Kumbukizi: Marehemu Horace Kolimba aliitwa ajieleze kwa kusema CCM imekosa dira, apumzike kwa amani

Kumbukizi: Marehemu Horace Kolimba aliitwa ajieleze kwa kusema CCM imekosa dira, apumzike kwa amani

Habari wakuu,

Wakati kolimba alipotoa kauli ya kwamba CCM imepoteza dira aliitwa na kamati kuu ya CCM na mwisho wa yote tulikuja kuambiwa alikuwa na aneurysm ambayo ilipasuka tumboni baada ya presha kupanda baada ya hapo kilichotokea wote tulisema RIP.

Sasa naomba tujikumbushe waliokuwepo kwenye kamati kuu Ile ya kolimba, Mimi nitaanza kwa kuwataja baadhi ya wajumbe wa wakati ule ili kuweka kumbukumbu vizuri na tuwe na calculated guess ya kitakachotokea kwenye kamati kuu hii iliyowaita kinana, makamba na membe
1. Mkapa
2. Mangula etc
3.
4.
etc

Paul Kistiki
 
Nimekumbuka miaka ile aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba aliposema CCM imekosa dira

Historia imejirudia,ila sasa wameitwa makatibu wakuu wawili,Makamba na Kinana wakajieleze

Mh. Kolimba alishaitwa mbele za haki, apumzike kwa amani
Ila kwa Makamba watachemka kama wakitaka kuketa miyeyusho ile waliyomletea Kolimba wataishia kumpet pet tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama hakijawahi kumuua mtu kwa kukosoa...Kolimba alikuwa anakifahamu chama ....akiwa siyo kiongozi alidhani angeweza kupambana kwa hoja dhidi ya wenzake...Alipoitwa kujieleza ndipo, nadhani, alipofahamu nguvu ya chama...Simply he couldn't cope with the pressure and also power of the organ-kamati kuu...alizoea kuwahoji wengine lakini alipowekwa kati ili ajieleze hakuchukua muda Aliomba maji na kuomba apumzike kidogo huku akitiririkwa na jasho...that was the end of him....Mungu amlaze mahali pema peponi...Ngoja tuone hawa wengine huku baadhi wakisema wanasubiri barua ya wito kwa hamu...mtakuja kuniambia ...wakiwa nje wanatamba .lakini wakiitwa kujieleza watabadilika mno ndani ya kikao...Baadhi ni lazima wataomba radhi kwa wenzao wanaowahoji...Baadhi hamjui nguvu ya vikao vile...Sisi wengine angalau kidogo tunafahamu ingawa siyo sana...Kamati kuu ya chama siyo chombo cha mchezo mchezo.....wait and see/hear...
Toa matakataka yenu nyie maccm, hamjawahi kuwa na manufaa yoyote nchi hii
 
Ben Kiko, aliniambiwa " ..dogo Jamaa kauwawa Kwa sumu ilopakwa kwenye MIC tena cha ajabu hakuna Mwandishi wa habari alobaki ndani ya ukumbi kushuhudia kikao hicho na hata yeye alokuwa akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu RTD alitolewa nje ya ukumbi huo wa whitehouse, pale Dom....

Aliendelea kusema hicho ndo kilikuwa kikao cha kwanza cha Kamati Kuu ya CCM kumtaka naye atoke nje.....

Hayo ni machache kati ya mengi alonambia BEN KIKO (rip) nikiwa Ofcn kwake pale RTD Dom....

Sent using Jamii Forums mobile app
Balaa
 
Back
Top Bottom