Kumbukizi: Mtifuano wa Tundu Lissu na Anna Makinda Bungeni. Nini cha kujifunza?

Kumbukizi: Mtifuano wa Tundu Lissu na Anna Makinda Bungeni. Nini cha kujifunza?

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Nimeangalia huu Mtifuano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Wakili Tundu Lissu na aliyekuwa Spika wa Tanzania Anna Makinda.

Je, Wabunge na Wanasiasa wa kizazi hiki, kuna cha kujifunza?

Hili lilikuwa bunge la kumi Mkutano wa kumi na nane na kikao cha tatu wabishana kuhusu hoja ya dharura

=====

KUMBUKIZI

======

Alhamis, January 29, 2015

HOJA YA DHARURA: WABUNGE WATAKA WAZIRI MKUU NA CHIKAWE WAWAJIBISHWE

BAADHI ya wabunge waliochangia hoja ya dharura bungeni leo wamewataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, wawajibishwe.

Hayo yametolewa wakati wa kujadili Hoja ya Dharura kuhusu kupigwa kwa baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) akiwemo mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba na baadhi ya wanachama wake juzi huko Mtoni-Mtongani jijini Dar es Salaam.

SPIKA MAKINDA: Spika wa Bunge, Anne Makinda, alianza kwa kusema kuwa wabunge wachangie hoja hiyo kwa dakika tatu.WAZIRI CHIKAWE: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alianza kwa kusoma ripoti ya serikali kuhusu kilichotokea wakati wa mkusanyiko wa wanachama wa CUF. Alisema jeshi la polisi lilipokea taarifa kuhusu nia ya chama hicho kufanya maandamano na mkutano wa kuwakumbuka wanachama wa CUF waliouawa Januari 27, 2001 huko Zanzibar.

Aliongeza kwamba kutokana na masuala ya kiusalama jeshi la polisi liliona si vyema kuruhusu maandamano hayo lakini wafuasi wa chama hicho waliamua kukiuka amri hiyo na kukusanyika huko Mbagala Januari 27, mwaka huu ambapo walidhibitiwa na polisi.

MWANASHERIA MKUU: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju, aliomba hoja ya dharura kuhusu polisi kuwapiga viongozi na wanachama wa CUF juzi isijadiliwe bungeni maana suala lipo mahakamani.

TUNDU LISSU: Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alianza kwa kukataa wabunge kuchangia mada kwa dakika tatu, akisema Waziri Chikawe alikuwa amepewa dakika 30, na Mwanasheria Mkuu akipewa dakika 15.

Asema sheria inamruhusu mbunge kuchangia dakika zisizozidi dakika 15 hivyo Lissu alisema angetumia dakika 15 ila Spika aliingilia kati na kusema wangetumia dakika 10 na Lissu akakubali.Lissu alisema mrithi wa Werema (Mwanasheria Mkuu wa sasa, Mh. Masaju) si mshauri wa bunge akiongeza kwamba bunge likitaka ushauri litamfuata Katibu wa Bunge.

Aliongeza kuwa ‘waziri wa mapolisi’ (Chikawe) ameongea uongo na kudhihirisha kuwa kauli ya 'Wapigwe Tu' (iliyowahi kutolewa na Waziri Mkuu Pinda bungeni) si ya bahati mbaya.Alisema viongozi wa upinzani wanapigwa kwa kuwa kuna mafasisti serikalini na katika jeshi la polisi akiongeza kwamba kazi ya polisi si kukataza maandamano bali ni kuyaratibu.

Alilijulisha bunge kuwa hivi sasa wapinzani wana kesi nyingi walizofunguliwa na polisi kwa njama wanazozijua na amelitaka bunge kuchukua hatua na kuwawajibisha Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa tukio hilo la juzi.

MHE. HABIB MNYAA: Mbunge wa CUF Mkanyageni, Habib Mnyaa, alisema ombi la kufanya maandamano lilipelekwa tangu Januari 22 na si 27 kama alivyosema Mh. Chikawe, mwaka huu na maandalizi yakafanyika ila jambo la kushangaza ni kwamba taarifa kutoka jeshi la polisi kusitisha maandamano hayo ilitolewa siku yenyewe ya maandamano asubuhi ya Januari 27, 2015.

Alihoji kwa nini nguvu zinazotumiwa na jeshi hilo kuwapiga wanachama wa CUF zisitumike kupambana na majambazi wanaovamia vituo kama kule Ikwiriri na Tanga?Katika kuhitimisha, alitaka jeshi la polisi livunjwe na Waziri Mkuu ajiuzulu.

MBOWE: Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alisema amesikitishwa na taarifa iliyotolewa na Waziri Chikawe bungeni kwani alivyoongea na baadhi ya maofisa wa polisi makao makuu walimwambia agizo la kupigwa wafuasi wa CUF lilitoka ngazi za juu.

Akisisitiza alisema yeye na wenzake wamewahi kushambuliwa mara nyingi na jeshi hilo lakini pamoja na kuripoti kwenye vyombo husika mpaka sasa hakuna ufutialiaji wowote uliofanyika.

Asema baadhi ya wabunge wanacheka bungeni maana hawajawahi kujeruhiwa na polisi na wanaouawa na kupigwa na polisi si ndugu zao.

MBATIA: Mbunge James Mbatia alisema uamuzi uliofanywa na serikali kuikimbizia mahakamani kesi dhidi ya Prof. Lipumba si sahii kwani zilikuwa ni njama za kutaka suala hilo lisijadiliwe bungeni.Hata hivyo, alimshukuru Spika wa Bunge kuruhusu mjadala ufanyike bungeni ambapo alisema ukweli utaliweka taifa letu huru, kwani mtu yeyote anayemwaga damu ya mwenzake ni gaidi na hawezi kuvumiliwa.

Mbatia aliongeza kuwa vitendo hivyo vilivyofanywa na polisi vinajenga uhasama ndani ya taifa letu na akawataka waliohusika katika tukio la juzi wachukuliwe hatua kali za kisheria na za kijeshi kwa kukiuka maadili ya polisi.
 
Salaam Wakuu,

Nimeangalia huu Mtifuano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Wakili Tundu Lissu na aliyekuwa Spika wa Tanzania Anna Makinda.

Je, Wabunge na Wanasiasa wa kizazi hiki, kuna cha kujifunza?

Hili lilikuwa bunge la kumi Mkutano wa kumi na nane na kikao cha tatu wabishana kuhusu hoja ya dharura
View attachment 3186323
Tundu Lissu amemkumbusha Kanuni pamoja na umuhimu wa jambo lenyewe kwa Taifa.

Atleast Mh Anna Makinda ameonesha uzalendo na Wisdom.
 
Salaam Wakuu,

Nimeangalia huu Mtifuano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Wakili Tundu Lissu na aliyekuwa Spika wa Tanzania Anna Makinda.

Je, Wabunge na Wanasiasa wa kizazi hiki, kuna cha kujifunza?

Hili lilikuwa bunge la kumi Mkutano wa kumi na nane na kikao cha tatu wabishana kuhusu hoja ya dharura
View attachment 3186323
My problem with Lisu is how he is handling/presenting his demands. Analeta hoja kwa kukigawa chama chake, kukiua , kukipasua vipande viwili!
 
My problem with Lisu is how he is handling/presenting his demands. Analeta hoja kwa kukigawa chama chake, kukiua , kukipasua vipande viwili!
Mtoto wa Mbowe utapata shida sana.

Anachodanya Lissu ndio kinatakiwa kufanyika kwenye Taifa, Chama na hata kwenye ngazi ya Familia.

Ukweli na uwazi.

Bahati Mbaya wafrika hatupendi hilo na tutazidi kudidimia miaka nenda miaka rudi
 
20241218_051429.jpg
 
Ukweli bila ushahidi? ametoa ushahidi gani? Unajua nyinyi mna argue kama layman.......ushahidi gani ameutoa? it is just revelations......submissions.......

Finaly ndio nyini kama Lisu, kuropoka....sasa mambo ya mtoto wa Mbowe yanatoka wapi? Is that the argement on the table? Basi mimi ni mtoto wa mama yako wa mwisho
 
Salaam Wakuu,

Nimeangalia huu Mtifuano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Wakili Tundu Lissu na aliyekuwa Spika wa Tanzania Anna Makinda.

Je, Wabunge na Wanasiasa wa kizazi hiki, kuna cha kujifunza?

Hili lilikuwa bunge la kumi Mkutano wa kumi na nane na kikao cha tatu wabishana kuhusu hoja ya dharura
View attachment 3186323
Huyu Spika ingalau alikuwa mvumilivu na mwelewa kidogo....

Lakini angekuwa huyu roboti la ikulu aliyepo sasa Dr Tulia Ackson, kwa mgomo wa Tundu Lissu alioufanya hapa kwa kusisitiza kanuni zifufuatwe, angesababisha bonge la vurugu na mwisho wanaishia kwenye kamati ya kinga na maadili ya Bunge...

Tundu Lissu mtu wa sheria, utaratibu na kanuni...
 
Ukweli bila ushahidi? ametoa ushahidi gani? Unajua nyinyi mna argue kama layman.......ushahidi gani ameutoa? it is just revelations......submissions.......

Finaly ndio nyini kama Lisu, kuropoka....sasa mambo ya mtoto wa Mbowe yanatoka wapi? Is that the argement on the table? Basi mimi ni mtoto wa mama yako wa mwisho
Wewe unaposemaga msigwa kanunuliwa mboa huwekagi ushahidi wa kununuliwa kwake?

Unaposemaga bashite no muuaji, mbona huwekagi ushahidi?

Unaposemaga chadema ilishinda uchaguzi 2015 mbona huwekagi ushahidi?

Unaposemaga waziri fulani ni fisadi mbona huwekagi ushahidi?

Ushahidi unautaka akisemwa mbowe tu?
 
Wewe unaposemaga msigwa kanunuliwa mboa huwekagi ushahidi wa kununuliwa kwake?
wapi nimesema hivyo? siwezi kusema upuuzi huo...... Sina ushahidi wa kusema hivyo. fact ni kuwa amehamia CCM, full stop! That is an undeniable fact! sababu za kuhamia huko sizijui, I can only speculat, e which speculation is not evidence!
 
Unaposemaga bashite no muuaji, mbona huwekagi ushahidi?

Unaposemaga chadema ilishinda uchaguzi 2015 mbona huwekagi ushahidi?

Unaposemaga waziri fulani ni fisadi mbona huwekagi ushahidi?

Ushahidi unautaka akisemwa mbowe tu?
sijawahi sema hivyo , labda kwa jokes, but not in a concrete statement. Quote me any such statement!
kuna muda hapa huwa tunaweka mautani..........
 
My problem with Lisu is how he is handling/presenting his demands. Analeta hoja kwa kukigawa chama chake, kukiua , kukipasua vipande viwili!
Sasa mbona CCM wakiteteana tunasema hawana uzalendo kwa kufichiana maovu?. Kwamba kusema Mbowe kakosea A and B hivyo tumchague Lissu aweze kubadili mambo ndio kukigawa chama? Duh
 
Hawa chawa probably walikuwa wanatoka kamasi darasa la pili kule wakati simba anamuelekeza mama spika! Hawajui historia ya hili jamaa wanaona jepesi tu km kina kibajaji wao, wanachonga tu hapa jf leo hii! Huyu ni mwalimu wazee
 
Back
Top Bottom