KUMBUKIZI: Mada maalum ya kumuenzi Munga Tehnan na kazi zake

Nilikuwa mapenzi mkubwa sana wa gazeti la Jitambue. Sikuwahi kosa nakala ya gazeti lile kila Jumatano kama sikosei. Nilishawahi andika makala kwenye nakala mojawapo ya gazeti lile. Nitapitia mails zangu nione kama nitapata kopi ya nilichomtumia Munga (RIP) nikiweke humu
[emoji1545][emoji1545][emoji1545] Sikubahatika kuandika kwenye magazeti yake , nilikuwa naandikia Mtanzania safu ya SHUSHA PUMZI kila Jumamosi
 
Jinsi nivyofedheheka: nikaropoka kichizi bachela ofu masta"

Naomba na mimi niwasaidie ndugu na jamaa zangu ambao hawajipendi.Nimejifunza kujipenda na kujipenda ni kujikubali mtu ulivyo.

Nakumbuka vizuri sana ilikuwa mwaka 1996,wakati huo nikiwa nafanya kibarua kwenye stationary moja jijini Dar as salaam.Nilikuwa nimemaliza kidato cha nne miaka miwili nyuma.Sasa kulikuwa na mkaka mmoja aliyekuwa anakuja pale dukani mara kwa mara.Huyu mkaka kwakweli nilimpenda siku ya kwanza tu nilipomuona.Nilikuwa najua ameoa,lakini nikashindwa kuvumilia kuendelea kumpenda.Kumbe nayeye akawa amenipenda.Basi,siku moja akanitania kama ningeweza kupata naye chakula cha mchana.Nilikubali utafikiri nilikuwa sijala kwa miaka kadhaa[emoji1]

Tulikutana chakula cha mchana na kuzungumza kuhusu vitu vya kawaida vya kimaisha.Tuliendelea kuwasiliana hadi siku aliponiomba tena tukutane kwa chakula cha jioni.Nilijifanya kuzuga kwamba nyumbani wata "maindi"lakini kesho yake nilimjibu inawezakana.Basi tulikubaliana tukutane J'mosi kwa chakula cha usiku.Siku hiyo hakuja pekeake Bali alikuwa na mwanaume mwingine na msichana ambaye alikuwa ni mchumba wa huyo mwanaume mwingine ambaye alikuwa ni rafiki yake sanaa.Tulikwenda hotel ambayo naomba nisiitaje lakini ya nyota 3.Wakati huo nilikuwa sijui hata kama hotel nazo sina sifa ya nyota[emoji4]

Yule jamaa yangu alinambia,huyo rafiki yake na mchumbake walikuja pale ili kula pamoja,halafu wangeondoka na kutupa nafasi ya kuzungumza.Niliona sio vibaya lakini ilinikera kwasababu niliona alitaka wale wanitathmini[emoji20]Basi jamaa yangu alinitambulisha kwao,niliwasalimu na tukaenda mezani,.kwakweli nilikuwa sijawahi kuingia hoteli kubwa hata siku moja....

ILILETWA menu na nilichagua kitu ambacho sikuwa nakijua[emoji85]Ilikuwa supu ya boga,afadhali. KUMBE;ilikuwa kwanza ni supu kabla ya chakula na kila mmoja pale aliagiza supu yake,lakini wenzangu wakiwa wanajua wanafanya nini..wakati tunakunywa supu yule rafiki wa jamaa yangu aliniuliza nilikuwa nimesoma wapi.Yeye alikuwa na maana ya shule au mkoa.Mimi kwasababu niliwasikia wakitia maneno ya kiingereza kila mara,niliona nijikweze kidogo.'Nilimaliza Mlimani.'.nilijikuta nikisema,.walishangaa wote[emoji44]Mwaka gani??Yule jamaa aliuliza kwa shauku.

Nilijua nimejibana mwenyewe kwa kutaka kujionesha.'Mwaka Jana.' Wote waliacha kunywa supu zao,.pengine wakijiuliza ilikuwaje hawakuniuliza swali hilo mapema.Yule jamaa yangu alionesha kushtuka zaidi. 'Ulikuwa unachukua nini?' Yuleyule tena aliuliza,.kiherehere tuu!![emoji57]Tangu nizaliwe nilikuwa sijawahi kukutana na mtihani kama ule.Nilifikiri harakaharaka."BACHELA OFU MASTA" nilisema kwa kujiamini[emoji6]Walishangaa zaidi na walijua nimekosea,walijua labda nilitaka kusema,Bachela ofu sayansi..Unajua,kwasababu ya matarajio makubwa mtu anaweza kudhani yeye ndiye kakosea.Labda walidhani wao ndiyo hawajasikia..

'Ulikuwa hostel au ofu kampasi' Yule mwanamke mwenzangu nae alishikwa na kiherehere,.Sikujua hata anauliza kitu gani na nilijilaumu kwasababu nilidhani wale jamaa pale walikuja wamemaliza kidato cha 6 au cha 4 kama changu,hivyo nilitaka KUWAKOGA....'hostel' nilisema nikiwa nimeshupaa utafikiri naapishwa kuwa rais wa nchi..'Ya wapi??' Yule mwanamke aliuliza tena(cha umbea) sikuwa najua hata hizo hostel ziko wapi,.Lakini nakumbuka niliwahi kusikia Mabibo hostel..Nikasema 'Mabibo'...'Digrii yako ulispesholaizi nini?? Hapo safari ikafika mwisho kama ni reli basi ikawa ni Kigoma.Nilifikiri kwa muda kabla sijasema 'kwani nyie mnataka nini hasa,sijafika chuo kikuu nilikuwa natania tuu.Mimi elimu yangu ni kidato cha nne' nilisema na wote wakaangua kicheko hadi wateja wengine wakavunja shingo kuangalia. 'Nilistuka Ile bachela ofu masta,du!!' Yule jamaa yangu alisema.

MWISHO;hivi sasa yule jamaa ndiye mume wangu na Mimi nasoma chuo cha biashara nikichukua diploma.Tuna watoto wawili.....Nataka kusema hivi,ukijikataa ni lazima utaadhirika..kuwa wewe haitakudhuru mwenzangu'[emoji108][emoji108]

NB:hii ni stori ya kweli iliandikwa kwenye gazeti JITAMBUE la July 13-19 mwaka 2005 chini ya Munga Tehenani(rip)
 
Jinsi nilivyofedheheka: Ikawa mwisho wa UKUWADI wangu

Nilikuwa kijana niliyehitimu kidato cha nne mwaka 1990. Baada ya kusota bila kazi kwa miaka mitatu(3),nilikuja kupata kwenye kampuni moja ya Wahindi jijini Dar.
Katika kampuni hiyo,palitokea mtoto wa bosi mwenye kampuni kunipenda na kuelekea kunizoeazoea.

Wakati wafanyakazi wenzangu wa Kiswahili wanatoka yeye alipenda kuniambia nibaki,huku akisema kama nina haraka basi naweza kwenda. Nami kwa woga wa kuwazoea mabosi,naondoka.

Siku moja aliniambia nibaki,la kushangaza silijui hata ni kwanini safari hii sikukataa. Baadaye,tulikaa ofisini hadi takribani saa 12 jioni,ndipo nilimsaidia kufunga ofisi. Akanituma nikachukue taxi maana aliniomba nikamsindikize mahali.

Baada ya kupanda kwenye taxi ile,akamwambia dereva kuelekea Tandika. Nikajawa na mshangao,bosi wa kihindi anatafuta nini Tandika? Naona alinielewa,akawa anasema,"..hapana sema juu ya hii safari..mi mependa veve rafiki yangu,tunza siri..."

Tulifika mahali penye kituo cha mafuta,akamwambia dereva atafute pa kupaki. Haikuchukua muda mrefu,akatokea dada mmoja ninayemfahamu,akafika na kumpa mkono,akachungulia zaidi ndani ya gari,akaniona,alinisalimia ingawa hakufurahia kuniona.
Yule dada anafanya kazi kampuni nyingine kama mesenja,na huwa anakuja pale ofisini kwetu kwa kukabidhi na kupeleka vifurushi.Ukweli ni kwamba dada yule hata kama ni mapenzi,hakuwa wa kutembea na kijana yule wa kihindi. Hakuwa na mvuto hata kidogo!

Tulikaa kwenye baa moja ya jirani na kuagiza vinywaji baridi. Mpaka muda ule sikuwa nimeelewa maana ya kuniita pale. Baadaye walinong'onezana na walipomaliza,yule bosi akatoa noti kama kumi hivi akampatia dada yule.
Wakati wa kurudi alinipa kama sh 5,000/-

Kesho yake akaniomba nibaki tena.
Nilibaki,na akaniambia yeye anapenda wasichana wazuri wa Kiswahili. Na yupo tayari kugharamia matumizi hadi ampate. Kwa hiyo akanielekeza kwa dada mmoja wa kampuni jirani,kwamba nimuunganishie. Kwa kazi hiyo alinipa Sh 15,000/-

Nilichuku elfu 5 nikaweka nyumbani. Nikajua elfu kumi itanitosha.. Kwa umahiri wangu wa kuongea nilifanikisha kumfikisha hoteli ambako alikutana na bosi,mi nikapewa posho nyingine ya sh 5,000/-.

Kesho yake alinisifu sana kwamba mi hodari.
Baadaye ikawa kama ndiyo kazi yangu,kwani ilikuwa inanipa kipato kuliko kazi niliyoajiriwa! Nilianza kupendeza kupitia kumkuwadia mabibi mtoto wa bosi! Sikuwa na shida ya hela ndogondogo.. Kuna wakati nilipanga kuandaa mazingira kuchukua hela nyingi kwake kwa mtindo huo kisha niache kazi.

Ni kuhakikisha katika wiki kuna wanawake walau wawili wa kuwafukuzia,ambao mpaka wiki inayofuata watalala na Mhindi wangu. Wakati mwingine naomba fedha nyingi za maandalizi ya kumtafuta na kum-intertain msichana hadi kumfikisha hoteli nako nalipwa tena.

Siku moja niliamua kumuingia dada mmoja ambaye huwa tunakutana kituo cha basi cha Posta mpya. Alinishangaa kidogo,lakini akasema kwa maongezi zaidi,niende kazini kwake kesho yake mitaa ya Oysterbay.Alikuwa zamu ya mchana,hivyo ilibidi kutafuta uongo ili nikatimize ahadi,maana dada alikuwa hotelier.

Alinipokea vizuri na dada alikuwa mrembo kweli. Nami niliomba hela nyingi za "promo" kwani nilimsisitizia huyu wa safari hii ni baab kubwa. Nikala lunch na kunywa. Baada ya kumwaga sera zangu,alionekana kushangaa,mshangao ambao sikuupenda..
Kisha akaniambia"Mbona we ni kijana handsome tu,ya nini utumike na mtu namna hiyo?" nilijibaraguza sana,ingawa sikuweza kuukwepa ukweli kuwa tabia ile si nzuri.
Akasema atanipa jibu kesho yake.

Tulipokutana akasema amekubali,na kwa kuwa anapenda kutunza heshima yake,basi huyo "bwana wake" achukue chumba,kwenye hoteli moja ya ghorofa,maeneo ya River Side.

Bosi kawaida alikuwa anatangulia,mi nikamchukua dada yule hadi chumba alichokuwa bosi wangu. Nikawatambulisha na kabla sijapewa bahasha yangu ili niondoke,paligongwa hodi.

Nikaona ngoja niwasikilize kwanza wahudumu. Nilipofungua,nilishangaa kuona majibaba matatu! mawili ya miraba minne..Moja likaingia kabisa,lingine likaingia na kubaki linaulinda mlango mtu asitoke..
"inaonekana umezoea kazi ya ukuwadi,sasa utakoma!!" aliongea yule mwembamba nadhani mume mtu. Wakati huo Mhindi naye jasho linamvuja..akaniruka kimanga kuwa alishaniambia hataki wake za watu. Wakaliona briefcase wakalifungua ambako ndani yake mlikuwa na minoti mingi sana!

Kabla sijakaa sawa,nilipigwa mtama ambao sijawahipigwa tangia nizaliwe! Nilirushwa juu sana,kabla sijatua,suruali ilikuwa tayari ishararuriwa! Mengine nadhani msomaji unaweza kuhisi kilichoendelea...
 
Jinsi nilivyofedheheka: Kama unadhani unavyochepuka bila kushtukiwa wewe ni mkali soma kisa hiki

Hii ilitokea mwaka 1998 hapa dar.

Alikuwa ni binti mrembo sana kutoka kijiji kimoja huko mkoani Shinyanga wilaya ya Kahama. Alilelewa kwa heshima zote za kisukuma. Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi haikuchukua muda akapata mchumba. Huyu mchumba alikuwa nimuajiriwa katika moja ya idara za serikali hapa dar. Hakuwa akimjua huyu binti zaidi ya kupewa taarifa na wazazi baada ya kuwa wameridhika na tabia za binti, Haikuchukua muda taratibu zikafanywa na kijana akatoka kwenda kuchukua jiko na kuja nae Dar.

Huyu bwana alikuwa akiishi ubungo-msewe na kufanyia kazi posta. Maisha ya mume na mke yakawa yameanza rasmi. Baada ya huyu Dada yangu(ni marehemu kwa sasa) kuishi kwa takribani miezi 8, alizoeana na mama mmoja jirani yao ambae alikuwa na umri mkubwa lakini hakuwa na mume. Alimuheshimu kama Dada yake na wakawa karibu sana kama ndugu. Huyu Dada ingawa hakuwa na mume lakini alikuwa na mtu wake wa kumkuna ambae alikuwa ni tax-driver.

Siku huyu mama akamwambia yule dada kesho yake amsindikize kwenda mtongani kumuona shangazi yake ambae alikuwa mgonjwa. Kwa vile hakuwa na mazoea ya kutoka bila mumewe, akasita kukubali moja kwa moja na kuahidi atakuwa tayari kama mumewe ataridhia. Jioni baada ya kurudi mumewe alimueleza juu ya ombi la yule mama, kwa vile jamaa huyu alimuamini sana mkewe na hata yule mama, aliwaruhusu.

Kesho yake baada ya staftahi, alikuja yule bwana wa yule mama na gari yake na kuwachukua kuwapeleka mtongani. Kuna sehemu walipita kumpitia rafiki wa huyu taxi-driver maeneo ya ubungo maji. Baada ya kuingia huyu bwana safari ikaendelea. Huyu jamaa aliyepitiwa njiani, alikaa siti ya nyuma sambamba na huyu Dada yangu mke wa mtu.

Jamaa alikuwa mchangamfu sana alijitambulisha kwa jina la Erasto na dada nae akajitambulisha kuwa anaitwa Catherine. Yule mama alikuwa anaitwa Husna na tax-driver Mussa. Huyu erasto alikuwa muongeaji sana haikuchukua muda wakawa wamezoeana kama watu wanaofahamiana siku nyingi. Safari ikawa nzuri sana. Walifika salama, jamaa wakawashusha wakawaacha na hadi jioni walipowarudia. Huo ukawa mwanzo wa kufahamiana erasto na cathy! Km nilivyoeleza awali,Husna na Cathy waliheshimiana sana, lakini siku moja wakiwa wameketi barazani wakipiga story Cathy aliambiwa jambo ambalo hakutarajia kuambiwa na mtu anayemuheshimu kiasi kile! Husna alimwambia Erasto anampenda na anamtaka ki-mapenzi. Cathy alihisi baridi ghafla na Husna aliigundua hali ile na kuamua kuwa mnyenyekevu kwa kumuomba radhi. Zilipita km wiki 2 hivi wakiwa hawaelewani,lkn baadae mambo yakaisha na maisha yakaendelea. Baada ya miezi 2 kupita,Cathy alianza kuhisi kitu kisicho cha kawaida,alianza kuhisi anampenda erasto!

Mwezi mmoja baadae alijikuta akiisaliti ndoa yake kwa mara ya kwanza! Penzi likakolea ingawa walijitahidi sana kuficha ili wasigundulike mapema. Awali walikuwa wakikutana buguruni ktk lodge moja iliyopo pale.

Baadae waliamua kubadilisha na kuanza kukutana kariakoo ktk duka la erasto. Erasto alikuwa na duka la nguo kariakoo,chumba cha duka kilikuwa kimekatwa katikati nyuma kulibaki chumba ambacho kilitumika kuhifadhia mizigo. Baadae erasto aliongeza matumizi kwa kununua kitanda na godoro kwa ajili ya penzi lake Catherine. Penzi liliendelea kukolea siku hadi siku. Walikuwa wanakutana mchana,wakati ambao jamaa(mume wa Cathy)anakuwa kazini.

Ilikuwa siku ya ijumaa ya mwezi august mwaka 1998,mchana. Wapenzi hawa walikuwa wanaendelea kuivunja amri ya sita ya Mungu. Km ilivyo kawaida ya kariakoo,kibaka mmoja alikuwa anajaribu kupora wallet ya mtu mmoja,baada ya kumshtukia alianza kufukuzana nae pamoja na raia wengine.

Kelele za mwizi ziliendelea kusikika na hata Cathy na erasto nao walizisikia lkn hawakuzitilia maanani. Yule kibaka alilijua lile duka na kwa vile alikaribia kukamatwa alikimbia kwa kasi na kuingia hadi ktk kile chumba kwa kuwa hakukuwa na ukuta wa kuzuia zaidi ya zile nguo. Yule mtu aliyekuwa anamfukuza yule kibaka,nae aliingia hadi ktk chumba kile kwa lengo la kumkamata mwizi wake.

Hamadi!!! Waliwakuta cathy na erasto wakiwa uchi wa mnyama wakivunja amri ya 6 Mungu. Unajua aliyekuwa anamfukuza mwizi alikuwa nani!!? Siku hiyo mume wa Cathy alitoka kazini mapema na kupitia kariakoo ambako alikuwa na shida binafsi. Akiwa kariakoo ndipo kibaka mmoja akajaribu kumpora wallet yake kwa bahati akamshtukia na kuanza kumfukuza ili amwadabishe. Baada ya kibaka kuingia chumba kile cha duka na yeye aliingia na ndipo alipokutana kitu asichokitarajia mkewe akiwa na mwanaume mwingine akifanyiwa kilekile anachokifanya yeye.

Kibaka alisalimika na tukio la Cathy na erasto ndo likachukua nafasi.

My take; Mungu akiamua kukuumbua atakuumbua kwa fedheha ambayo hutaisahau maishani!
 
Namkumbuka Sana huyu mtu...hili gazeti nilikuwa na nakala zake zote!
Ila Kuna dada mmoja alijifanya mjuaji eti anasafisha gheto langu ....😰😨😰
Ilikuwa ni sabaabu tosha kabisa ya kumpiga chinina kunichkewesha kuoa!
Kimsingi alikuwa mpuuzi
Nakumbuka mwaka 2001 Munga aliitsha shindano dogo la kuandika Makala fupi!
Niliwahi kushinda 10,000/...kupitia Makala moja ya mahusiano...Niliandika 'Kama unataka kuolewa Usijifungie ndani!
Kimsingi kamakala kale ' kalikuwa kanabainisha kuwa enzi za wadada kusubiri wachumba nyumbani zimepitwa na wakati!
RIP Munga
 
Jinsi nivyofedheheka: nikaropoka kichizi bachela ofu masta"

Naomba na mimi niwasaidie ndugu na jamaa zangu ambao hawajipendi.Nimejifunza kujipenda na kujipenda ni kujikubali mtu ulivyo.

Nakumbuka vizuri sana ilikuwa mwaka 1996,wakati huo nikiwa nafanya kibarua kwenye stationary moja jijini Dar as salaam.Nilikuwa nimemaliza kidato cha nne miaka miwili nyuma.Sasa kulikuwa na mkaka mmoja aliyekuwa anakuja pale dukani mara kwa mara.Huyu mkaka kwakweli nilimpenda siku ya kwanza tu nilipomuona.Nilikuwa najua ameoa,lakini nikashindwa kuvumilia kuendelea kumpenda.Kumbe nayeye akawa amenipenda.Basi,siku moja akanitania kama ningeweza kupata naye chakula cha mchana.Nilikubali utafikiri nilikuwa sijala kwa miaka kadhaa[emoji1]

Tulikutana chakula cha mchana na kuzungumza kuhusu vitu vya kawaida vya kimaisha.Tuliendelea kuwasiliana hadi siku aliponiomba tena tukutane kwa chakula cha jioni.Nilijifanya kuzuga kwamba nyumbani wata "maindi"lakini kesho yake nilimjibu inawezakana.Basi tulikubaliana tukutane J'mosi kwa chakula cha usiku.Siku hiyo hakuja pekeake Bali alikuwa na mwanaume mwingine na msichana ambaye alikuwa ni mchumba wa huyo mwanaume mwingine ambaye alikuwa ni rafiki yake sanaa.Tulikwenda hotel ambayo naomba nisiitaje lakini ya nyota 3.Wakati huo nilikuwa sijui hata kama hotel nazo sina sifa ya nyota[emoji4]

Yule jamaa yangu alinambia,huyo rafiki yake na mchumbake walikuja pale ili kula pamoja,halafu wangeondoka na kutupa nafasi ya kuzungumza.Niliona sio vibaya lakini ilinikera kwasababu niliona alitaka wale wanitathmini[emoji20]Basi jamaa yangu alinitambulisha kwao,niliwasalimu na tukaenda mezani,.kwakweli nilikuwa sijawahi kuingia hoteli kubwa hata siku moja....

ILILETWA menu na nilichagua kitu ambacho sikuwa nakijua[emoji85]Ilikuwa supu ya boga,afadhali. KUMBE;ilikuwa kwanza ni supu kabla ya chakula na kila mmoja pale aliagiza supu yake,lakini wenzangu wakiwa wanajua wanafanya nini..wakati tunakunywa supu yule rafiki wa jamaa yangu aliniuliza nilikuwa nimesoma wapi.Yeye alikuwa na maana ya shule au mkoa.Mimi kwasababu niliwasikia wakitia maneno ya kiingereza kila mara,niliona nijikweze kidogo.'Nilimaliza Mlimani.'.nilijikuta nikisema,.walishangaa wote[emoji44]Mwaka gani??Yule jamaa aliuliza kwa shauku.

Nilijua nimejibana mwenyewe kwa kutaka kujionesha.'Mwaka Jana.' Wote waliacha kunywa supu zao,.pengine wakijiuliza ilikuwaje hawakuniuliza swali hilo mapema.Yule jamaa yangu alionesha kushtuka zaidi. 'Ulikuwa unachukua nini?' Yuleyule tena aliuliza,.kiherehere tuu!![emoji57]Tangu nizaliwe nilikuwa sijawahi kukutana na mtihani kama ule.Nilifikiri harakaharaka."BACHELA OFU MASTA" nilisema kwa kujiamini[emoji6]Walishangaa zaidi na walijua nimekosea,walijua labda nilitaka kusema,Bachela ofu sayansi..Unajua,kwasababu ya matarajio makubwa mtu anaweza kudhani yeye ndiye kakosea.Labda walidhani wao ndiyo hawajasikia..

'Ulikuwa hostel au ofu kampasi' Yule mwanamke mwenzangu nae alishikwa na kiherehere,.Sikujua hata anauliza kitu gani na nilijilaumu kwasababu nilidhani wale jamaa pale walikuja wamemaliza kidato cha 6 au cha 4 kama changu,hivyo nilitaka KUWAKOGA....'hostel' nilisema nikiwa nimeshupaa utafikiri naapishwa kuwa rais wa nchi..'Ya wapi??' Yule mwanamke aliuliza tena(cha umbea) sikuwa najua hata hizo hostel ziko wapi,.Lakini nakumbuka niliwahi kusikia Mabibo hostel..Nikasema 'Mabibo'...'Digrii yako ulispesholaizi nini?? Hapo safari ikafika mwisho kama ni reli basi ikawa ni Kigoma.Nilifikiri kwa muda kabla sijasema 'kwani nyie mnataka nini hasa,sijafika chuo kikuu nilikuwa natania tuu.Mimi elimu yangu ni kidato cha nne' nilisema na wote wakaangua kicheko hadi wateja wengine wakavunja shingo kuangalia. 'Nilistuka Ile bachela ofu masta,du!!' Yule jamaa yangu alisema.

MWISHO;hivi sasa yule jamaa ndiye mume wangu na Mimi nasoma chuo cha biashara nikichukua diploma.Tuna watoto wawili.....Nataka kusema hivi,ukijikataa ni lazima utaadhirika..kuwa wewe haitakudhuru mwenzangu'[emoji108][emoji108]

NB:hii ni stori ya kweli iliandikwa kwenye gazeti JITAMBUE la July 13-19 mwaka 2005 chini ya Munga Tehenani(rip)
😃😃😃 Umenikumbusha mbali Sana!
 
Hizi chai zilikuwa zinabamba sana. Lakini zina u-afadhali mara dufu ya hizi chai za sasa zinazorushwa hapa JamiiForums... Hahahah
 
Jinsi nilivyofedheheka: Kama unadhani unavyochepuka bila kushtukiwa wewe ni mkali soma kisa hiki

Hii ilitokea mwaka 1998 hapa dar.

Alikuwa ni binti mrembo sana kutoka kijiji kimoja huko mkoani Shinyanga wilaya ya Kahama. Alilelewa kwa heshima zote za kisukuma. Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi haikuchukua muda akapata mchumba. Huyu mchumba alikuwa nimuajiriwa katika moja ya idara za serikali hapa dar. Hakuwa akimjua huyu binti zaidi ya kupewa taarifa na wazazi baada ya kuwa wameridhika na tabia za binti, Haikuchukua muda taratibu zikafanywa na kijana akatoka kwenda kuchukua jiko na kuja nae Dar.

Huyu bwana alikuwa akiishi ubungo-msewe na kufanyia kazi posta. Maisha ya mume na mke yakawa yameanza rasmi. Baada ya huyu Dada yangu(ni marehemu kwa sasa) kuishi kwa takribani miezi 8, alizoeana na mama mmoja jirani yao ambae alikuwa na umri mkubwa lakini hakuwa na mume. Alimuheshimu kama Dada yake na wakawa karibu sana kama ndugu. Huyu Dada ingawa hakuwa na mume lakini alikuwa na mtu wake wa kumkuna ambae alikuwa ni tax-driver.

Siku huyu mama akamwambia yule dada kesho yake amsindikize kwenda mtongani kumuona shangazi yake ambae alikuwa mgonjwa. Kwa vile hakuwa na mazoea ya kutoka bila mumewe, akasita kukubali moja kwa moja na kuahidi atakuwa tayari kama mumewe ataridhia. Jioni baada ya kurudi mumewe alimueleza juu ya ombi la yule mama, kwa vile jamaa huyu alimuamini sana mkewe na hata yule mama, aliwaruhusu.

Kesho yake baada ya staftahi, alikuja yule bwana wa yule mama na gari yake na kuwachukua kuwapeleka mtongani. Kuna sehemu walipita kumpitia rafiki wa huyu taxi-driver maeneo ya ubungo maji. Baada ya kuingia huyu bwana safari ikaendelea. Huyu jamaa aliyepitiwa njiani, alikaa siti ya nyuma sambamba na huyu Dada yangu mke wa mtu.

Jamaa alikuwa mchangamfu sana alijitambulisha kwa jina la Erasto na dada nae akajitambulisha kuwa anaitwa Catherine. Yule mama alikuwa anaitwa Husna na tax-driver Mussa. Huyu erasto alikuwa muongeaji sana haikuchukua muda wakawa wamezoeana kama watu wanaofahamiana siku nyingi. Safari ikawa nzuri sana. Walifika salama, jamaa wakawashusha wakawaacha na hadi jioni walipowarudia. Huo ukawa mwanzo wa kufahamiana erasto na cathy! Km nilivyoeleza awali,Husna na Cathy waliheshimiana sana, lakini siku moja wakiwa wameketi barazani wakipiga story Cathy aliambiwa jambo ambalo hakutarajia kuambiwa na mtu anayemuheshimu kiasi kile! Husna alimwambia Erasto anampenda na anamtaka ki-mapenzi. Cathy alihisi baridi ghafla na Husna aliigundua hali ile na kuamua kuwa mnyenyekevu kwa kumuomba radhi. Zilipita km wiki 2 hivi wakiwa hawaelewani,lkn baadae mambo yakaisha na maisha yakaendelea. Baada ya miezi 2 kupita,Cathy alianza kuhisi kitu kisicho cha kawaida,alianza kuhisi anampenda erasto!

Mwezi mmoja baadae alijikuta akiisaliti ndoa yake kwa mara ya kwanza! Penzi likakolea ingawa walijitahidi sana kuficha ili wasigundulike mapema. Awali walikuwa wakikutana buguruni ktk lodge moja iliyopo pale.

Baadae waliamua kubadilisha na kuanza kukutana kariakoo ktk duka la erasto. Erasto alikuwa na duka la nguo kariakoo,chumba cha duka kilikuwa kimekatwa katikati nyuma kulibaki chumba ambacho kilitumika kuhifadhia mizigo. Baadae erasto aliongeza matumizi kwa kununua kitanda na godoro kwa ajili ya penzi lake Catherine. Penzi liliendelea kukolea siku hadi siku. Walikuwa wanakutana mchana,wakati ambao jamaa(mume wa Cathy)anakuwa kazini.

Ilikuwa siku ya ijumaa ya mwezi august mwaka 1998,mchana. Wapenzi hawa walikuwa wanaendelea kuivunja amri ya sita ya Mungu. Km ilivyo kawaida ya kariakoo,kibaka mmoja alikuwa anajaribu kupora wallet ya mtu mmoja,baada ya kumshtukia alianza kufukuzana nae pamoja na raia wengine.

Kelele za mwizi ziliendelea kusikika na hata Cathy na erasto nao walizisikia lkn hawakuzitilia maanani. Yule kibaka alilijua lile duka na kwa vile alikaribia kukamatwa alikimbia kwa kasi na kuingia hadi ktk kile chumba kwa kuwa hakukuwa na ukuta wa kuzuia zaidi ya zile nguo. Yule mtu aliyekuwa anamfukuza yule kibaka,nae aliingia hadi ktk chumba kile kwa lengo la kumkamata mwizi wake.

Hamadi!!! Waliwakuta cathy na erasto wakiwa uchi wa mnyama wakivunja amri ya 6 Mungu. Unajua aliyekuwa anamfukuza mwizi alikuwa nani!!? Siku hiyo mume wa Cathy alitoka kazini mapema na kupitia kariakoo ambako alikuwa na shida binafsi. Akiwa kariakoo ndipo kibaka mmoja akajaribu kumpora wallet yake kwa bahati akamshtukia na kuanza kumfukuza ili amwadabishe. Baada ya kibaka kuingia chumba kile cha duka na yeye aliingia na ndipo alipokutana kitu asichokitarajia mkewe akiwa na mwanaume mwingine akifanyiwa kilekile anachokifanya yeye.

Kibaka alisalimika na tukio la Cathy na erasto ndo likachukua nafasi.

My take; Mungu akiamua kukuumbua atakuumbua kwa fedheha ambayo hutaisahau maishani!
Hahahaha.... nacheka sana mimi wallah..
 
Hizi chai zilikuwa zinabamba sana. Lakini zina u-afadhali mara dufu ya hizi chai za sasa zinazorushwa hapa JamiiForums... Hahahah
Hii yangu ni OG kabisa

Ile chupi ikaanguka mbele ya wote...
 
Hahahaha.... nacheka sana mimi wallah..
Wakaniambia 'shemeji piga mzigo'

Nilikutana na binti huyu mwaka 1990 wakati huo nikikaa na kaka yangu maeneo ya Mwenge. Siku hiyo nilikuwa nimetumwa maeneo ya Ubungo na nilikuwa naendesha gari la kaka yangu aina ya Toyota Mark II ambayo ilikuwa bado ina hali nzuri na mziki mnene. Nilikuwa nimepiga T-shirti na Jinzi na miwani ya jua. Niliamua kupitia barabara ya Chuo Kikuu lengo langu likiwa ni kujaribu bahati yangu kama nitakutana na binti yeyote anayesubiri usafiri nimpe lifti na kujaribu kutupia nyavu.

Ilikuwa ni kawaida yangu kila nikitumwa na kaka na kupewa gari napitia barabara ya Chuo Kikuu lengo langu likiwa ni hilo la kuopoa vimwana na mara nyingi nilikuwa sikosi kimwana wa kumpa lifti na kumtongoza. Wapo niliokuwa nikiwapata na wale niliokuwa nikiwaona washamba nilikuwa nawapotezea.

Siku hiyo nilibahatika kumpata binti mmoja. Alikuwa ni mzuri hasa kwa sura na umbo na weupe unaoashiria kuwa mambo yake ni mazuri. Nilisimama na kumtupia salaam, na yeye bila kusita aliniitikia na ndipo nikamwambia kama anaelekea Ubungo nimsogeze. Awali alisita lakini baada ya kumsisitiza alikubali kupanda nikaondoka naye. Njiani nilianza kumsomesha, hakuonekana kuwa mgumu, ingawa nilijishtukia kutokana na binti huyo kuonekana ni wa matawi.

Aliponiuliza ninaishi wapi na ninachofanya, nilimwambia ninaishi kwa kaka yangu ambaye ni mwanajeshi na nikamdanganya kwamba, ndio nimemaliza chuo kikuu mwaka uliopita na kwa sasa ninafanya kazi kama mwanadiplomasia pale wizara ya mambo ya nchi za nje. Nilimwambia kuwa, huwa nasafiri mara kwa mara nje ya nchi kwa shughuli za kikazi na kuonekana kwangu nchini ni mara chache sana. Aliponiliza kama huwa nasafiri nchi gani, nilimwambia, huwa natembelea zaidi nchi za Maziwa makuu. Hata hivyo nilimwambia kwamba, ndio ninajipanga nitafute nyumba ili nihame kwa kaka yangu kwa kuwa ndio nimeanza kazi nilikuwa bado najipanga ingawa kaka yangu hataki nihame hapo kwake.

Kwa upande wake alinijulisha kwamba na yeye amesoma nchini Uingereza na anafanya kazi katika ubalozi fulani wa mojawapo ya nchi za Scandinavia (naomba nisiutaje huo ubalozi) na anaishi na wazazi wake ambapo baba yake ni mhadhiri hapo Chuo kikuu. Alianza kunipigisha mastori yanayohusiana na mambo ya kidiplomasia ikabidi nimpotezee na kubadilisha stori ili asije akanishtukia.

Baada ya kumpa soma alikubali na kuniahidi nimtembelee hapo nyumbani kwao wiki ijayo mwishoni mwa juma ili tutoke out kwa ajili ya kufahamiana zaidi. Kwa kuwa simu za mkononi zilikuwa bado hazijaingia nchini alinipa namba ya simu ya nyumbani kwao. Tulipofika Ubungo aliteremka na kushika hamsini zake akiniacha na mimi nikifanya shughuli iliyonipeleka hapo Ubungo. Kwa muda mfupi nilioongea na yule binti alionekana kunipenda sana kwani hata wakati anashuka kwenye gari alinisisitiza sana tuonane hiyo wiki ijayo.

Ukweli ni kwamba nilikuwa sina kazi, na nilikuwa ndio nimemaliza kidato cha nne na kuangukia pua, yaani kwa kupata divisheni ya ziro. Wiki iliyofuata tangu nikutane na yule binti nilipata kazi ya kutembeza vitu na kuuza, maarufu kama promosheni. Siku hiyo nikiwa na furushi langu la vyombo na mwenzangu mmoja, yule binti aliniona. Alinikuta maeneo ya Kijitonyama akiwa kwenye gari. Mimi sikumwona, na alinipigia honi na alipoona sisikii alishuka. Alinikimbilia huku akiniita jina. Niligeuka na kugundua kuwa ni yule mpenzi wangu wa Chuo Kikuu niliyempa lifti na kumpiga fix.

Nilibabaika sana kwa kweli. Ilibidi hata kabla hajanisemesha, nimwambie Yule mwenzangu, ‘au labda ni nyumba hii hapa, maana nimechoka sana.' Yule binti akiwa ameshikwa na butwaa aliniuliza mbona niko kule na furushi kubwa. Nilimwambia, ‘ninamsindikiza huyu boy shamba wetu kwao. Ameacha kazi nyumbani nataka nimkabidhi kwa kaka yake. Ndio anajaribu kunionyesha nyumba, lakini naona kama naye kapasahau.' Nilimjibu nikiwa nimebabaika sana.
‘Oh, Nilishangaa kukuona na hilo furushi. Je nikupeni lifti ili tutafute hiyo nyumba yenyewe?' aliniuliza. Nilimwambia asisumbuke, tutatafuta hiyo nyumba na tutaipata tu. Aliniaga akionyesha kutoridhishwa na maelezo yangu.

Baada ya tukio lile niliona kazi ile haifai na nikaamua kuiacha. Nilipata kazi kwenye mghahawa mmoja uliopo mjini karibu na posta. Nilianza kazi pale kama mhudumu yaani waiter. Siku moja nikiwa nachukua order ya chakula waliingia wateja, sikuwatazama vizuri kwa sababu ya kashkash ya kazi mchana huo. Nilikwenda katika meza yao ili kuchukua order yao. Nilipofika pale walipokaa hao wateja nilikutana uso kwa uso na yule mpenzi wangu wa Chuo Kikuu. Niliishiwa pozi. Niligeuka haraka na kutaka kuondoka. Nilikuwa nataka kukimbilia jikoni. Lakini nilikuwa nimechelewa. Kwani aliniita kwa jina na kusema, ‘usijali, najua kinachoendelea. Ndio maana nimeamua kuja kula hapa. Chukua order yetu ya chakula na kuwa tu huru, kwani tangu wakati wa promosheni ya vyombo, nilikuwa najua….'

Aliposema hivyo aliwatazama wale wenzake. Mmoja wao aliniambia, ‘shem usijali piga mzigo, mapenzi kitu kingine na kazi zetu kitu kingine.' Nilienda jikoni, lakini sikurudi tena. Yaani ilikuwa ni kashfa kubwa ambayo sitakuja kuisahau mpaka leo hii niko na mama Ngina. Hadi leo sijui yule binti yuko wapi. Maana niliacha kazi na kwenda kusoma mkoani Arusha. Nashukuru hakujua ninaishi wapi pale Mwenge. Hata hivyo nilijifunza mengi, lakini kubwa zaidi nilijifunza kujiamini na ndio maana hadi leo mtu akiniliza nakaa wapi na ninafanya kazi gani ninamwambia ukweli kwamba ninaishi Mwanayamala kwa Kopa na ninafanyakazi ya Kuuza kahawa mjini.
Mtambuzi
 
Ukiweka ahadi lazima uitimize.. Ukiweka nadhiri ni lazima uitangue la sivyo itakutesa kifikra na kudai utanguzi

Mwaka wa jana kwenye post moja, tukiwa na mjadala, tulimjadili gwiji wa falsafa maizi Hayati Munga Tehnan na nikaahidi kuna na mada maalum kwa ajili yake kumuenzi. Naomba sasa nitangue nadhiri na ahadi yangu hii kupitia mada hii

Kwa wengi wasiomfahamu ndio alikuwa Mmiliki wa gazeti la utambuzi liitwalo JITAMBUE na MSHAURI. Humo ndani kulijaa madini tupu ya falsafa kindakindaki, saikolijia, mambo ya kiroho kijamii hata utani na simulizi za kufurahisha sana

Mimi ni mmoja wa shabiki na mwanafunzi wake mkubwa... Wengine ninaoweza kuwakumbuka kwa haraka ni pasco na Mtambuzi ..Natambua list ni ndefu na kila mmoja atakuja na mchango wake

Uzi utakuwa updated kutokana na kadiri maudhui yatakavyokuwa yanapatikana ili hatimaye tuwe na mada iliyoshiba kumhusu Munga Tehnan

Naamini kati yetu kuna wanaojua historia yake, maana mtandaoni haupatikani

Ombi kwa Moderator Kama kuna uwezekano wa kuziweka mada zake pamoja kwenye mada moja kuu, zile zenye maudhui ya kufanana

Ombi kwa wana JF kama kuna mwenye hard copy ya kazi zake kupitia JITAMBUE pls share
Huyu jamaa alikuwa maarufu sana kabla ya 1999. Baada ya kifo cha Mwl. Nyerere mwanzoni kwa mwaka 2000 "alitunga" kitabu akimsema vibaya Mwalimu kuwa alishindwa kuilea vizuri familia yake na umaarufj wake ukaishia hapo. Ndio akaanza kuandika mambo ya uchawi uchawi na kumvutia sana Mshana Jr.
 
Halafu wewe ukavutiwa na nini
 
Mtaalam na mwalimu wa Utambuzi Munga Tehenan alifariki tarehe 5 Mei 2008 na kuzikwa pale makaburi ya Kisutu. Siku chache kabla ya kufariki aliandika makala isemayo 'HII NI MAITI YA NANI?'. Hii ilikuwa kama utabiri wa kitakachotokea na kwa waliokuwepo msibani wanaelewa kuwa kulitokea kama makala ilivyoeleza

HII MAITI NI YA NANI?
Nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari, niliwahi kushuhudia mwili wa mwanafunzi mwenzetu ukigombewa na wazazi wake. Huyu mwanafunzi mwenzetu alifariki ghafla shuleni na ikabidi wazazi wake wafahamishwe ili waseme maiti isafirishwe kwenda wapi.Mama alisema, maiti ya mwanaye ibaki hapo alipofia, kwani atakuja kuichukua na kuisafirisha kuipeleka kwao (mama) kwa mazishi. Baba naye alisema hivyo hivyo. Walimu wakaamini kwamba, baba na mama wanazungumza jambo lilelile. Lakini walipowasili pale shuleni, ndipo walipogundua kwamba, hawakuwa wanawasiliana na watu walio pamoja.Baba alikuwa na dini nyingine na mama alikuwa wa dini nyingine na walishaachana kitambo.

Tangu walipoachana wazazi hawa, kila mmoja akawa anamvutia mtoto aingie au afuate dini yake. Kwa jinsi tulivyokuwa tunamfahamu marehemu, hakuwa hasa mtu wa dini fulani. Wakati wa vipindi vya dini, huyu mwenzetu alikuwa anaingia mara kwenye madarasa ya waislamu, mara wakristo na alikuwa anaingia kwenye madhehebu mbalimbali.Basi, wazazi hawa walikuwa kila mmoja akitaka kuchukua mwili wa marehemu. Kila mmoja alikuwa akitoa maelezo ni kwa nini yeye ndiye anayestahili kumzika mtoto kwa dini yake. Malumbano haya yalikuwa makubwa mpaka vyombo vya dola vikahusishwa. Nakumbuka alikuja afisa mmoja wa upelelezi kwenye malumbano hayo. Katika kujaribu kutafuta muafaka, afisa huyu alizungumza kama vile kwa kuhutubia akisema: Inasikitisha kwamba, kijana wetu mpendwa, anaingizwa kwemye choyo na ubabe wa kuoneshana nani zaidi, katika hali hii ambapo hawezi kujitetea.

Naamini, huyu marehemu kwa sasa anawachukia wazazi wake wote, kwani anajua wazi hakuna anayempenda hata mmoja, bali wanatumia kifo chake kama uwanja tu wa mapambano ya kujitosha kwao.Naamini, hivi sasa marehemu angeombwa kuchagua rafiki na ndugu wa kweli, angechagua wanafunzi wenzake na walimu wa dini. Hii inatokana na ukweli kwamba, hawa hawakutaka kumpangia aabudu au kuifuata imani gani ya dini. Tunaambiwa aliingia kwa waislamu, na aliingia kwa wakristo pia, hakuzuiwa au kusemewa, alikuwa huru.

Kuwa na dini ni kuwa na uhuru. Kuwa na dini ni kuwapa wengine uhuru wa kuwa wao. Kuwa na dini siyo kutumia tatizo la mwingine kujifaharisha, kuonesha ubabe na urijali ulionao. Hiyo ni kibri ambayo kwa mtu aliyepoteza mwili kama huyu kijana wetu anaiona na kuijua vizuri, haipendi hali hii..Hotuba hiyo ilisaidia sana, kwani hatimaye ndugu wa upande wa mama na wale wa upade wa baba walikaa chini wakiwa na adabu mpya na kujadili. Hatimaye walikubaliana kijana azikwe kwa dini ya mama yake.

Miaka 30 baadaye, nakutana tena na watu wanaogombea maiti, watu wanaoamini kwamba mzoga wa binadamu una maana yoyote. Sijawahi kuona mtu akitoa shati au gauni kwenye mfuko wa nailoni na kuvaa mfuko huo badala ya kuvaa shati au gauni, nimesema sijawahi kuona, huko ni kujidanganya. Nimekuwa nikiona sana jambo hilo, ambapo ni pale watu wanapogombea mwili.Inaonesha wazi kwamba, binadamu. bado ni mjinga sana juu ya maisha yake.

Mwili, mwili ni nini, na hadi wapi? Kama mwili ungekuwa na maana sana, baada ya mtu kufariki usingekimbizwa mochuari, usingepakwa asali au usingechomwa sindano ili usiharibike na kuleta usumbufu wa harufu na maradhi. Mwili siyo mimi wala wewe. Mwili haujawahi kuwa mwenye mwili na hautakuja kuwa. Mwili ni kama tochi tu, ambayo umeiazima ili iweze kukusaidia kufika kijiji cha pili, kutokana na giza na njia ya uchochoro ambayo unatakiwa kuipita ili kufika kijiji hicho cha pili. Mwili ni kifaa na siyo wewe, bali wewe unakitumia kifaa hicho Binadamu anajibainisha kwenye maisha haya ya hapa duniani kupitia mwili wake, lakini yeye siyo mwili. Mwili ni ubainisho, ni chombo cha kutumika kwa kusudi la kidunia tu. Baada ya muda mwili hukoma kuwepo, hujimaliza wenyewe au kumalizwa, ili binadamu amudu kuingia hatua nyingine ya maisha ambayo haitumii au haihitaji mwili.

Tangu ulipozaliwa umeoneshwa na kufundishwa kwamba, wewe ni mwili kwa njia zote. Akili yako imeshika kutu kwa kuamini kwamba, mwili ni wewe na wewe ni mwili. Huna uwezo tena wa kuuona ukweli, kwa sababu vipimo vyako vyote kuhusu maisha vinaishia kwenye akili, ambayo nayo pia haikuhusu, siyo yako, umepachikwa tu. Kwa ujinga huu wa kutojua mwili ni nini na sisi ni nani, ndipo ambapo tunaingia kwenye ujinga wa kuendeshwa na miili yetu, hisia zetu na akili. Kila mmoja anaamini kwamba, mwili wake ukipotea, ukishindwa kutumika, yaani akifa, basi huo ndiyo mwisho wake. Kama hiyo ni kweli, ina maana binadamu hana maana kabisa, ni upuuzi usiofaa kuelezewa!Yaani binadamu amekuwepo ili awepo kwa mwezi mmoja, miaka kumi, hamsini, sabini, tisini, au mia tu. Halafu baada ya hapo basi. Huu ni uongo mkubwa sana, unaoweza kukubaliwa na akili makapi ya kulishwa tu! Anayetafakari zaidi kidogo, atabaini kwamba, mwili ni mwili tu, ni kasha tu. Ni kasha ambalo muda wake wa kutumika ukiisha mtumiaji au [wewe] analiacha kwa sababu haliwezi kukidhi kile anachokihitaji hapa duniani.

Mtumiaji anachukua kingine ambacho kinakidhi wakati huo [baada ya kifo] . Kwa hiyo, binadamu hafi bali mwili ndiyo unaofikia ukomo wa muda wake wa matumizi kwa sababu mbalimbali.Anapokufa John au Hamisi, haina tofauti. Anapokufa mkulima hohehahe au tajiri kuliko wote duniani, pia haina tofauti. Wote wanapita kwenye hatua muhimu ya mabadiliko, ambapo wanaacha matumizi ya kifaa kilicho kuwa ndicho pekee kinachoweza kuwabainisha na wengine hapa duniani na kuchukua kingine ambacho hakiwezi kuwabainisha tena na wale wenye miili bado. Anapokufa John au Hamisi, haijalishi kama amezikwa kwa jeneza la dhahabu na mizinga 100 au kwa masululu butu na kaniki. Kuzikwa ni utaratibu wa kimazoea wa kuhifadhi mwili ambao sasa ni mzoga tu, ili usisumbue watu wengine kwa harufu na maradhi. Kuzika haina maana kwamba, kunambadili aliyekuwa akitumia mwili huo [marehemu], la hasha.

Kama unadhani kwamba Mungu anahesabu umezikwa na dini gani, umezikwa na shehe au padri gani, ndiyo afanye uamuzi wa kukupokea mbinguni au hapana, ujue unahitaji msaada wa haraka, kama siyo kupelekwa milembe. Ujue hujui chochote ingawa umekuwa ukujidanganya kwamba unajua.Mungu wa kweli hahangaiki na mzoga, bali sisi kwa ufinyu wetu ndiyo tunaodhani kwamba, mizoga au[maiti] hii ina maana. Mara nyingi nimekuwa nikiwaambia jamaa zangu, ‘nikifa, mtaangalia ni mazingira gani ni rahisi kwenu kuutupa au kuuhifadhi mwili wangu. Kwa nini? Kwa sababu, kama sikuwa karibu na Mungu wakati nikiwa na mwili, huo, ukaribu utaletwa leo wakati nimeupoteza mwili huo kwa sababu tu, mwili wangu umezikwa kwa dini ya babu yangu? Ukosefu wa ufahamu wa kiwango kikubwa sana. Kama nilikuwa karibu na Mungu wakati wa uhai wangu, basi hata nikitupwa chooni baada ya kufa, ukaribu huo hautakufa. Mungu hayatazami mambo kama Abdallah Juma au John Maiko! Kwani kuzika hasa ni kitu gani.

Hatuziki watu ili waende mbinguni. Kama ni hivyo, wanaoliwa na wanyama, kuungua na kuteketea kabisa, wao Mbinguni hawatafika? Kama hawatafika, watahukumiwa vipi siku ya mwisho? Mwili hautakiwi Mbinguni, hauna kazi huko, kwani huko siyo makazi ya miili. Mwili unafaa tu duniani Kuna zile jamii ambapo mtu akifa mwili wake huchomwa moto na kuteketezwa kabisa Unadhani hizi jamii hazimjui Mungu kama wewe unavyomjua? Zinamjua, tena pengine vizuri zaidi yako. Lakini, zimeng’amua kwamba, mwili ni kasha tu, likishindwa kufanya kazi, ni sawa na taka nyingine, hutupwa dampo na kuteketezwa kwa moto. Mtu akishauacha mwili wake [kufa] hana tena uhusiano na mwili huo. Mtu huyo anakuwa ameingia kwenye awamu nyingine ya maisha ambayo haihitaji mwili na ambayo haihitaji kujua huo mwili umezikwa na nani na wapi. Ni akili isiosogea ndiyo ambayo inashindwa kufanya mikokotoo midogo kama hii.Ukiona watu wanagombea maiti, jua kwamba, hata kama wamevaa masuti na kubandika digrii zao kwenye kila ukuta, ni watoto wadogo kiufahamu.

Ukiona mtu pia anaacha wosia mrefu wa namna anavyotaka akifa azikwe, naye huyo ni mpujufu tu wa ufahamu. Kwa nini? Unagombea kuuzika mwili wa fulani ili upate kitu gani, ili huyo marehemu naye apate nini? Hata usipouzika, kumbuka kwamba, ameshakufa na ukiuzika, ameshakufa pia. Haifanyi tofauti yoyote kwa kweli. Kama nilivyosema awali, huuziki mwili ili uende Mbinguni kwa sababu mbingu haiko ardhini. Unaufukia ili usisumbue kwa harufu.Ukienda kwenye nchi zenye vita hasa vya wenyewe kwa wenyewe, utagundua kirahisi kwamba, maiti hana maana, maiti ni msumbufu kwa kunuka na kusambaza magonjwa.

Tunazika kwa sababu tuna nafasi ya kuhifadhi mwili kwa heshima na taratibu ambazo zinaonesha kujali mwili wa mwenzetu ambao ulitumika kufanya mema au maovu. Kwenye kizuizi na misukosuko au vita, hakuna anayeweza kukumbuka, siyo kuzika bali hata kufukia maiti. Kila mmoja anafikiria kuendelea kubaki na mwili wake kwanza. Aliyepoteza wake, basi hakuna anayemjali, kwani haina maana kabisa kumjali. Hata aina nyingine za mazishi zinaonesha tu ujinga na utoto wa binadamu. Mazishi ya kifahari yenye kuhusisha majeneza ya dhahabu na vyakula na vinywaji vya bei mbaya. Ni ujinga uliopindukia kwa sababu, inawezekana kabisa marehemu au wanaotoa fedha hizo hawajawahi kumsaidia aliye hai hata kwa chupi ya mguu.

Sasa kusaidia huo mzoga kwa mapambo inaongeza kitu gani? Nimesema unapoona mtu anaacha wosia ili azikwe vipi, wosia ambao wakati mwingine ni kero tupu, ujue huyo naye ni mtoto wa miaka sita, bila kujali anamiliki au amesoma hadi kiwago gani. Ni utoto kwa sababu, unapoacha mwili, siyo kazi yako kusema huo mwili ufanyiwe kitu gani. Waliobaki, wanaweza kuamua kuuchoma mishikaki [kama wanakula watu], wanaweza kuukausha na kuuweka kwa maonesho, wanaweza kuufukia kwenye kijishimo cha futi tano na ukafukuliwa na fisi usiku, na wanaweza kuuzika kwa matarumbeta na sanduku la dhahamu. Ni hiari yao. Ukishauacha mwili huna mamlaka nao tena. Ni wale waliobaki ndiyo wanaolimbuka nao tu.

Nimekuwa nikitazama hii tabia ya kugombea maiti kwa jicho lenye mashaka na ufahamu wa binadamu, hofu zake na ufisadi wa nafsi alionao. Mtu amekufa, wewe unasema nataka nimzike mimi, sawa. Kwani mbona huendi hospitalini ukaulizia maiti ambazo hazina ndugu na kuzichukua ili ukazizike? Wewe si unapenda kuzika na unaamini kumzika mtu kwa dini yako ni jambo kubwa na la maana sana? Pia hospitalini, utapewa maiti nyingi zisizo na ndugu. Ukishazipata zibadili majina na kuziingiza kwenye dini yako kwa mujibu wa utaratibu wa dini yako. Halafu zika! Hiyo huitaki kwa sababu haina maslahi, haina kuonesha ubabe ambao umefundishwa na wazazi, na jamii na pengine hata na dini yako hiyohiyo. Kugombea maiti ni kujiogopa.

Kugombea maiti ni kujitafuta kimakosa. Kugombea maiti ni kutojua dini. Kugombea maiti ni kudhani mtu anaweza kuwa na uhuru wa kuwa mtu mwingine. Kugombea maiti ni kufikiri wewe ni mwili, Kugombea maiti ni njaa ya mali au haja ya kupanda kithamani. Kwa ujumla ni ubabe wa kimtaa zaidi. Mara nyingi imeshatokea, anapookotwa maiti na watu wakaanza kuulizana, jamani maiti hii ni ya nani? Ujue maiti hiyo itazikwa na serikali. Hakuna mtu au kundi la kidini la eneo hilo ambalo litajitokeza kuichukua na kuizika maiti hiyo kwa imani yake. Hilo haliwezekani kwa sababu halina utamu.

Halina kubishana, halina kulumbana, halina ujuaji na ubabe. Anasubiriwa mtoto mwenye mzazi walioachana na walio na dini tofauti. Huyu akifa, hasira na visasi vyote vya nyuma vinaishia kwenye mwili wake. Atasubiliwa yule ambaye alishakuwa kwenye dini yetu akatoka, huyo akifatuna sababu ya kugombea maiti. Kama nilivyosema, hapo kuna malumbano na ujuaji na kuoneshana. Halafu bado mnajiita mnatumikia dini, zipi? Ni ujinga tu.

Rest in Peace, Munga Tehenan.

Mshana umeandika ndefu mno ila imejaa maneno ya maana tupu mtu huwezi choka soma hadi mwisho.Ila kuna mahali nilitaka kidogo niongezee ni kupanga uzikwe vipi si jambo la maana.Mimi ninachopinga ni mtu kusema azikwe labda kwenye sanduku la dhahabu au na gari lake zuri haina maana kabisa.
Ila mtu kupanga azikwe sehemu gani kama ndugu watakuwa wanaweza hii kwa upande mwingine ina mantiki flani.Jiulize kwanini waislam hadi leo kaburi la mtume Mohamed lipo na wanakwenda kuhiji hii inaimarisha dini ya kiislam kwa YESU sina usemi maana alipaa mbinguni.Watu wa mikoa ya Kilimanjaro mmoja wapo wewe hii mila mnaitukuza sana kiukweli ina mantiki kufanya watu wapende kwao.Familia kuna wakati hata kama wako nchi za nje na mikoa mbali mbali kila baada ya mwaka au miaka miwili wanakumbuka kwenda kwao ajili wanajua mwili wa babu yao au baba yao ndipo ulipo.Usione wazungu wameendelea ila hakika wanapenda kwao.Mtu asiyependa kwao ni mtumwa.
Kumbuka maiti ya binadamu na mbuzi sio sawa binadamu ana heshima zaidi na ndio maana kuna baadhi ya watu mashuhuri walifariki vifo visivyo na heshima wakazikwa vibaya baada ya kupita miaka wanafukuliwa wanapewa maziko ya heshima.Elewa hili jumba(mwili) ambalo sio wewe ndio lilikuwa na dhima ya kukubeba wewe ukiwa duniani jumba na lenyewe lina heshima yake.
Hata nyumba uliyokuwa unaishi ukaja hama utakuwa unaiheshimu na kuikumbuka.Siku moja nilipita mtaa wa Makiyungi Magomeni nikaona nyumba tulikuwa tunaishi na baba yangu nilikuwa mdogo sana mwaka 1969 ila sikusita kugeuza macho na kuonyesha kidole nikaonyesha wenzangu kuwa tuliishi hapa zamani japo baba yangu kafariki siku nyingi au watu maarufu mfano baba wa Taifa pale Magomeni japo aliondoka siku nyingi lakini sehemu hiyo inabeba historia kuwa hii nyumba aliishi baba wa Taifa.Nilipita siku moja Mwanza karibu na Mkuyuni nikaona kuna mwenge umeweka sehemu karibu na barabarani nikakuta maandishi kwa chini hii nyumba baba wa Taifa Nyerere alilala hapa kipindi amekuja Mwanza kutafuta uhuru.
Unaona Nyerere mwenyewe hayupo lakini sehemu au nyumba aliyoishi inapewa bado heshima.
 
Elewa hili jumba(mwili) ambalo sio wewe ndio lilikuwa na dhima ya kukubeba wewe ukiwa duniani jumba na lenyewe lina heshima yake..... [emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Wakristo hili jumba mwili ndio wanaita kanisa
 
Back
Top Bottom