwenye Uislamu kuna taratibu za ufanyaji wa kila jambo.
Ni makosa kuweka uhusiano wa ibada ya Hija na kaburi la Mtume. Mitume huzikwa pale wanapofia, yaani sehemu ambayo amekufa mwili unasogezwa mwili kaburi linachimbwa anazikwa. Imekuwa hivyo sababu kihistoria mtume alifia kwenye nyumba, kaburi likachimbwa hapo hapo akazikwa, msikiti wa Makka, kutokana kutanuliwa kwake Kaburi likaingia ndani ya Msikiti.
Kadhalika kiislamu haifai kusafirisha maiti, sababu ardhi yote ni ya Mola, na tunacho usiwa sisi Waislamu kabla ya kufa, tuwe tumeandika usia wa kuwasihi watu ukifa wakuzike kama alivyofundisha Mtume, huu ndiyo utaratibu wetu na hili ni jambo la wajibu.